Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,312
- 152,112
Ukweli ni kwamba mabadiliko ya kweli ya kusafisha nchi hii na kukamata wezi na mafisadi wote wa nchii bila kujali vyeo au nafasi zao katika jamii hayawezi kuletwa na CCM bali yataletwa na wapinzani siku upinzani ukifanikiwa kushika dola iwe ni mwaka 2020,2025,2030 au vinginevyo.
CCM baada ya kugundua kuwa hali imekuwa mbaya kwao kitu kilichopelekea hata mgombea wa uraisi wa chama chao kuzomewa wakati wa kampeni mwaka jana,sasa wameamua kujaribu kujisafisha na kupitia watumishi wa umma ndio wamepata pa kutokea huku kashifa kubwa za mabilioni ya shilingi zikipewa kisogo utadhani fedha zilizopotea kupitia kashifa hizo hazikuwa za walipa kodi wa nchi hii!
Hivi sasa watanzania wanaonekana kufurahia hatua zinazochukuliwa na serikali hii bila kujali kuwa kashifa kubwa kama za EPA, ESCROW, RICHMOND,n.k hazifanyiwi kazi.
Kwanini hali hii:Sababu kubwa ni kuwa, watanzania hawa walishakata tamaa hivyo inabidi washukuru na kufurahia hata kwa kile kidogo kilichopatikana na hiki kidogo si kingine bali ni hatua za Magufuli na serikali yake kujaribu kumaliza uozo uliopo kwa kutumia "selective style" ambayo mpaka sasa haijagusa wanasiasa /vigogo wakubwa.
Yaani hivi sasa watanzania miyoni mwao wanajisemea: "something is better than nothing" hivyo wanashukuru walau kwa hiki kidogo kilichopatikana kwahiyo msifikiri ni wajinga hawayajui yaliyoko nyuma ya pazia ila wanavumilia tu na mtambue mioyoni mwao furaha yao bado haijakamilika.
Watanzania hawa leo hii wanafurahia lakini mimi nawambia wakati unakuja ambao watanzania hawa hawatafurahia tu,bali watafurahia huku wakicheza mdundiko watakapoona "mapapa" wa ufisadi wakipanda mahakamani kujibu tuhuma zao hata wakiwa ni wazee wa miaka 80 na kuendelea na ninaamini wakati huo tutakuwa na katiba mpya ambayo hata kile kinachoitwa "kinga ya raisi" hakitakuwepo katika katiba hiyo na hapo ndio kila mtu atawajibika kwa madhambi yake.
Wakati huo ukifika kila aliehusika katika EPA, ESROW, RICHMOND, KAGODA, MEREMETA, UUZAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI,N.K atabeba mzigo wa wake na hapo ndio tutakuwa tumefikia kilele cha mabadilko tunayoyataka.
"MUOSHA, HUOSHWA."