UKAWA waitisha kikao cha dharura

UKAWA waitisha kikao cha dharura

BREAKING NEWS:UKAWA WAITISHA KIKAO CHA DHARULA KESHO:

Kufuatia hali kuwa tete ndani ya kambi ya UKAWA, viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wanatarajia kukutana kwa dharura kesho kujadili mwenendo wa umoja wao.

Taarifa za ndani ya UKAWA zinasema Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambaye yupo nchini Marekani atalazimika kurudi haraka nchini na inaelezwa huenda akaingia usiku huu au mapema kesho kwaajili ya kikao hicho cha dharura ambacho kitaamua hatma ya umoja huo.

Mbali na Mbowe, timu yote ya kampeni za mgombea urais na mgombea mwenyewe pamoja na mgombea mwenza wanatarajia kusitisha kampeni na kurudi Dar es Salaam kwa siku ya kesho hadi watakapopata mwafaka wa masuala yanayobishaniwa ndani ya umoja huo.

Taarifa zinasema, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi wa CUF kulalamikia kutotimizwa kwa makubaliano yaliyofikiwa wakati wanaungana na kupjnga jinsi Chadema wanavyoendesha umoja huo hadi kufikia hatua ya mgombea mwenza wa Chadema Juma Duni kutangaza kujitoa kwenye chama hicho na inaelezwa kikao hicho kitatumika kumuomba asijitoe.

CUF wanalalamikia UKAWA kuendeshwa na mtu mmoja ambaye ni Mbowe badala ya kuendeshwa kama taasisi na amekuwa akichukua maamuzi bila kushirikisha wengine.

"UKAWA ni Mbowe na yeye ndo anaendesha mambo anavyotaka kwa maslahi yake na mkwewe mzee Mtei. Huu ni uhuni ambao tulikuwa tunausikia tu ila leo tunajionea baada ya kuingia ndani" alisema kiongozi mmoja wa CUF ambaye alisisitiza kama Mbowe lengo lake lilikuwa ni kuua CUF amefanikiwa ila dhambi hiyo itamtafuna na watahakikisha Chadema haibaki salama.

Hakuna breaking news hapo Lowasa anaendelea na safari yake ya kikazi Dar
 
Babu Duni leo alikuwa viwanja vya Barafu Mburahati na Jumapili atakuwa mkoa wa Manyara Katesh Hanang.
Una lingine la kuzusha!?

Huwa mnakosa la kujitetea? Moshi huo unafuka, tunawasubiri tu, halafu mje tena na utetezi🙂 Sijui mtasema nini tena!
 
Washapigwa asubuhi kama wataendelea na migogoro yao. Tatizo ni tamaa ndo inayowasumbua hawa viongozi, wanachama nao ndo fuata upepo, mbaya zaidi ukiwauliza kwa nini mzee hakuna jibu la msingi zaidi ya kutamka mabadiliko.

Na wewe tukikuuliza kwanini CCM? naomba majibu
 
Nakwambia lowasa anasaidia kuongeza viti vya urais wala sio kuwa rais, na snayebisha akiwa rais animate kichwa

Nakushauri bure panda daladala alafu sema hayo maneno yako kitakachokutokea utakuja kutujuza
 
Bilion 150 za ccm kazini, hata Wawanunue wote Mabadiliko lazima, Ccm mwisho wao umefika, Lowassa Ikulu full stop!!
 
Tehtehteh hivi unachoongea una uhakika nacho au unaongea tu kujifurahisha?! Ukweli ni kwamba ukawa hali ni tete na mbowe ndo kawafikisha hapo.. Sometimes mkubali kupikea ukweli mchungu. . Usijifanye hujaona jana walichokifanya viongozi wa nccr... Au wao sio ukawa?? Na Duni je, kaishia wapi?? Think BIG..

Mwache atufikishe popote sisi ni Lowasa tu
 
Back
Top Bottom