Hamjajipanga vizuri kitengo cha propaganda, kupost thread zaidi ya kumi haimaanishi ndo utakuwa unaweza propaganda saaaaana mpaka uwafurahishe mabosi wako, ila kinachotakiwa ni contents tuu ili uweze kuwanasa wale wasio na vyama, ingependeza kuhubiri Sera na ilani ya chama. Bado namkumbuka sana Tambwe Hiza, Mkuu wa Polisi Mahita enzi za visu vya CUF, hao ndo walikuwa wanajua maana ya propaganda haswaaa. Sasa nyie mnashindana thread na post nyingi as if mnalipwa kutokana na thread mnazoanzisha kukiponda chama Fulani.
Amkeni, Wapiga kura wengi hawana chama, wanataka Sera mbadala.