UKAWA vs CCM katika urais, piga Kura hapa

UKAWA VS CCM KATIKA URAIS

  • UKAWA

    Votes: 757 85.2%
  • CCM

    Votes: 118 13.3%
  • NONE OF THE ABOVE

    Votes: 13 1.5%

  • Total voters
    888
Status
Not open for further replies.
Lowasa hata akishinda sio kwamba ndo neema kwa taifa
tunaweza juta kuzaliwa.....miminaona hao undecided ni very very smart people
The Boss kila nikifatilia post zako nimegundua wewe ni gamba

Shame on you
 
Last edited by a moderator:
mtashangaa ccm tutakavyokabidhiwa nchi,nyie wachache mnaoandika hapa jf ndo ukawa ila wengi ambao hawaijui hata jf wote ni ccm!
 
Wanajamvi!
Tuko katika kipindi ambacho mijadala mikubwa katika maeneo mengi hapa nchini ni suala la uchaguzi mkuu na hasa katika nafasi ya urais. Inavyooneka ni kwamba mmoja kati ya Lowasa au Magufuli atashinda nafasi hii kubwa ya uongozi hapa nchini. Hii ni kutokana na mijadala na mivutano ya wengi iko juu ya hawa watu wawili.

Magufuli amekuwa akitajwa na wengi kwamba ni mchapa kazi lakini pia ni mtu anayesimamia sera na sheria lakini anatoka katika chama ambacho kwa miaka mingi kinatuhumiwa kwenye suala la ufisadi na kushindwa kuwa na vipaumbele katika suala la maendeleo ya taifa letu na mahitaji ya wakati huo. Kwa hiyo kuna watu wanaoona kuwa sasa hivi kipaumbele kiwe ni kuitoa CCM madarakani bila kujali mgombea wao ni mtu wa aina gani.

Lowasa pia amekuwa akitajwa na watu wengi kuwa ni mchapa kazi na mtu mwenye maamuzi magumu (sijayajua haya maamuzi magumu ni yapi, huenda ni kujiuzuru uwaziri mkuu ndo maamuzi yenyewe magumu). Kwa upande mwingine Lowasa amekuwa akitajwa mara nyingi sana kwa suala la ufisadi (sijui kama ushahidi upo au haupo) na hata matumizi makubwa ya pesa katika harakati za kuusaka urais. Huyu ndiye mgombea wa urais aliyesimamishwa na Chadema na hata UKAWA nzima imekubaliana. Chadema na UKAWA nzima siku zote wamekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi na kumtaja Lowasa kama Fisadi hali inayowafanya baadhi ya watu washindwe kuiamini tena chadema katika yale wanayoyasema siku zote hasa pale wanapojitokeza leo na kusema "Lowasa siyo fisadi".

Mimi ni mmoja wa watu waliobaki njia panda ya kufanya maamuzi ya "nimpigie nani kura ya urais". Naomba tujadili kwa pamoja bila ushabiki kwa masilahi ya taifa letu, kizazi chetu na kizazi kijacho; Ni lipi bora, kumchagua Lowasa na tuhuma zake zote akiwa Chama kinachopiga vita ufisadi au kumchagua magufuli ambaye hana tuhuma za ufisadi (kama anazo hazijulikani sana) lakini anatoka chama kinachotuhumiwa kwa ufisadi?

hapa ni ukawa tu aka mamvi
 
Shirika la New Deal Africa kupitia mtandao wake wa Easypolls.com wanaendesha utafiti (opinion poll) kwa wagombea Urais nchini Tanzania waliojitokeza hadi sasa ambao ni Edward Lowassa wa (CHADEMA /UKAWA) na John Magufuli (CCM).

Hadi leo jioni matokeo ya mtandao huo yanaonesha kuwa uchaguzi ungefanyika leo Lowassa angeshinda kwa 64%, na Magufuli angefuatia kwa 31%, huku 5% ya wapiga kura wakiwa hawajaamua wampigie nani kati ya Lowassa na Magufuli.

Bila shaka hawa ni wale wanaosubiri wagombea wa vyama vingine wajitokeze. Kwa maana hiyo ni kwamba wagombea watakaojitokeza kupitia ACT, TADEA, CHAUSTA, na vyama vingine watagawana 05% ya hao "undecided".

Nawe pia unaweza kupiga kura yako na kumchagua Rais umtakaye kwa kubofya hapa

View attachment 274429

Mbonahiyo inaonyesha tofauti na hii
Poll - EasyPolls.net
 
Utafiti wa mwanzo walio ongoza ilikua ni lowasa na Dr slaa na aliye ongoza alikua ni lowasa utafit huo kwa sasa nikama umekufa kwan kuna mpya imejitokeza na sura Moja haipo itakua vyema kama mtafanya tafit nyingine kama mlivyofanya apo awali
 
Wanajamvi!
Tuko katika kipindi ambacho mijadala mikubwa katika maeneo mengi hapa nchini ni suala la uchaguzi mkuu na hasa katika nafasi ya urais. Inavyooneka ni kwamba mmoja kati ya Lowasa au Magufuli atashinda nafasi hii kubwa ya uongozi hapa nchini. Hii ni kutokana na mijadala na mivutano ya wengi iko juu ya hawa watu wawili.

Magufuli amekuwa akitajwa na wengi kwamba ni mchapa kazi lakini pia ni mtu anayesimamia sera na sheria lakini anatoka katika chama ambacho kwa miaka mingi kinatuhumiwa kwenye suala la ufisadi na kushindwa kuwa na vipaumbele katika suala la maendeleo ya taifa letu na mahitaji ya wakati huo. Kwa hiyo kuna watu wanaoona kuwa sasa hivi kipaumbele kiwe ni kuitoa CCM madarakani bila kujali mgombea wao ni mtu wa aina gani.

Lowasa pia amekuwa akitajwa na watu wengi kuwa ni mchapa kazi na mtu mwenye maamuzi magumu (sijayajua haya maamuzi magumu ni yapi, huenda ni kujiuzuru uwaziri mkuu ndo maamuzi yenyewe magumu). Kwa upande mwingine Lowasa amekuwa akitajwa mara nyingi sana kwa suala la ufisadi (sijui kama ushahidi upo au haupo) na hata matumizi makubwa ya pesa katika harakati za kuusaka urais. Huyu ndiye mgombea wa urais aliyesimamishwa na Chadema na hata UKAWA nzima imekubaliana. Chadema na UKAWA nzima siku zote wamekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi na kumtaja Lowasa kama Fisadi hali inayowafanya baadhi ya watu washindwe kuiamini tena chadema katika yale wanayoyasema siku zote hasa pale wanapojitokeza leo na kusema "Lowasa siyo fisadi".

Mimi ni mmoja wa watu waliobaki njia panda ya kufanya maamuzi ya "nimpigie nani kura ya urais". Naomba tujadili kwa pamoja bila ushabiki kwa masilahi ya taifa letu, kizazi chetu na kizazi kijacho; Ni lipi bora, kumchagua Lowasa na tuhuma zake zote akiwa Chama kinachopiga vita ufisadi au kumchagua magufuli ambaye hana tuhuma za ufisadi (kama anazo hazijulikani sana) lakini anatoka chama kinachotuhumiwa kwa ufisadi?

Tunampigia Magufuli matokeo
 
Ukiyatafuta hayo ya pronouns huyo pombe ndo hajui kabisa kwa kuchapia yuko vzr kshenz.
 
Hata wewe bila shaka ungependekeza aliye zaidi kishabikı.Jipeni moyo lakini rohoni mnajua Lowasa hafai na hawezi.Na kwa jinsi mlivyochemka kumkarıbisha Edo, mtapungukiwa hata viti vya ubunge mlıvyokuwa navyo,I can bet.

Tukutane October 25
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom