DuppyConqueror
JF-Expert Member
- Mar 30, 2014
- 9,466
- 6,970
Kwa bandiko hili MMM amejitangaza rasmi kuwa adui wa mabadiliko. Kumbe zile ngoja ngoja, subiri subiri na kauli zinazofanana na hizo zilikuwa ni ishara ya kutumikia kusudi lililo kinyume na shauku ya watu kupata mabadiliko
UKAWA sasa imekuwa ni IKAWA! Vyama vitatu vinavyounda ushirikiano huu wenye mashaka tayari vimekuwa na matatizo na viongozi wao wajuu kisa UKAWA. Imekuwa hivyo kwa CHADEMA - na kuondoka kwa Dr. Slaa - Katibu Mkuu, CUF - kwa Prof. Lipumba (Mwenyekiti) na sasa NCCR-Mageuzi na malalamiko ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kuhusiana na dubwasha hili.
Kuna ushirikiano wowote unaokosa misukosuko?
Tena mbaya kwenye siasa ambayo Chama Dola ina miaka 50 madarakani?
Kuna tofauti gani ya mazingira ya siasa ya sasa na za enzi ya UKoloni?
Hivi bado unaamini huku kote na mawazo huru ya mtu mmoja mmoja ?
Hivi mfano wa Kipenzi chako Dr hakujatosha kupa jibu kuwa Chama dola imeshaanza kutumia nguvu ya pesa?
Kimsingi sasa UKAWA imekuwa IKAWA kwani itakuwa ni shida nyingine ambayo hata hatujaifikiria sana; kwamba tayari vyama hivi vina migogoro ya ndani kuhusiana na ushiriki wao kwenye UKAWA na wengine kwa maamuzi ya kusimamisha wagombea mbalimbali. Ngoma yote itakuwa chungu pale baada ya Uchaguzi vyovyote itakavyokuwa - wakishinda CHADEMA na wagombea wake au wakishindwa kutakuwa na matokeo kwenye vyama hivi vikuu.
Kwa hiyo CCM ikishindwa hakuna matokeo?
Hivi kwenye mechi si kuna anayeshinda na anayeshindwa?
Mzee Mwanakijiji ungeonekana wa maana kuhamasisha mabadiliko kupitia chama mbadala na Ukawa..badala yakutumia nguvu nyingi kuuponda huku ukiacha room kwa ccm kuendelea ...
Sio muungano wa Kilaghai tuliutarajia wengi, sio muungano wa kusigina Democrasia, kwa hali ilivyo sasa utaita muungano au "Genge" no planning, no strategy, no leadership..no reasoning, no motive, no ambitions, no mission, no vision ni uhuni na utapeli wa hali ya Juu, Chadema ikishinda uchaguzi Tz itakua ni Nchi inayoongozwa na Majuha Duniani elewa katiba iliyopp niya 1977 hebu nipangieni Baraza la Mawaziri la hawa matapeli usinitajie Mnyika,Sugu, Nyerere, Mbowe,Msigwa, Lema etc hawana sifa zote za kua viongozi.
Too low Mwanakijiji, kwani pilipili usioila yakuwashia nini?
Kura yangu ni mabadiliko.
Wanageuza watanzania kama chapati. Ila baadhi ya wanasiasa wamekimbilia UKAWA iwe sehemu ya wao kujificha.team lowasa na uzushi hamjambo.
nakumbuka 1995 mlimzushia sumaye ana tilioni kadhaa nje ya nchi.
Leo kawa rafiki wa kuwakomboa watz
Dubwasha hili linaundwa na vyama vinne; vitatu kati ya hivyo ni vikubwa na vina historia ndefu tu ya upinzani Tanzania. Nimeliita "dubwasha" siyo kama kejeli bali ni kitu ambacho huwezi kukielezea kikaeleweka. SIyo chama, siyo muungano, siyo umoja ni ushirikiano tu fulani hivi ambao unataka kutuaminisha kuwa unataka kuja kuongoza Taifa. Kwa muda mrefu wapo watu ambao wameushabikia sana kiasi kwamba wanafikiria UKAWA ni kama chama cha siasa fulani hivi au kina mgombea au wagombea katika Uchaguzi. Kumbe UKAWA siyo chama cha siasa na hakina wala hakiwezi kuwa na Ilani, Sera, wagombea n.k.
Lakini ambacho kimethibitika mapema sasa na wengine tumeonya tangu kuundwa kwa hili dubwasha ni kuwa UKAWA unajiandaa kutuletea matatizo; tayari mengine tumeyaona na mengine yameashiriwa tu. Baada ya uongozi wa NCCR-Mageuzi nao kuja na kulalamikia dubwasha hili nimejikuta nikisema kuwa hili sasa siyo tena UKAWA bali ni IKAWA
UKAWA sasa imekuwa ni IKAWA! Vyama vitatu vinavyounda ushirikiano huu wenye mashaka tayari vimekuwa na matatizo na viongozi wao wajuu kisa UKAWA. Imekuwa hivyo kwa CHADEMA - na kuondoka kwa Dr. Slaa - Katibu Mkuu, CUF - kwa Prof. Lipumba (Mwenyekiti) na sasa NCCR-Mageuzi na malalamiko ya Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kuhusiana na dubwasha hili.
Kimsingi sasa UKAWA imekuwa IKAWA kwani itakuwa ni shida nyingine ambayo hata hatujaifikiria sana; kwamba tayari vyama hivi vina migogoro ya ndani kuhusiana na ushiriki wao kwenye UKAWA na wengine kwa maamuzi ya kusimamisha wagombea mbalimbali. Ngoma yote itakuwa chungu pale baada ya Uchaguzi vyovyote itakavyokuwa - wakishinda CHADEMA na wagombea wake au wakishindwa kutakuwa na matokeo kwenye vyama hivi vikuu.
Fikiria kwa mbali tu ije itokee wajaribu kuunda Baraza la Mawaziri...!!!
Wanachama wa vyama hivi huko waliko nina uhakika wanaangalia kwa makini yanayoendelea kwenye vyama vyao; ukimya wao sidhani kama ni woga...
Na Itakuwa IKAWA kweli kweli...
NLD peke yao inaonekana ndio wamenufaika zaidi na dubwasha hili!
MMM
Mkuu Mzee Mwanakijiji, ulikuwa ukitetea ustawi wa demokrasia na kutaka mabadiliko ya uongozi hapa Tanzania na kwingineko. Umekuwa ukiwataka wapinzani waungane ili wawe na nguvu kwenye uchaguzi na kuweza kuiondoa Serikali iliyo madarakani kwa njia ya kura. Leo hii unaita UKAWA dubwasha!? Nini kimekupata kaka? Ndawakiki wikita naa?
Mzee Tupatupa
Baada ya uchaguzi heshima ya huyu Mwanakijiji hapa jamvini itakuwa imeharibika kabisa
Mkuu Vuta Nkuvute pesa ni sabuni ya roho, waswahili wanasema, penye udhia penyeza rupia na hakika imeweza kupenya kwa huyu mzee wa ughaibuni. RIP MMM