UKAWA mko wapi? ya Dar,Tanga na Kilombero Itisheni Press mtujuze

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,335
72,799
Sasa hivi imekuwa fasheni wabunge wetu kukamatwa hasa maeneo niliyotaja kwenye uchaguzi ambao ni dhahiri Ukawa wana uwezo wa kupata meya.

Ajabu viongozi wa juu mko kimya kwa nini? Mumechoka na kuona bora liende? Wananchi ndio waliowachagua madiwani kwa nini wanyimwe haki yao ya kuongoza hizo halmashauri?

Nawashauri muitishe press tena live coverage kwenye Tv zetu na kutueleza kwa nini wabunge wetu wananyanyasika kiasi hiki?

Hivi kweli miaka ijayo watu watajitokeza kugombea kwa vyama vyetu kama mateso ndio haya?

Kimya chenu kinatutia hasira sana na sisi hatuwezi kukubali unyonge huu abadani.

PSE haraka sana tuambieni na taifa lijue maana wapo wanaoaminishwa kuwa wabunge wa Ukawa ni wakorofi na kupoteza maana ya wanachopigania.
 
Ccm ni sawa na mtoto mlafi na mroho anayetumia kila hila ili ale Chakula chote peke yake, kwa hiyo viongozi wetu wa ukawa wanatafakali kwa hekima na busara kabla ya kuchukua hatua maana mtoto huyo mlafi kapewa rungu
 
Huko ccm Kuna Mitezi dume halafu badala ya kuipeleka
Syria ikatumbuliwe wanahangaika na
Vijipu visivyo na madhara.
 
Ni dhahiri kabisa kuwa hivi vioja vinavyofanywa na viongozi wa CCM kung'anh'ania kwa lazima kupata Umeya jijini Dar, ndiko kutakakokipeka kuzimu chama hicho kikongwe hapa nchini.

Kwa kuwa wamejaribu kwa mbinu zote kuongeza idadi ya madiwani 'mamluki' ambapo mbinu hiyo haikufua dafu.

Wakaja na mazuio mfululizo ya kuzuia uchaguzi huo wa Umeya hadi sasa CCM wameamua 'kupitiliza' na kuja na zuio feki la mahakamani!

Hakika siku Ukawa watakapokuwa wamepata huo Umeya wa jiji la Dar (ambapo sasa ni just a matter of time) na hapo ndipo utakapokuwa mwamzo wa mwisho wa CCM, kutokana na 'dili' za kutisha walizokuwa 'wanachonga' Mameya wa zamani wa jiji hilo.
 
Acha watumie nguvu kutufanyia kila aina ya hila lakini hawawezi kuzishinda nguvu za wakati.
Kuchelewa Ku react viongozi wa juu kunakatisha tamaa wapambanaji wanaokamatwa na kuachiwa kama Dr Besigye wa Uganda.
Nasikia huko Kilombero Mhe Lijuakali na Devota Minja nao wamekamatwa Leo
 
Huko kilombero kwanini madiwani wa ukawa wakubali kushiriki uchaguzi bila wabunge lijualikali na devotha minja?
 
CCM ishajua Watanzania ni watu wa manenomaneno tu, vitendo hamna... Mara oooh ikiwa hivi hapatalika, end of the day kila mtu anajificha ndani mwake akitegemea mwenzie ndo atafanya. So wanatumia hiii karata vizuri, mtalalamika siku mbili halafu kimyaa...


Generation ya kuitoa CCM madarakani bado saaana.

Tutulie tu dozi iingie.
 
Ukimya huu utaiponza Ukawa at high cost. Iteni vyombo vya habari wekeni kila kitu wazi Mwisho mtumieni mkuu wa nchi ujumbe 'Angalisho' '
 
Back
Top Bottom