UKAWA mko wapi? ya Dar,Tanga na Kilombero Itisheni Press mtujuze

Tulizoea kuona Chadema ambayo ikitokea kitu cha uonevu dhidi ya wananchi maandamano yataitishwa na hata polisi wakigoma tutaandamana. Hata kama Polisi CCM wakitanda na magari,mbwa, mabomu lakini lazima tutaandamana hata kama tunapigwa na kuuwawa.

Tangu uchaguzi umalizike, na matokeo tuliyoyaona kuwa CCM hawakushinda. Lakini viongozi wameshindwa hata kuitisha mikutano hata Kutueleza yaliyotokea. Tuachane na ilo la uchaguzi, sehemu zote tulizoshinda tukishirikiana na wenzetu tunanyang'anywa ushindi na tupo kimya hata kuitisha maandamano ili sisi wananchi tudai haki Yetu mnakaa kimya.

Jana mbunge anakamatwa na kulazwa ndani mpaka ninapoandika mko kimya. Mbunge Halima Mdee anajulikana anapokaa ni mbunge hawezi kutoroka lakini polisi ccm wamweka ndani tangu jana utafikiri jambazi.

Chadema mmekaa kimya, inavyoonekana baadhi ya viongozi wameridhika na vyeo vyao hawataki tena kuwatetea wananchi. Mnategemea kuwa mtapata haki kwa kupiga kelele kwenye spika. Swala la umeya mlishajua itakavyokuwa na kweli yakatokea mmefanya nini mpaka sasa zaidi ya Wabunge wenu kuwekwa ndani.

Mnaogopa nini wananchi kuandamana na kudai haki zao?? Nyie ndio viongozi na Chadema ni chama na ipo kihalali. Mnaogopa nini???

Mnakaa kimya hata tamko la Zanzibar mko kimya mnaruhusu MACCM kurudia uchaguzi. Kwanini msiwashitaki kwa wananchi ili tuandamane kudai haki zetu.

Chadema niambie ni nchi gani ambayo imepata Demokrasia bila kumwaga damu, bila baadhi yao kufa kwa ajili ya wenzao.

Bila baadhi Yetu kufa au kumwaga damu hakutakuwa na haki wala Demokrasia katika nchi hii. Kwani bado kuna baadhi ya watawala ambao bado wanaamini kuwa watanzania wote ni CCM na usipokuwa CCM WEWE SIYO MTANZANIA. Yote wanayoyafanya ni kulinda maslahi yao pamoja na familia zao.
Chadema/Ukawa AMKENI SASA NAONA BADO MMELALA. Mlishinda kwenye uchaguzi mkaogopa kudai haki eti mnaogopa kufa kwani nchi zingine wanao kufa kwa ajili ya wenzao siyo nchi. Mnategemea mngekataa uonevu leo hii Tanzania ingekuwa na hizi figisu figisu. Nchi ingekuwa shwari na heshima kwa kila mtanzanzani. Uku tukiomboleza vifo ya baadhi ya mashujaa wetu waliopoteza maisha kwenye kudai haki.

BINADAMU UMEUMBWA KUFA HATA UFANYE NINI UTAKUFA TU.
Lakini hakuna kifo kizuri kama ya kuitetea familia yako na nchi yako. WATAWALA WA CCM WANAJIONA MIUNGU WATU. BILA KUKOMAA TUTAZIDI KUNYANYASIKA KATIKA NCHI YETU.
 
Mkuu busara I2umike procedure Za dhamana zifanyike aachiwe huru mbunge Na lawyer kama Halima hawezi kujamp bail Na kushindwa kufika mahakamani
 
Here we go again, ukawa na siasa za TV na Magazeti, huku kenya wakiendelea kujimegea nchi, olduvai ishakua yao baada ya kuimaliza kilimanjaro, sasa tusubirie zanzibar nayo itatajwa kua ipo kenya mda si mrefu....
 
Hizi figisufigisu za ccm katika uchaguzi wa mameya Na wenyeviti wa halmashauri zitatufikisha pabaya.
 
Wale wabunge wote wa Chadema ambao waliona aibu kumuunga mkono Lowasa, na wale waliokuwa wakaribu na Dr Slaa, chama kimeamua kuwatoa mhanga. LOWASA na Mbowe hawana time nao . Masikini kubenea ameponzwa kufungwa pamoja na Mdee.
 
Ukimya huu utaiponza Ukawa at high cost. Iteni vyombo vya habari wekeni kila kitu wazi Mwisho mtumieni mkuu wa nchi ujumbe 'Angalisho' '

Mkuu wa nchi gani wakati hawamtambui? Labda wamtumie Kikwete ujumbe!
 
Sasa hivi imekuwa fasheni wabunge wetu kukamatwa hasa maeneo niliyotaja kwenye uchaguzi ambao ni dhahiri Ukawa wana uwezo wa kupata meya.

Ajabu viongozi wa juu mko kimya kwa nini? Mumechoka na kuona bora liende? Wananchi ndio waliowachagua madiwani kwa nini wanyimwe haki yao ya kuongoza hizo halmashauri?

Nawashauri muitishe press tena live coverage kwenye Tv zetu na kutueleza kwa nini wabunge wetu wananyanyasika kiasi hiki?

Hivi kweli miaka ijayo watu watajitokeza kugombea kwa vyama vyetu kama mateso ndio haya?

Kimya chenu kinatutia hasira sana na sisi hatuwezi kukubali unyonge huu abadani.

PSE haraka sana tuambieni na taifa lijue maana wapo wanaoaminishwa kuwa wabunge wa Ukawa ni wakorofi na kupoteza maana ya wanachopigania.

fvck ukawa!
 
Wale wabunge wote wa Chadema ambao waliona aibu kumuunga mkono Lowasa, na wale waliokuwa wakaribu na Dr Slaa, chama kimeamua kuwatoa mhanga. LOWASA na Mbowe hawana time nao . Masikini kubenea ameponzwa kufungwa pamoja na Mdee.
 
Sasa hivi imekuwa fasheni wabunge wetu kukamatwa hasa maeneo niliyotaja kwenye uchaguzi ambao ni dhahiri Ukawa wana uwezo wa kupata meya.

Ajabu viongozi wa juu mko kimya kwa nini? Mumechoka na kuona bora liende? Wananchi ndio waliowachagua madiwani kwa nini wanyimwe haki yao ya kuongoza hizo halmashauri?

Nawashauri muitishe press tena live coverage kwenye Tv zetu na kutueleza kwa nini wabunge wetu wananyanyasika kiasi hiki?

Hivi kweli miaka ijayo watu watajitokeza kugombea kwa vyama vyetu kama mateso ndio haya?

Kimya chenu kinatutia hasira sana na sisi hatuwezi kukubali unyonge huu abadani.

PSE haraka sana tuambieni na taifa lijue maana wapo wanaoaminishwa kuwa wabunge wa Ukawa ni wakorofi na kupoteza maana ya wanachopigania.
CHADEMA haina viongozi wa juu!

Sema hivi "MGOMBEA WETU WA URAIS UPO WAPI"????
 
CCM wanapima "upepo" kwa kuwachokonoa UKAWA ili wakurupuke kuitisha "Press Conference" ili wajue ya moyoni mwao.Msione kobe ameinama...mjue anatunga sheria!!Hata ukimya nalo ni jibu tena MUJARABU.
 
Du! haya mambo yanasikitisha na kuliza sana, Mungu wetu kwa nini unatuacha? movu haya ya ccm mpaka lini jamani? Kwa nini serikali haiingilii kazi ya huu udhulumaji? Viongozi hebu toeni tamko why watu wanaonewa mko kimya? kwa nini haya?
 
Matendo ya CCM ni chukizo kubwa mbele ya Mungu, Matendo yao hayana tofauti na matendo ya shetani. Matendo haya hunifanya kumulaumu mwenyezi Mungu kwa nini aliniumba kuwa Mwaafrika matendo haya katika nchi za Kiafrika (hasa Tanganyika, Zanzibar, Uganda, Rwanda, Burundi, Zimbabwe na South Sudani) yanadhihirisha bila chembe ya shaka Uafrika ni LAANA!
 
Back
Top Bottom