UKAWA limebaki jina? Washindwa kukubaliana kuhusu wagombea udiwani

Vyama vinavyounda UKAWA vimeshindwa kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja katika kila kata 20 ambazo uchaguzi wake unafanyika tarehe 22 January 2017.

Kampeni za uchaguzi zimeanza jana tarehe 23 Desemba na zitamalizika tarehe 21 January 2017.

Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye maeneo hayo.

Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha mgombea wetu eneo hilo.

Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.

“Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.

Akatanabaisha kuwa CUF lazima itachukuwa kata hiyo na kazi ndio imeanza ya kuhakikisha kata inaingia mikononi mwetu tukiwa na lengo la kukijenga chama ili kuhakikisha mwaka 2020 tunakuwa na viti zaidi vya udiwani na ubunge katika jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

“Tumekuwa tukiongea kweye vikao bila hatua kuchukuliwa na wenzetu wamekuwa waongeaji wazuri kwenye vikao bila utekelezaji hali inayotuwiwa vigumu kukijenga chama na kuwa na viti vya wabunge na madiwani katika mkoa huu kutoka na hila za wenzetu”alisisitiza Mwinyi

Orodha ya kata zitakazofanya uchaguzi ni;
View attachment 449762
View attachment 449763
nachoshauri ni kwamba hawa viongozi wa UKAWA wakubaliane kugawana kanda za kufanyia opereshenii ili kila chama kijijenge kwenye maeneo husika kwani itasaidia kila kanda kuwa na chama kimoja cha upinzani chenye nguvu na hicho chama ssa kipewe jukumu la kusimamisha mgombea ubunge na udiwani kwenye maeneo hayo.
kwanni nashauri hivi?? kuanzia 2010-2015 kila chama kilifanta operesheni zake kivyake vyake hivo kujikuta vimeshajijenga na kujenga wanachama wenye nguvu ambao mwishoni walitia nia kugombea kwenye majimbo hayo. sasa ikawa vigumu mtu kumpisha mwenzie maana unakuta kawekeza sana kwenye jimbo hilo to mapema ssa akisema amuachie mwingine ile nguvu yake itakuwa imeenda bure hiyo ilipelekea UKAWA kusimamisha wagombea zaidi ya mmoja.
SULUHISHO: kila chama kipewe kanda,eneo au mkoa wa kufanya operesheni zake mfano hakuna haja ya chadema kupeleka M4c pemba vilevile haina haja ya cuf kufanya mikutano mingi kwenye maeneo kma arusha au kilimanjato ambapo upinzani wa chama kingine tayari umejizatiti nafkiti nimeeleweka na ikiwezekana watia nia wajulikane mapema na waanze kujijenga kupitia vyama vyao mapema ili kuepusha migogoro ya kuachiana majimbo mwishoni
 
CUF not in sound mind at the present , so you can't enter into agreement with a person with an unsound mind or minor . Nccr as well ni wagonjwa refer mwenyekiti wake so you can imagine the situation.
You have point although is half-baked.

Mimi nilidhani walishaingia makubaliano na kilichokuwa kinatakiwa ni utekelezaji.
 
Back
Top Bottom