UKAWA limebaki jina? Washindwa kukubaliana kuhusu wagombea udiwani

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,258
2,000
Vyama vinavyounda UKAWA vimeshindwa kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja katika kila kata 20 ambazo uchaguzi wake unafanyika tarehe 22 January 2017.

Kampeni za uchaguzi zimeanza jana tarehe 23 Desemba na zitamalizika tarehe 21 January 2017.

Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye maeneo hayo.

Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha mgombea wetu eneo hilo.

Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.

“Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.

Akatanabaisha kuwa CUF lazima itachukuwa kata hiyo na kazi ndio imeanza ya kuhakikisha kata inaingia mikononi mwetu tukiwa na lengo la kukijenga chama ili kuhakikisha mwaka 2020 tunakuwa na viti zaidi vya udiwani na ubunge katika jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

“Tumekuwa tukiongea kweye vikao bila hatua kuchukuliwa na wenzetu wamekuwa waongeaji wazuri kwenye vikao bila utekelezaji hali inayotuwiwa vigumu kukijenga chama na kuwa na viti vya wabunge na madiwani katika mkoa huu kutoka na hila za wenzetu”alisisitiza Mwinyi

Orodha ya kata zitakazofanya uchaguzi ni;
uchaguzi.jpg

uchaguzi2.jpg
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,258
2,000
Kwa sasa UKAWA mpaka wanafanyiana udukuzi kati yao hata kwa viongozi wao kama tulivyoona kwa Kafulila.

Maneno ya Kafulila kama alivyonukuliwa na Gazeti la Raia Mwema yanasadifu na kutoa hitimisho kuwa, UKAWA is walking dead.

Kwa mtazamo wa Kafulila, CHADEMA ndio chama pekee cha upinzani chenye malengo, mipango na mikakati ya kuingia Ikulu. Maneno ya Kafulila ni dharau kwa vyama vingine ndani ya UKAWA.

Kafulila alinukuliwa na Gazeti la Raia Mwema akisema;

‘’Sababu kuu ya kuelekea Chadema ni fikra kwamba tukiunganisha nguvu pamoja ya kila mpiganaji kwenye chama kimoja kuhusu mabadiliko tunayotaka na kuamini ndani na nje ya vyama,, safari ya kuhitimisha utawala ulioshindwa kwa zaidi ya nusu karne itakuwa fupi.

Na kwa maoni yangu, chama ambacho kimefanikiwa kujipambanua kama taasisi yenye kiu ya kuondoa utawala huu, ambapo pamoja na kubadili sura na majina ya marais mara tano, bado maisha ya mtanzania yameendelea kuwa nafuu ya jana awamu hadi awamu chama hicho ni Chadema.

CHADEMA, kwa kiasi kikubwa pamoja na vizingiti vingi vya kujenga taasisi ya upinzani kwenye nchi ambayo mfumo mzima wa dola (state) ni wa chama kimoja, bado imeweza kufikia hatua ya kujipambanua kwa kwa kiasi kikubwa kama chama chenye malengo, mipango na mikakati ya kufikia malengo hayo’’.
 

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,523
2,000
Mdudu (lipumba) huyooo mduduu......kaingiaje.....mdudu ndani ya kokwa ya embe.....kaingiaje.......?
 

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,137
2,000
CUF not in sound mind at the present , so you can't enter into agreement with a person with an unsound mind or minor . Nccr as well ni wagonjwa refer mwenyekiti wake so you can imagine the situation.
 

ligema274

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
321
250
Watanzania mpaka sasa hawajui nani anaukoroga UKAWA..Jibu liko vichwani midomoni wanalikwepa .

Jibu ni hili:-
walipoanzisha huu UKAWA walikubaliana vizuri na hoja walikuwa nayo mpaka kufikia muafaka kutoka nje ya BUNGE LA KATIBA..

Wakati wanajadili na kuafikiana hayo kuna Waliokuwa wanaona wamepotoka na hawana maana ni wale wa upande wa CHAMA TAWALA.

Hapo kilichoangaliwa ni MTAJI WA KISIASA baina ya MAKUNDI hayo MAWILI vyama (UKAWA) na CHAMA TAWALA na baadhi ya WAWAKILISHI wa vyama vingine vya UPINZANI ambao WALIWAPINGA kimsimamo (Mrema,Mtikila,Cheyo,Dovutwa nk)

Kwa kitendo cha KUWAPOKEA walioupinga UKAWA MWANZONI na kuwaleta NDANI YA UKAWA kwa minajili ya KUSAIDIA UCHAGUZI 2015 na kuwapa UMUHIMU na USEMAJI ndiyo hasa LILILOITAFUNA,LINALOITAFUNA&LITAKALOITAFUNA UKAWA kwa jambo jepesi tu IMEKUMBATIWA QUANTITY na siyo QUALITY

UKAWA itazame ILIPOJIKWAA siyo ILIPOANGUKIA.


WASSALAAM..lig274
 

kanyela mumo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,037
2,000
CCM chama kubwa, na ukawa ni moja la tawi la CCM.

Ndio maana CCM huita UKAWA ( UKIWA ).

CCM wanajua wanachofanya, UKIWA hawajui wanachofanya ndio maana kila siku wanakuja na sijui MC4 mara 442, mara opareshi sangara, vitu kibao ambayo havina mafanikio.

hivyo hawajui wanachofanya kama vile mtoto Mdogo kila kitu anataka kwa baba yake. Cha msingi fanya kazi acha siasa.

Baba mwenye Nyumba kasema tufanye kazi tuache siasa oohoo shauli yako utakuja kuwapa shida watoto wako za kujitakia kama wewe ulivyo kulia.

Wewe ndio mwenye jukumu la kubadirisha familia yako cha ajabu upo kwenye siasa!! sasa hizo si rahana? Unashinda kutafuta watu wa kuongea bad language kwenye mitandao.

Acheni ujinga fanyeni kazi. Tufanye kazi.
 

kanyela mumo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,037
2,000
Mdudu (lipumba) huyooo mduduu......kaingiaje.....mdudu ndani ya kokwa ya embe.....kaingiaje.......?
Sio mdudu bali anafanya kile anacho stahili kufanya.

Moja ya majukumu yake wala hajatoka njee ya mstari. Wewe ndio mdudu badili ufanye kazi unabaki kushikiwa akili.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,406
2,000
Mdudu (lipumba) huyooo mduduu......kaingiaje.....mdudu ndani ya kokwa ya embe.....kaingiaje.......?
Nilijua Tu.

- Asiporushiwa Lawama Lipumba Basi Ni CCM. Wakihurumiwa Hawa Then ACT Wanakula Lawama

- Chadema Wako Sahihi Siku Zote, Masikini CUF
 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,010
2,000
CUF ipewe kata Arusha?
Arusha kata ipo Rukwa au hii Arusha nayo ijua mm ya Kaskazini?
Mwenye mawazo haya kama CUF iachiwe kata Arusha ana wadudu funza kwenye ubongo wake
 

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
1,856
2,000
Mbona Pwani na Zanzibar huwa wanaachiwa hawa Cuf japokuwa Chadema ni wabinafsi lakini Arusha wana uzito mkubwa ukilinganisha na vyama vingine including Miccm
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom