UKAWA kususia Futari za Viongozi wakuu Mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni jambo la ajabu

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa wasiojua ni nguzo mojawapo kubwa katika Nguzo kuu za dini ya waislam.

Na mwezi huu kwa waislam ni mwezi wa kufututrishana kusamehehana na kuombeana mema. Ata kama mnaugomvi mkubwa wengi huwa wanausubiri kwa ajili ya kusameheana ni mwezi wa rehema kwa waislam, Lakini kwa nchi yetu hatujafikia hatua mbaya ya kususia ata chakula au maji.

Ukawa wanachofanya ni kutaka kutengeneza Chuki baina ya watanzania ifikie hatua hatuzikani kisa siasa, Najiuliza tu km kiongozi wanayeshindana nae hakifiwa na mtu wa karibu yake Je wapo tayari kumsaidia au kumfariji??

Kama wameweza kususia Futari kisa yupo Naibu Spika?
Watanzania je tumefikia hapo?

6.jpg


Mi naomba ili suala ni dogo lakini kwa mkutadha ni kubwa?
wamesusa Futari ya RAISI JOHN POMBE. Unaweza sema ni sawa kutokana na Imani yake

Je kususa Futari ya waziri mkuu?
Si waziri mkuu tu ata akiandaa mbunge wa CCM wanagoma kwenda kula Futari.

NAOMBA TU WABADILIKE ; KUNA MAISHA BAADA YA SIASA . SIASA SI UGOMVI WALA CHUKI.

10.jpg








 
Nani kakudanganya waziri mkuu ni muislamu?,au ukishaona jina tu unatambua ni muislamu?.

Vipi kwani dini ina amuru kuftulisha watu wasio funga?,hata kwa wanaofunga?.

Kwa nini hawaendi kuftulisha watu wasio nauwezo wakupata futuru?.
 
Nani kakudanganya waziri mkuu ni muislamu?,au ukishaona jina tu unatambua ni muislamu?.

Vipi kwani dini ina amuru kuftulisha watu wasio funga?,hata kwa wanaofunga?.

Kwa nini hawaendi kuftulisha watu wasio nauwezo wakupata futuru?.
Mkuu, kwani kwenye mada imeandikwa Waziri Mkuu ni Muislam? Kilichoelezwa ni kwamba futari hiyo iliandaliwa na Waziri Mkuu kwa ajii ya wafungaji ambao ni waislam. Hata Pinda naye alikuwa anaandaa futari. Rais pia juzi kafuturisha pale Ikulu
 
Sasa kama wanasusia bunge watapataje hizo barabara? By the way futari si ishu sana. Muhimu ni pale mnapojumuika na kushirikiana kwenye mambo yasiyo ya kisiasa kama kwenye imani za dini
Ameposema kukataa futuru ya JPM inaweza kuwa sawa kulingana na imani yake, halafu akauliza kukataa ya waziri mkuu je?.

Au umesoma kichwa cha habari tu.
 
Futurisha watu wasio na uwezo hizi mbwembwe nyingine ni upuuzi tu.

Huwezi kuji associate na mchawi kwa sababu tu unakamilisha nguzo za upendo, huo ni unafiki wa kiwango cha hali ya juu! Mimi hata birthday za watoto wa hawa mchwa wa hiki chama kilichokosa dira huwa sihudhuri! Nifikiri itafika mahali hata kuoa kwenye familia ya mwana CCM iwe mwiko!
 
Dhihaka ni kwenda kufuturu wakati mchna umekula kiti moto na bia za kutosha, halafu unashika kijiko cha kuchotea futari amabacho muislam aliefunga kweli anakishika na kuchotea futari. Alikeni watu kwenye sherehe hizi futari wale walio unga.
 
6.jpg

Siasa zinachekesha sana. Tunataka kufanya siasa mpaka kwenye mambo ya kiimani za kidini! Tutalaumiana sana katika dhana ya kufuturisha waliofunga lakini tuangalie ukweli kama ukitaka kupata idadi ya waliofunga ili kutimiza nguzo ya uislamu katika hao waalikwa utacheka sana.
 
Back
Top Bottom