UKAWA kuongea na wanahabari leo saa 8 mchana

UKAWA kuongea na wanahabari leo saa 8 mchana

Status
Not open for further replies.

Prosoo

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
471
Reaction score
167
UKAWA Wataitisha mkutano na wanabari leo saa 8 mchana na utarushwa live na ITV.

Habari za leo, uongozi wa Ukawa utakuwa na Mkutano na Wahariri leo saa 08:00 mchana Bahari Beach Hotel, kuzungumzia masuala makubwa kuhusu uchaguzi. Tafadhali fika bila kukosa.
=========

MBOWE: Ameomba pole kwa kuwashtukiza wanahabari kwa kuwapa taarifa ya ghafla, amemualika Sumaye na anamkaribisha aje kuzumza na wanahari.

Sumaye: Nimewaita juu ya mambo mawili makubwa, moja ni kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa nimejitoa CCM na kuhamia UKAWA. Ile taarifa ilikuwa uongo, niliempa aikanushe alienda mbele zaidi na kusema Sumaye hatajitoa CCM maisha yote, la pili akasema Sumaye atazunguka na Magufuli nchi nzima kumnadi, hili nalo si sahihi. Bado namshukuru ndugu Lema kukanusha taarifa japo aliongezea mambo mawili matatu.

Nina raha Magufuli ndie mgombea kupitia CCM, ninaamini ni mchapakazi japo ana mapungufu yake mengi. Mimi nina tatizo na mfumo wetu au mfumo wao katika uchaguzi, kwa sababu kile chama cha mapinduzi ni cha zamani. Mimi kwa imani yangu na naamini imani ya wengi safari hii yametokea sana katika chama cha CCM. Ni vizuri tuige kwa wenzetu waliokomaa kidemokrasia, binafsi nilitarajia sitafika mbali katika mchakato huo. Tatizo la rushwa katika CCM, hili linathibitishwa na pesa nyingi zilizotumika wakati wa mchakato, watu waliwanunua wapiga kura

MORE UPDATES, tembelea
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ahamia NCCR-Mageuzi Rasmi - Agosti 22, 2015
 
Asante, tunasubiri kwa hamu. Tetesi za mkutano huo wa waandishi wa habari ni nini hasa?
 
asanteni sana makamanda kwa taharifa ila umeme wamesha uchukua,
 
Mada kuu ni nini....nadhani Slaa atakuwa karudi..
 
CCM wanatamani kuifunga ITV,washaianzia figisufigisu!!!

Kama ni ujio wa Sumaye,hii ni nzuri zaidi na ngumi ya Chembe kwa maCCM na kibaraka wao Makufuli!!
 
UKAWA Wataitisha mkutano na wanabari leo saa 8 mchana na utarushwa live na ITV.

======
Habari za leo, uongozi wa Ukawa utakuwa na Mkutano na Wahariri leo saa 08:00 mchana Bahari Beach Hotel, kuzungumzia masuala makubwa kuhusu uchaguzi. Tafadhali fika bila kukosa.

Ahsante mkuu, tunahamu sana ya kusikia kitu toka kwao.
 
Lowassa kishawahishwa Ujerumani nini kwa matibabu zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom