UKAWA kugomea Kamati za Bunge

UKAWA kugomea Kamati za Bunge

badoo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
512
Reaction score
249
Inashangaza sana kuona wabunge wetu tunaowaamini wa ukawa Jana kugoma kuingia ktk kamati walizoteuliwa kwa kudai kuwa sizo walizozitaraji,cha kuchekesha zaidi Mh kubenea baada ya kuona amepangwa ktk huduma za jamii akakasirika na kusikika akisema haiwezekani apangwe huko,kubenea alitarajia atapangwa PAC kitu ambacho kimemkasirisha sana hiyo jana,cha kujiuliza tu kwanini ukawa wagome?

Walijipangia nini ktk nia zao?kwa sheria za bunge PAC lazima iongozwe na mpinzani,je wabunge wa ukawa walioteuliwa kwenye kamati hiyo ya PAC hawana akili na sio watendaji?kwanini kina kubenea na wenzao wasiwaamini wabunge wao?

Sio bure ukawa walikuwa na nia ovu,hakuna hata mbunge mmoja aliejaza kamati alioitaka kisha akapangwa huko,safari hii ni tafauti kabisa,na ukawa takriban wote hakuna aliejaza kamati nyengine zaidi ya PAC na maliasili na utalii,nishati na madini.

Poleni sana kwa kukosa ulaji mlioutarajia pigeni kazi tumewachagua mkatuwakilishe,na mwaka huu mkigoma mara tatu tu unafutiwa ubunge.
 
Inashangaza sana kuona wabunge wetu tunaowaamini wa ukawa Jana kugoma kuingia ktk kamati walizoteuliwa kwa kudai kuwa sizo walizozitaraji,cha kuchekesha zaidi Mh kubenea baada ya kuona amepangwa ktk huduma za jamii akakasirika na kusikika akisema haiwezekani apangwe huko,kubenea alitarajia atapangwa PAC kitu ambacho kimemkasirisha sana hiyo jana,cha kujiuliza tu kwanini ukawa wagome?walijipangia nini ktk nia zao?kwa sheria za bunge PAC lazima iongozwe na mpinzani,je wabunge wa ukawa walioteuliwa kwenye kamati hiyo ya PAC hawana akili na sio watendaji?kwanini kina kubenea na wenzao wasiwaamini wabunge wao?Sio bure ukawa walikuwa na nia ovu,hakuna hata mbunge mmoja aliejaza kamati alioitaka kisha akapangwa huko,safari hii ni tafauti kabisa,na ukawa takriban wote hakuna aliejaza kamati nyengine zaidi ya PAC na maliasili na utalii,nishati na madini.
Poleni sana kwa kukosa ulaji mlioutarajia pigeni kazi tumewachagua mkatuwakilishe,na mwaka huu mkigoma mara tatu tu unafutiwa ubunge.
Wamekwisha kuanza!!!! Kuna wabunge wanajiona zaidi ya wabunge wenzao! Sasa wao wangoje tu wanadhani sasa hivi ni mambo ya kuchjeza rede! Sisi tunataka kazi baasi mambo ya mara wamesusia nini na huku posho hawasusii hatutaki kusikia!
 
Hii habari kama ni ya kweli basi ni ya kufedhehesha sana.......hapa ndipo tunapopata kuona sura halisi za waheshimiwa wetu huko mjengoni....
 
K
Wamekwisha kuanza!!!! Kuna wabunge wanajiona zaidi ya wabunge wenzao! Sasa wao wangoje tu wanadhani sasa hivi ni mambo ya kuchjeza rede! Sisi tunataka kazi baasi mambo ya mara wamesusia nini na huku posho hawasusii hatutaki kusikia!

Kama mlipanga kuwaburuza sasa mtakiona cha mtemakuni nyie ccccccccm, kama mlijipangia kivyenu na kuweka wadhaifu ili mambo yenu yasonge mbele kilaini huu si wakati wake. tunataka usawa na si vinginevyo. Bunge ni la wooote si lenu na marafiki zenu
 
wanagoma nini? upinzani si walisema wabunge wao wote ni wa viwango vya juu kumbe kuna wengine hamuwaamini hasa wa viti maalumu
 
Nitatoa mawazo yangu baada ya kujua sababu hasa ya wao Kugomea.

Kwasasa nasoma kwanza maoni yenu.

Asanteni Sana
 
Nawaunga mkono wabunge wote wa UKAWA kwa hatua hiyo.

Haiwezekani kamati ya PAC kwa mfano spika amejaza wabunge wa CCM kibao.
Kama sio makusudi ni nini??

Wakati huo huo kamati ya kilimo, mifugo na uvuvi ndo amejaza wabunge wa upinzani.

Kwa hiyo kubenea alivyokuwa anajipigia upatu kwenye mitandao na kumchafua Zitto imekuwa kazi bure.

Hili bunge huenda wabunge wa upinzani wakafanya vibaya zaidi kuliko bunge lililopita. ...kama wabunge wenyewe ni a ina ya Kubenea sioni jipya zaidi ya umaarufu binafsi.
 
Duuuhh, kweli kila uchwao watanzania tunazidi kukosa maarifa. Nimeduwaa nikisoma "mada na michango" ya wanajamii forum miaka ya 2012 kurudi nyuma inaonekana kuwa bora zaidi. Mada za sasa na michango ya watu wengi inaonekana kuwa "duni /dhaifu". TUJIPANGE.
 
Kama ni kweli, wamekariri maana ya UPINZANI vibaya, wapinge na wao kuchaguliwa na wananchi kuwa wabunge basi tujue moja.
 
Ni aina ya uandishi lakini nafikiri mleta mada umekosea sana! Hujui kwanini wamegomea lakini umejaribu kuingiza fikra zako za ufitini kati yao kwa muundo wa maswali "je wabunge wa ukawa walioteuliwa kwenye kamati hiyo ya PAC hawana akili na sio watendaji ? Athari ya muundo huu ni kuwafanya watu wajadili zaidi fikra zako ambazo kimsingi sio njema kuliko kutaka kupata uhalisia wa jambo lenyewe. Niungane nawe kuwashangaa wabunge wa UKAWA kama kweli wote walichagua kamati ya PAC!!! Hivi hata Lisu, Mdee au Mnyika waliomba kuwa katika kamati ya PAC??? Nimshangae pia spika kama amempanga Mnyika au Lisu kwa mfano kwenye kamati ya maendeleo ya jamii kwa kuwa wanafani zao; hivyo naungana na wabunge wa UKAWA kugomea uteuzi huo kwa sababu kukosea kwao kuchagua hakuhalalishi au mpa mamlaka spika ya kuwapangia wabunge kiholela bila kufuata taaluma zao au weledi wao.
 
Wamekwisha kuanza!!!! Kuna wabunge wanajiona zaidi ya wabunge wenzao! Sasa wao wangoje tu wanadhani sasa hivi ni mambo ya kuchjeza rede! Sisi tunataka kazi baasi mambo ya mara wamesusia nini na huku posho hawasusii hatutaki kusikia!

Mwana, kwa comment hii siamini kama nawe ni great thinker na zaidi naona kabisa umevamia jukwaa ambalo sio saizi yako hivyo nakushauri kwa wembamba wa akili yako kama sindano na udogo wa fikra zako kama jina lako MWANA it is better urudi fasta facebook kwani naamini huko ndio kwako huku umepotea njia. Siamini kwa mtu mwenye kufikiri vizuri anaweza akasema wabunge wote ni sawa HAPANA wabunge wanatofautiana sana hasa kuanzia upatikanaji wa ubunge wao (MAJIMBO, VITI MAALUM na UTEUZI WA RAISI), wanatofautiana elimu na weledi (KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA, DARASA LA SABA, ELIMU YA JUU PhD, Prof? wanatofautiana uzoefu wa shughuli za kibunge (Kipindi kimoja, viwili, vitatu NK), wanatofautiana uwezo wa kifra na kujenga hoja (Tundu Lissu + Deo Sanga, Mnyika +Lusinde, Zitto+Assumpter Mshama)
 
Inashangaza sana kuona wabunge wetu tunaowaamini wa ukawa Jana kugoma kuingia ktk kamati walizoteuliwa kwa kudai kuwa sizo walizozitaraji,cha kuchekesha zaidi Mh kubenea baada ya kuona amepangwa ktk huduma za jamii akakasirika na kusikika akisema haiwezekani apangwe huko,kubenea alitarajia atapangwa PAC kitu ambacho kimemkasirisha sana hiyo jana,cha kujiuliza tu kwanini ukawa wagome?

Walijipangia nini ktk nia zao?kwa sheria za bunge PAC lazima iongozwe na mpinzani,je wabunge wa ukawa walioteuliwa kwenye kamati hiyo ya PAC hawana akili na sio watendaji?kwanini kina kubenea na wenzao wasiwaamini wabunge wao?

Sio bure ukawa walikuwa na nia ovu,hakuna hata mbunge mmoja aliejaza kamati alioitaka kisha akapangwa huko,safari hii ni tafauti kabisa,na ukawa takriban wote hakuna aliejaza kamati nyengine zaidi ya PAC na maliasili na utalii,nishati na madini.

Poleni sana kwa kukosa ulaji mlioutarajia pigeni kazi tumewachagua mkatuwakilishe,na mwaka huu mkigoma mara tatu tu unafutiwa ubunge.
Watanzania sasa tupunguze UBINAFSI mimi nauona umeenea kwa kila mtu, watu hatuaminiani kabisaaaaa!

Asanteni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom