UKAWA kugomea Kamati za Bunge

UKAWA kugomea Kamati za Bunge

Tarudi baadae kuchangia kiduchu...
 
Hoja zaifu sana kudai wabunge wa upinzani waliowekwa kwenye kamati hizo (PAC & LAAC) Ni wabunge wachanga na hawana uzoefu kwani bunge hili halina uhasiano wa namna yoyote na historia wala bunge lililopita na sifa ya kuwa mjumbe wa kamati au mwenyekiti kikanuni haisemi uwe mbunge kwa awamu mbili au moja, watanzania naomba mtambue wazi kuwa kinachopiganiwa ni masilahi tu na network pana ya wizi wa dhahiri na hivyo unapaswa kukemewa vilivyo.
 
Kwani sheria na kanuni zinasemaje kuhusu nani ana wajibu wa kupanga hizo kamati? Ukawa fuata sheria za bunge wakati mnasubiri kupata speaker wenu.
 
Nimeipenda comment yako!
Kimsingi wapinzani hawana ubunifu, kamati kama hizi za kilimo, huduma za jamii ndizo walipaswa watu kuzigombania kwa maana mnakaa na kufikiri pamoja na serikali!
Haya ndiyo matatizo ya msingi ya watanzania, hapa ndipo maendeleo yanapolengwa, watanzania wanatamani kuona wanapata nafuu ktk maeneo haya lkn wabunge wanataka kuwepo ktk kamati moja tu! Yes usimamizi wa pesa za umma ni muhimu lkn ubunifu katika uzalishaji na kutatua matatizo ya msingi ya wananchi nalo lina umuhimu namba 1.

Nadhani mawazo ya wabunge wetu hasa wa kambi ya upinzani - wamefocus kuibua ufisadi na kuona matumizi ya PAC na serikali za mitaa , wakidhani ndio kazi pekee, wanaweza kuwa sahihi ila wanasahau kufahamu hizi sekta za uzalishaji ni muhimu zaidi kuliko hizo sekta za matumizi wanazozililia.
 
Majukumu ya PAC unayafahamu lakini?

Kwa namna wanavyokuwa na kuenenda wabunge wa CCM ni dhahiri kamati hii itakuwa butu na haitatimiza majukumu yake ipasavyo kama hawataweka ushabiki wao pembeni na kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa
It's just watching expenditures, na wanainga'ang'ania PAC kwa ajili kick ya kisiasa, ila wanastahili kutuinyesha ubunifu zaidi kwenye hizo kamati za uzalishaji - kilimo, mifugo, uvuvi ambazo zinawahusu watu wengi zaidi. Naona kwa kulilia PAC ipo kibinafsi zaidi maana kamati zote za bunge zipo sawa na hakuna mbunge bora zaidi ya mwenzake.
 
Kwenye hio kamati ya PAC huwa inakuwa na wajumbe wangapi? Je akidi inakuwaje?

Kilimo na mifugo ndio uti wa mgongo wa taifa - kupitia wapinzani tunataka kuona mifugo, kilimo na uvuvi vinatutoa, kamati zingine majungu na unafiki tu.

Hizo kamati zingine zimejaa ulaji na rushwa.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Naomba mnisaidie kwa wabunge wa ukawa Kama ni kutendewa haki kweli baadhi ninafahamu mfano msomi Lissu H Mdee hawa no sheria Sugu na J mziki mwenyekiti wao Mbowe Dj hawa wengine kina kubenea wanafani gani maana hata ktk habari hauumo na mnalilia kamati za???
 
ccm ni wajanja sana. wameweka wabunge dhaifa kwenye kamati muhimu za taifa letu kama nishati na madini,maliasili na utalii. nk. kiukweli wabunge hawako sawa kiuwezo na kimtazamo. hilo ni kwa vyama vyote hasa ccm. mfano wabunge wa viti maalumu.
 
wabunge walienda bungeni kwa ajili ya kamati au kuwakilisha wananchi hizo sababu ni za kijinga kama kila mbunge anajiamini anastahili kuwa bungeni sioni sababu ya kugomea kamati anayopangwa
tatizo ukawa na uchache wao wanafikiri wanaweza kumburuza spika wataisoma namba hadi 2020
Wabongo Kwa ushabiki!
 
K


Kama mlipanga kuwaburuza sasa mtakiona cha mtemakuni nyie ccccccccm, kama mlijipangia kivyenu na kuweka wadhaifu ili mambo yenu yasonge mbele kilaini huu si wakati wake. tunataka usawa na si vinginevyo. Bunge ni la wooote si lenu na marafiki zenu
Sisi wananchi tunachotaka kazi na maendeleo baassi. Mambo ya midomo. fijo, mahakamni hatutaki!!! Hapa ni Kazi tu sio ubabaishaji na visingizio kibao!
 
Mwana, kwa comment hii siamini kama nawe ni great thinker na zaidi naona kabisa umevamia jukwaa ambalo sio saizi yako hivyo nakushauri kwa wembamba wa akili yako kama sindano na udogo wa fikra zako kama jina lako MWANA it is better urudi fasta facebook kwani naamini huko ndio kwako huku umepotea njia. Siamini kwa mtu mwenye kufikiri vizuri anaweza akasema wabunge wote ni sawa HAPANA wabunge wanatofautiana sana hasa kuanzia upatikanaji wa ubunge wao (MAJIMBO, VITI MAALUM na UTEUZI WA RAISI), wanatofautiana elimu na weledi (KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA, DARASA LA SABA, ELIMU YA JUU PhD, Prof? wanatofautiana uzoefu wa shughuli za kibunge (Kipindi kimoja, viwili, vitatu NK), wanatofautiana uwezo wa kifra na kujenga hoja (Tundu Lissu + Deo Sanga, Mnyika +Lusinde, Zitto+Assumpter Mshama)
Pole sana Movich boy. Wasingekuwa sawa Kubenea mwenye elimu ya hapa na pale asingepata Ubunge. My point tunachotaka wananchi si mbwembwe zozote abli na kazi tu na maendeleo endapo yataletwa na Kubenea mwenye elimu ya hapa na pale sawa , endapo yataletwa na Prof. sawa waht we want ni kazi na commitment ya wabunge period!
 
ku

kumbe kuna wabunge dhaifu upinzani tulikuwa hatujui. !! ni ajabu na kweli. sasa kwa nini wananchi waliwachagua? ? napendekeza wajiuzuru kama wanakubali wao ni dhaifu kwa hiyo ni mizigo

hakuna mbunge mdhaifu upinzani wewe Babeli, ila nyie maccm ndo mnjifanya kujipa shavu kama mlivvyoshauriwa na waziri mkuu mstaafu pinda, tunajua kuna maeneo mmebana kimaslahi ila poa tu haina majoto, bunge si ndo hili liasonge mbele!!!!! tatabanana mulemule hadi kitaeleweka, endeleeni kujipa moyo kwenye hakuna tu.
 
Sisi wananchi tunachotaka kazi na maendeleo baassi. Mambo ya midomo. fijo, mahakamni hatutaki!!! Hapa ni Kazi tu sio ubabaishaji na visingizio kibao!
Najua tunataka maendeleo, maisha bora na mambo kama haya , Lakini si kwa staili ileile ya kihafidhina mkuu. Kila mtu anastahili kupata anachostahili mwingine. Sjui kama umenipata!!! wabunge wetu wanayo stahiki sawasawa na ile ya wale wa ccm, sasa kama umefuatilia kwa karibu kilichoanza pale mjengoni ni ama kuna mtoto wa tumboni na wa mgongoni wakati mama yetu ni mmoja.
 
Narudia tena hawa wabunge wa ukawa ni wajinga maana wabunge wote wanahadhi sawa hakuna mbunge mwenye thamani kuliko mwingine.
 
Tatizo Hao wabunge wa ukawa wamepewa vichwa na wafuasi wao nyumbu sasa wakajiona ya kuwa wao ni muhimu na wao ndiyo wenye haki ya kupewa priority kila kitu. Wanajiona wao tu wenye elimu wakati wengi wao rcord zao za shule zinaoneka na upeo wa wa kufikiri ni mdogo sana lakini kinachowasaidia ni madomo kaya na hawa nyumbu wetu wakiona hivyo ndiyo wanapagawa kwa kuwamwagia sifa kem kem. hata wakigoma haitosaidia kitu kwani speaker ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho au wataenda mahakamani??..
 
Ni aina ya uandishi lakini nafikiri mleta mada umekosea sana! Hujui kwanini wamegomea lakini umejaribu kuingiza fikra zako za ufitini kati yao kwa muundo wa maswali "je wabunge wa ukawa walioteuliwa kwenye kamati hiyo ya PAC hawana akili na sio watendaji ? Athari ya muundo huu ni kuwafanya watu wajadili zaidi fikra zako ambazo kimsingi sio njema kuliko kutaka kupata uhalisia wa jambo lenyewe. Niungane nawe kuwashangaa wabunge wa UKAWA kama kweli wote walichagua kamati ya PAC!!! Hivi hata Lisu, Mdee au Mnyika waliomba kuwa katika kamati ya PAC??? Nimshangae pia spika kama amempanga Mnyika au Lisu kwa mfano kwenye kamati ya maendeleo ya jamii kwa kuwa wanafani zao; hivyo naungana na wabunge wa UKAWA kugomea uteuzi huo kwa sababu kukosea kwao kuchagua hakuhalalishi au mpa mamlaka spika ya kuwapangia wabunge kiholela bila kufuata taaluma zao au weledi wao.
Fani ya Mnyika ni nini kaka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom