UKAWA kufungua kesi mahakamani leo

UKAWA kufungua kesi mahakamani leo

Now we are talking the same language UKAWA.People were asking what will UKAWA do to fight for the best constitution after walking out of the Parliament,Some dumb supporters of CCM thought they already won the battle after UKAWA decision,What they didn't know is that UKAWA had a PLAN B & C to fight for this katiba,Filing a constitutional case at the high court was that PLAN B.

Very good! I like it!
 
Taarifa toka katika gazeti moja la leo la mtanzania 29/4/2014 limeripoti kuwa UKAWA wanajiandaa kumfungulia kesi mwanasheria mkuu wa serikali juu ya wa mjadala wa rasimu bungeni.

Mashtaka yake yatakuwa ni kutosimamia sheria inayowataka wajumbe wa bunge maalum kujadili rasimu iliyowasilishwa bungeni kwa mujibu wa sheria kinyume chake wajumbe wamejikita kujadili mambo ambayo hayamo katika rasimu iliyoletwa bungeni.

Sheria ya mchakato wa katiba namba 25(2) inasema wajumbe wataboresha rasimu na sikubadilisha ama kufuta yaliyomo ndani ya rasimu.

Mantiki ya kuboresha mfano wake ni kuwa nyumba ina madirisha 3 umeambiwa uyaboreshe maana yake sio kuongeza madirisha yawe 4 ama kupunguza yawe 2 ila mantiki yake kuyaboresha maana yake ni kama yalikuwa ya mbao unaweka ya viyoo lakini yale yale 3,kama yalikua hayana nondo za ulinzi unayawekea nondo lakini yatabakia yale yale 3 na sio kuongeza yawe 4 au kupunguza yawe 2,huko si kuboresha.

Mtakumbuka kuna uzi mmoja nilidokeza kuwa UKAWA imejaa watu mahiri kwa fikra na mikakati, nikaonya kuwa '' ukiona kobe kainama....ujue sheria yaja...'' Ndiyo UKAWA wamekuja, kuonyesha kweli wapo kwa maslahi ya Umma na sii tumbo.

Hapa NDIPO tunaelekea ktk kupambana na wezi wa mali ya umma na maoni ya mma, kifikra, kikatiba na Kisheria kuhakikisha mstari unachorwa kujenga wigo thabiti wa upatikaji wa ulinzi kwa maoni ya WANANCHI yaliyowailishwa ktk rasimu ya 2.

Nachoweza kuongezea ni kuwa....mbali na kuomba ufafnuzi wa Kisheria, thamira kuu nyingine zijumuishe, kujilinda na kuiboresha misingi ya rasimu kama ilivyowasilishwa, kujenga wigo wa kuongezwa mitizamo na sera za vyama whatsoever na pia kulinda maslahi, uhai, heshma na credibility ya wajumbe wote wa TUME kwa Mujibu wa SHERIA iliyounda TUME hiyo
.
 
Mimi sio mwanasheria lakini nimesikia kua Bunge la katiba la haki ya kujadili, kubadilisha, kurekebisha, kuongeza au kuondaa kifungu chochote cha rasimu ya katiba. Kama ni kweli haki hiyo ipo, basi wanaofungua kesi wanapoteza muda wao na wanachelewesha upatikanaji wa katiba mpya. Tumeshuhudia matatizo mengi na tuhuma nyingi dhidi ya tume ya uchaguzi kwamba ndio wanawachelewesha wapinza kuingia Ikulu, mi naona wangezingatia mfumo wa tume ili wachukue nchi kisha watuletee hiyo katiba mpya ndani ya siku 100.

Hivi inawezekana akina Lissu, Mbatia, Mtatilo, Pr Safari etc, hawakujadili na kuchambua jambo hilo kisheria ili kuona uhalali wake? Sidhani.... Go ahead UKAWA!
 
Ni wahaini safi ukawa buruza hawa magaidi kizimbani
 
Natamani ingewezekana ile mi mama ya CCM iliyokuwa inapiga mipasho kule bungeni niione ikipandishwa mahakamani
 
Mimi binafsi nachelea kusema huko waendako haki HAWATAIPATA wanafungua kesi wapi? Ktk mahakama zetu hizihizi nizijavyo mmi na wewe angalau ingekua international court hapo ningepata imani kdogo lakn kwa hizi mahakama zetu itakuwa ngumu sana kupata haki N'WAY LET THEM TRY.
 
Bravo UKAWA.
This is a very good move.Mimi nilikuwa nawashangaa sana hawa UKAWA pamoja na kua na Wanasheria lukuki tena waliobobea kukaa kwenye BMK wakipigizana kelele na WENDAWAZIMU WA CCM! Wazungu wana msemo, "NEVER ARGUE WITH A FOOL PEOPLE MAY NOT NOTICE THE DIFFERENCE"

BMK imetumia Tshs. 20 BILLIONs kwa siku 67 na bado KATIBA HAIJAPATIKANA hata dalili hakuna! Vichaa wa CCM wameishia kuporomosha matusi ya nguoni na kuwatukana wenzao WACHACHE wa Upinzani kana kwamba wao si Watanzani!!Hii ni aibu na fedheha kubwa sana.

Kitu chochote kinachofanyika chini ya jua na kiko kinyume cha SHERIA ILIYOWEKWA NA WANANCHI LAZIMA KIPINGWE MAHAKAMANI, na hivo basi UKAWA wako perfect kabisa kufungua kesi ya Kikatiba Mahakamani! Kama Mahakama Kuu ya hapa nchini itakataa bado wanaweza kwenda Mahakama ya EA,AU na mpaka UN!!!

Kesi hii ya Kikatiba lazima iamuliwe mapema kabisa kabla ya Mkutano wa BMK awamu ya 2 mwezi wa August mwaka huu. Watanzania tunasema hatutaki kusikia matusi,mipasho,ushabiki na ujinga wa aina yoyote. Tunachotaka kusikia ni RASIMU YA KATIBU-2 IKIJADILIWA KAMA ILIVOWASILISHWA BUNGENI NA JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA. Nje ya hapo afadhali BMK ivunjulie mbali tujue tunaendelea na KATIBA YA ZAMANI, basi!
 
Taarifa toka katika gazeti moja la leo la mtanzania 29/4/2014 limeripoti kuwa UKAWA wanajiandaa kumfungulia kesi mwanasheria mkuu wa serikali juu ya wa mjadala wa rasimu bungeni.

Mashtaka yake yatakuwa ni kutosimamia sheria inayowataka wajumbe wa bunge maalum kujadili rasimu iliyowasilishwa bungeni kwa mujibu wa sheria kinyume chake wajumbe wamejikita kujadili mambo ambayo hayamo katika rasimu iliyoletwa bungeni.

Sheria ya mchakato wa katiba namba 25(2) inasema wajumbe wataboresha rasimu na sikubadilisha ama kufuta yaliyomo ndani ya rasimu.

Mantiki ya kuboresha mfano wake ni kuwa nyumba ina madirisha 3 umeambiwa uyaboreshe maana yake sio kuongeza madirisha yawe 4 ama kupunguza yawe 2 ila mantiki yake kuyaboresha maana yake ni kama yalikuwa ya mbao unaweka ya viyoo lakini yale yale 3,kama yalikua hayana nondo za ulinzi unayawekea nondo lakini yatabakia yale yale 3 na sio kuongeza yawe 4 au kupunguza yawe 2,huko si kuboresha.

Mimi natabiri kuwa UKAWA wakitoka mahakamani watasema "Hata mahakama nayo si huru ni ya CCM" Halafu baadhi ya wananchi watawauliza "Mbona mlipoteza fursa ya kurekebisha Hilo kwenye Bunge la Katiba" Jamani ni utabiri wangu tu.
 
Mimi natabiri kuwa UKAWA wakitoka mahakamani watasema "Hata mahakama nayo si huru ni ya CCM" Halafu baadhi ya wananchi watawauliza "Mbona mlipoteza fursa ya kurekebisha Hilo kwenye Bunge la Katiba" Jamani ni utabiri wangu tu. Msinipige Mawe.
 
mmmmmmh kweli ukawa mmetushika pabaya,ngoja nimwambie nchemba tuendeleze ubabe, serikali yetu bana aalaah
 
Je kuboresha hakuwezi kuwa ni kuongeza, kupunguza au hata kubadilisha kitu ndani ya unachokiboresha?
 
Sishauri kabisa UKAWA wafungua kesi mahakamani. Katiba kwa kiasi kikubwa inaongozwa na maridhiano. Mahakamani siyo sehemu ya kupata maridhiano. Kama serikali haijawa tayari kisiasa kukubali serikali tatu, haitabariki maamuzi ya mahakama hata kama yatakuwa in their favour. Mtikila alishinda kesi ya mgombea binafsi, lakini hadi leo serikali haijaruhusu mgombea binafsi. UKAWA waiondoe haraka kesi hii, waendelee na political process ya kuelimisha umma kuhusu maoni ya wananchi waliyoyatoa kupendekeza serikali tatu katika rasmu ya II katiba. Hapa UKAWA wanahitaji kutafakari upya suala hili.
 
I'm afraid hoja hii haijakaa vizuri na nirahisi sana kujibiwa kisiasa. BMK linauwezo wa kuongeza ama kupunguza yaliyoko kwenye Rasimu kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wa Tanzania...
Dont be afraid. Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria husika ili kuona kama "walio wengi" au BMK lina uwezo wa kukataa mapendekezo ya wananchi (walio wengi) na leta mapendekezo ya CCM (rasimu mbadala). Hicho kinachowapeleka UKAWA mahakamani. Mimi nawaunga mkono, wewe je? Nakushauri uwaunge mkono.
 
Taarifa toka katika gazeti moja la leo la mtanzania 29/4/2014 limeripoti kuwa UKAWA wanajiandaa kumfungulia kesi mwanasheria mkuu wa serikali juu ya wa mjadala wa rasimu bungeni.

Mashtaka yake yatakuwa ni kutosimamia sheria inayowataka wajumbe wa bunge maalum kujadili rasimu iliyowasilishwa bungeni kwa mujibu wa sheria kinyume chake wajumbe wamejikita kujadili mambo ambayo hayamo katika rasimu iliyoletwa bungeni.

Sheria ya mchakato wa katiba namba 25(2) inasema wajumbe wataboresha rasimu na sikubadilisha ama kufuta yaliyomo ndani ya rasimu.

Mantiki ya kuboresha mfano wake ni kuwa nyumba ina madirisha 3 umeambiwa uyaboreshe maana yake sio kuongeza madirisha yawe 4 ama kupunguza yawe 2 ila mantiki yake kuyaboresha maana yake ni kama yalikuwa ya mbao unaweka ya viyoo lakini yale yale 3,kama yalikua hayana nondo za ulinzi unayawekea nondo lakini yatabakia yale yale 3 na sio kuongeza yawe 4 au kupunguza yawe 2,huko si kuboresha.

Nafikiri hii ni hatua nzuri zaidi ambayo taratibu za kimahaka zitasaidia kuweka mambo sawa kuliko mikutano ni sawa na kumpigia gitaa mbuzi.
 
ww ndo hamnazo.

UKAWA wafanye mengine.hili wanapoteza muda.UKAWA wenyewe walishaanza kutoa maoni yao kuboresha katiba.wataachaje mchakato WA kidemokrasia halafu wakimbilie mahakamani eti kwa kuwa maoni ya wachache yamekosa support..HILI NI BUNGE LA KUTUNGAKATIBA NA SIO LA KUPOKEA KATIBA
 
Back
Top Bottom