hivi hakuna yeyote anayetakiwa kukamatwa kwa ukiukwaji wa kanuni za kujadili rasimu ?
hapo atakuwa mwenyekiti wa bunge la katiba
hivi hakuna yeyote anayetakiwa kukamatwa kwa ukiukwaji wa kanuni za kujadili rasimu ?
Nahisi unachanganya kati ya bunge la Jamhuri ya muungano na bunge maalumu la katiba (BMK).Hawatafanikiwa na wanafahamu hawatafanikiwa!.
Bunge Maalum la Katiba lina kinga kisheria za kuzuia kuhojiwa na chombo chochote kuhusu lolote linalofanyika/lililofanyika ndani ya bunge.
Hawa wanatafuta sifa ambazo hazipo.
Ha ha ha! Hiyo ni kweli tupu mdau! Kamishna polepole anajua aisee! Kwa maneno yake mwenyewe Kamishna Polepole anadai yeye ni mara yake ya kwanza kuandika katiba na amepata uekewa mkubwa sana, kwa kuwa walifanyakazi ile kama team, wakafafanuliwa pale walipokosa kuelewa, mwishowe kila Mjumbe akatoka na Elimu kubwa ya Uandikaji wa katiba, tafsiri pana ya kila kifungu ndani ya Rasimu na mambo mengi ya Kikatiba!
Hawa jamaa kama wehu vile!!
ukawa baada ya kunyimwa posho wanahangaika sana
inayoboreshwa ni nyumba sio madirisha,huwezi kuboresha dirisha pekee kama nyumba haipo.Taarifa toka katika gazeti moja la leo la mtanzania 29/4/2014 lime ripoti kuwa ukawa wanajiandaa kumfungulia kesi mwanasheria mkuu wa serikali juu ya wa mjadala wa rasimu bungeni;mashtaka yake yatakua ni kutosimamia sheria inayo wataka wajumbe wa bunge maalum kujadili rasimu iliyo wasilishwa bungeni kwa mujibu wa sheria kinyume chake wajumbe wamejikita kujadili mambo ambayo hayamo katika rasimu iliyo letwa bungeni;sheria ya mchakato wa katiba namba 25(2) inasema wajumbe wataboresha rasimu na sikubadilisha ama kufuta yaliyomo ndani ya rasimu;mantiki ya kuboresha mfano wake ni kuwa nyumba ina madirisha 3 umeambiwa uyaboreshe maana yake sio kuongeza madirisha yawe 4 ama kupunguza yawe 2 ila mantiki yake kuya boresha maana yake ni kama yalikua ya mbao unaweka ya viyoo lakini yale yale 3,kama yalikua hayana nondo za ulinzi unayawekea nondo lakini yatabakia yale yale 3 na sio kuongeza yawe 4 au kupunguza yawe 2,huko si kuboresha;
Tunaona kila Siku na kusikia wajumbe waliobaki bungeni na wale wanaojiita tanzania kwanza wakiwapiga vijembe ukawa. Eti ooh! Sijui wanataka kuvunja muungano! Mara oh! Ni wanafiki! Mara hawaitakii mema Tanzania ! Mara kuwakejeli eti hata wasiporudi bungeni wao watapitisha katiba inayokubalika na wananchi. Hapa najiuliza' hivi ukawa na Hawa wengine nani anatetea maoni ya wananchi? Tuwe Wa kweli hapa! Tuache porojo hapa. Nauliza tu tuache itikadi tuache upenzi Wa mire go yetu
Taarifa toka katika gazeti moja la leo la mtanzania 29/4/2014 limeripoti kuwa UKAWA wanajiandaa kumfungulia kesi mwanasheria mkuu wa serikali juu ya wa mjadala wa rasimu bungeni.
Mashtaka yake yatakuwa ni kutosimamia sheria inayowataka wajumbe wa bunge maalum kujadili rasimu iliyowasilishwa bungeni kwa mujibu wa sheria kinyume chake wajumbe wamejikita kujadili mambo ambayo hayamo katika rasimu iliyoletwa bungeni.
Sheria ya mchakato wa katiba namba 25(2) inasema wajumbe wataboresha rasimu na sikubadilisha ama kufuta yaliyomo ndani ya rasimu.
Mantiki ya kuboresha mfano wake ni kuwa nyumba ina madirisha 3 umeambiwa uyaboreshe maana yake sio kuongeza madirisha yawe 4 ama kupunguza yawe 2 ila mantiki yake kuyaboresha maana yake ni kama yalikuwa ya mbao unaweka ya viyoo lakini yale yale 3,kama yalikua hayana nondo za ulinzi unayawekea nondo lakini yatabakia yale yale 3 na sio kuongeza yawe 4 au kupunguza yawe 2,huko si kuboresha.
Lakini sio kuondoa msingi mkuu uliojenga rasimu nzima, ambayo ni muundo wa serikali..
ukawa baada ya kunyimwa posho wanahangaika sana
sizani kama waweza hata simamia familia yako!
Mkuu nahitaji kuelimishwa zaidi, kama hutojali tafadhali saidia kunifafanulia mambo ya fuatayo:- Katiba ya China imejengwa katika Misingi Mikuu mitatu/ 3 principles of the people ambayo ni Nationalism, Democracy and Socialism. kwa kiasi kikubwa sana katiba yao imeweza kuwasaidia na sasa wanatarajiwa kuiengua USA kileleni kwa nguvu kubwa za kijeshi baada ya kufanikiwa kiuchumi! NATIONALISM, DEMOKRACY and SOCIALISM ndiyo Misingi ya Kuzaliwa kwa Azimio la Arusha kwa uelewa wangu. SWALI:- Kama Muundo wa Serikali ndiyo msingi Mkuu unaojenga rasimu nzima, Je? Rasimu Katiba Tarajiwa itakidhi Mahitaji ya Nchi katika nyakati hizi za Ushindani Mkali wa Kiuchumi? Kuweka kwenye KATIBA mpya kipengele cha KUWAVUTIA WAWEKEZAJI WA NJE huku sikuuza nchi?...Mkuu fikiria kabla ya kuandika kwanza ili nipate majibu yanayosadifiana na maswali yangu... Danken!
ukawa baada ya kunyimwa posho wanahangaika sana