Ukawa kuandamana nchi nzima

Ukawa kuandamana nchi nzima

Kusema kweli pamja na kuwaunga mkono 100% kwa kutoenda Bungeni kwa hili sioni mantiki. Wakae kimya maana kimya kingi kina mshindo mkubwa. Wakati wa kuhamasisha umma kupinga rasimu ya Sitta bado.

Tatizo kule mjengoni hawakai bure....ingekua wanakaa bure kujadili katiba yao, tungewaachia warekebishe hadi nukta afu tuje kuipinga
 
Nishamuona buku saba mmoja wa lumumba kaja kutetea hapa......akawaite wenzake akina faizer foxy waje huku kumsaidia...
 
Hawana kazi ya kufanya acha wakatembee mtaani wauze sura wataonekanaje bila kujiuza.

Umesema kweli.
Ila hujajiuliza nani anawajibika kuhakikisha maisha bora?
Nani anawajibika kuhakikisha rasimu ya tume inazingatiwa ?
Nani anawajibika kuhakikisha maridhiano yanafikiwa ?
Na je, nani anaruhusu fedha za watanzania kuchezewa ?
 
yanapingwa matumizi mabaya ya fedha za umma kutokana na kujadili mambo ambayo hatujawatuma.

Hakuna lolote ukawa wamechemsha wanawapiga mkwara wabunge wao mbowe mbatia na lipumba wanapiga hela toka ujerumani
 
Hakuna lolote ukawa wamechemsha wanawapiga mkwara wabunge wao mbowe mbatia na lipumba wanapiga hela toka ujerumani

Wabunge wa ukawa kuweni macho viongozi wenu wanatajirikia migongoni mwenu na ukimya wenu ndiyo Msemo ule wajinga ndiyo waliwao
 
Kaeni chonjo na Lameck madilu asije akawalipua tena. Mungu awatangulie.
 
Penye CHADEMA hapakosi maandamano!

Safari hii tunataka viongozi wa UKAWA wakae frontline.

Sio kutanguliza vijana kama chambo!
 
Tunawatakia kila la heri kitu cha maana ni ujumbe maalum katika mikutano si kutukana au kumwaga kashfa.Ningependa mikutano hiyo ilenge kuwajenga na kuwafunza waTanzania uchafu unaofanywa na bunge la posho huko mjini Dodoma.

Unatuhimiza sisi tuandamane, wewe utajifichia wapi?
 
UKAWA KUFANYA MAANDAMANO NCHI
NZIMA KUANZIA WIKI IJAYO YASIYOKUWA
NA RATIBA WALA KIKOMO.
Mhe James Mbati akisoma Tamko la UKAWA
kwa niaba ya Mchumi wa Kimataifa Prof I
brahim Lipumba na Freeman Mbowe
"Maandamano Nchi nzima na Mikutano ya
Hadhara kwa ajili ya kuhamasisha watu
kupinga matumizi mabaya ya Fedha za
Wananchi katika Mchakato wa Bunge Maalum
la Katiba."
Mhe; Mbatia ameendelea kusema "Baada ya
kukamilika kwa Mazungumzo yanayoendelea
na CCM wiki hii.Hata hivyo Ukawa
wamesema,kwa kadiri mazungumzo
yanavyoendelea hakutakuwa na tija hivyo
ameamua kuweka wazi azma ya kufanya
maandamano"
Professa Lipumba amerudia WITO wake wa
kuwataka VIJANA kuanza mazoezi ya VIUNGO
kwajili ya ukombozi.
Freeman Mbowe amesema NGUVU ya UMMA
sasa kutumika ili kuleta UKOMBOZI hakuna
kulala mpaka kieleweke kuanzia wiki ijayo.
Ni MAANDAMANO ni MAANDAMANO mpaka
Mkoloni mweusi atupatie KATIBA yetu.
NB Ikumbukwe JINI likitoka kwenye CHUPA
huwa halirudi ndani ya CHUPA serikali 3 ni
lazima sio ombi tena.

Safu ya mbele iwe, Tundu, Slaa, mbowe, lipumba,mbatia,josephin, madem wa mbowe wote, familia zao wote hata wale wanawasomesha nje ya nchi waje wakae mbele, dada yake Lissu na shemeji zake wale watoto wa mtei na the like wasikose.
 
Tanziania serikali tatu eti Mbowe anataka alikuja na majimbo kashindwa sasa serikali tatu hatafaulu andamaneni mkimaliza mtaikuta katiba mpya
 
ila wahakikishe kwenye maandamano hayo wake zao na watoto wao wawemo.

Una akili kama kangaroo, kwan wale watoto walio uwawa kule south wakipinga unaguzi wa rangi na kutaka mandela aachiwe, je watoto wa mandela walikuwa kwenye yale maandamano?
 
Kaeni chonjo na Lameck madilu asije akawalipua tena. Mungu awatangulie.

Mbowe alienda kuchukua hela mombasa mpaka gari lake likakamatwa alipewa hela za posho za siku 60 za wabunge wa ukawa cha kushangaza wanaendelea kuzila yeye lipumba na mbatia
 
Back
Top Bottom