Ukawa kuandamana nchi nzima

Ukawa kuandamana nchi nzima

Naona toka maandamano yatangazwe raia hawana mbwembwe kitaa.......wameshawazoea hamuwasumbui tena RAIA........
 
Inakuwaje mnaandamana na watu wenye uhakika wa kula milo mitatu?
 
Mkuu nchi nyingi zilizoishia kwenye machafuko ni kwa watawala kuupuuza umma. Ona nchi kama Siera Leon, Liberia na hata Kenya mambo yalikuwaje? Tatizo la hapa kwetu, viongozi wa chama Tawala kama wakina Nape wakiingia mitandaoni na kuona maoni ya wafuasi wao vidampa kama waliochangia hapa wanaona ni haki yao kuendelea na wakifanyacho. Wanasahau kwamba iwapo nchi itavurugika na kutokea machafuko wao viongozi ndio watakaowajibika kwenye mahakama za uhalifu wa kivita sio hawa wapiga debe wa JF na mitandao mingine.
Maridhiano ni jambo la muhimu sana kwani wote ni Watanzania kwa nini tufikie kugombana? Utakuta mume ni CUF au Chadema na mke ni CCM jee ni haki kweli kwa kuwa itikadi za kisiasa ni tofauti basi tutwangane?
Hebu watumie akili watuepushe na hizo dhahama pia waangalie nao wasiishie pabaya.

Sent from my iPad using JamiiForums
Ndugu, Unaemuona mfuasi kidampa lazima uelewe kuwa kwa CCM ana kura iliyosawa na wale ambao unawaona siyo wafuasi kidampa.

Maridhiano kuhusu Rasimu ya Katiba hayapatikani barabarani. Maridhiano kuhusu Rasimu ya Katiba yanapatikana ndani ya Bunge la Katiba.

Ukikimbia bunge, ina maana hata maridhiano utakuwa umeyakimbia.

Amani ya Tanzania inalindwa kama mboni ya jicho na serikali ya CCM, ndiyo maana taifa letu bado ni mfano wa kuigwa na nchi zingine Africa. Tutaendelea kuwa ni mfano wa kuigwa chini ya serikali ya CCM.
 
nashangaa kwa nini wamshinikize raisi asitishe bunge la katiba wakati wao hawataki kuvitumia vyombo vya usuluhishi walivyovitunga wenyewe katika kanuni ili Kuwasuluhisha!. Halafu isitoshe kuna Chombo cha mahakama ambacho wana haki ya kufungua shauri la kuomba kusitisha shughuli za bunge hilo AU kuomba kupewa tafsiri ya sheria iliyoanzisha mchakato huu
 
Ndugu, Unaemuona mfuasi kidampa lazima uelewe kuwa kwa CCM ana kura iliyosawa na wale ambao unawaona siyo wafuasi kidampa.

Maridhiano kuhusu Rasimu ya Katiba hayapatikani barabarani. Maridhiano kuhusu Rasimu ya Katiba yanapatikana ndani ya Bunge la Katiba.

Ukikimbia bunge, ina maana hata maridhiano utakuwa umeyakimbia.

Amani ya Tanzania inalindwa kama mboni ya jicho na serikali ya CCM, ndiyo maana taifa letu bado ni mfano wa kuigwa na nchi zingine Africa. Tutaendelea kuwa ni mfano wa kuigwa chini ya serikali ya CCM.

Mkuu hukunielewa niliposema vidampa umenielewa vibaya. Nimemaanisha kuwa hawa ni wafuasi wanaoshangilia kila kitu bila kujali madhara yawezayo kujitokeza wala kutoa ushauri pale panapo stahili. Mtu kama anakipenda chama chake na anaona kuna mahali hakiendi vizuri lakini anashangilia kama yuko mpirani huyo ni KIDAMPA tuu.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Kuna haja gani; ya kupinga vikao vya bunge visiendelee wakati ukawa mumejitoa wenyewe, mmesusa na sasa mnatamani, kama mmpenda rudini
 
Tunawatakia kila la heri kitu cha maana ni ujumbe maalum katika mikutano si kutukana au kumwaga kashfa.Ningependa mikutano hiyo ilenge kuwajenga na kuwafunza waTanzania uchafu unaofanywa na bunge la posho huko mjini Dodoma.

Inawezekana wakati huu si muafaka kupiga kampeni hasi.Kama wangeweza kuzuia kuendelea kwa bunge sawa,vinginevyo wasubiri hayo madudu yapitishwe then,wakutane kwenye kura ya maoni
 
Inakuwaje mnaandamana na watu wenye uhakika wa kula milo mitatu?

Mbowe acha usanii umevuta hela ujerumani umepeleka kwenye miradi yako unataka kuandamanisha watu?anza kwanza kueleza na uweke wazi fedha ulizovuta ujerumani kwa ajili ya wabunge wote wa ukawa
 
Kwanza naomba kukiri kuwa mimi sio mwanasheria. Naomba kuuliza Je kufuatana sheria ya kuundwa kwa Bunge la Katiba , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana mamlaka ya Kusitisha Bunge la Katiba kwa sababu ye yote ile? Maana sioni shinikizo hili litafanikiwaje ikiwa hana madaraka hayo kisheria. Utawala wa sheria ni muhimu sana.
 
Khaa!! Safari hii angalau watulipe hela japo ya kula siku ya maandamano. Mbona wenyewe wanalipana padei?? Na sisi tunaacha shughuli zetu zinazotupatia riziki ya siku hiyo ili tuwaunge mkono bana
 
Tunayasubili maandamano kwa hama sana,ila tunawaomba viongozi wetu wa ukawa mtoe elimu zaidi kama walivyo fanya wajumbe wa iliyokuwa tume ya mabadiko ya katiba,maana kuna wengine hawakubatika kuona mdahalo ule.
 
Ukawa ilishashindwa sioni jipya hawana mvuto kwa umma walipotoka walienda kwa wananchi wakakosa watu kinachofanyika sasa ni usanii ili wafadhili wawape fedha halafu mbowe anazifisadiiiiiiii
 
Chezea mbowe kwa usaniii? Yaani mbatia na lipumba hawajui wanatumia tu jamaa anapiga hela
 
Sisi huku Songea tumejipanga, ni mawe tu wakithubutu kuleta makengeza na vipara vyao vya kutengeneza. Huku sisi ni full mauzalendo tu hakuna ukawa wala serikali tatu, huku mbili tuuuuuuu!
 
Back
Top Bottom