UKAWA kitengo cha habari mmelala?

UKAWA kitengo cha habari mmelala?

Hawako active hata kidogo, mnajua kuwa Radio, TV na magazeti mengi nchi hii ambavyo ndio vyombo vya kufikishia habari ya nini kinaendelea haviko huru kwa woga au kwa kujipendekeza ili wapate matangazo ya biashara kuendeshea vyombo vyao.

Cha kushangaza matukio yao wanashindwa kuhakikisha waandishi wa vyombo vya nje waliopo hawashirikishwi. Vyombo kama CNN, BBC, ALJAZEERA, REUTERS, SABC nk hivyo matukio mengi hayafahamiki nje ya nchi na wao kudhani mambo ni poa sana kama ikivyokuwa zamani.

Hata hapa ndani, mumeshindwa kuandaa vipindi hata vya kulipia katika TV venye maudhui ya kujitangaza dhamira na nini kinaendelea.

Wakati umefika muamke ili msije kuwalaza na wengine au ongezeni nguvu vitengo vyenu vya habari. Na kila tukio hakikisheni mnawawezesha waandishi wa vyonbo vya nje wahudhurie sio kuwajaza wa Uhuru ambao mnajua badala ya kujenga wataleta damage
Mkuu asante kwa kukumbusha hili! Binafsi nitajaribu kumtafuta Makene tuongee juu ya hili pengine huenda kuna kitu anapanga. Nikimaliza nitakujuza PM.
 
Kigezo chako ni duni. Au unataka watumie staili ya CCM ili kuonekan a wajanja machoni pako. Pole
Akili za namna hii haziisaidii Chadema, kale kanyumba kwa hadhi ya Chadema ya sasa kanatakiwa kawe makao makuu ya jimbo au wilaya na siyo makao makuu ya Taifa.

Nenda pale buguruni ukaone makao makuu ya CUF yalivyo na hadhi yake licha ya kuwepo uswahilini, mjifunze kukosoana kwa adabu ndani ya vyama vyenu na siyo kusifu tu kila kitu, hivi unadhani mtu kama Lowasa umpe ofisi pale kichochoroni ufipa ataacha kwenda kwenye ofisi yake mikocheni?

Muwaeleze viongozi wenu ukweli huu, ofisi ya taasisi yoyote ni alama ya seriousness ya taasisi husika, hata tapeli mwenye ofisi ya kisasa ndio anayeweza kutapeli pesa nyingi kwa ufanisi.
 
Pole sana
 
Back
Top Bottom