UKAWA hawaijui historia ya Zanzibar

UKAWA hawaijui historia ya Zanzibar

WAKATI LEO 08/10/2014 rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akienda Dodoma kukabidhiwa katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la katiba kupitia kwa mwenyekiti wake SAMWEL SITTA, kuna uongo,propaganda na upotoshaji mkubwa unaofanywa na wafuasi wa upinzani hususan ukawa kuhusu mutakabali wa matokeo ya kura ya maoni pindi muda wa kupiga kura husika utakapowadia.

Upotoshaji huu unafanywa na hawa watu kwa sababu labda hawajui historia ya visiwa hivi.. unguja na pemba au agenda binafsi zilizowagubika bila kujali maslahi ya taifa kwa ujumla wake.

Labda nianze kwa kifupi tuu kuwapa historia ya zanziba muda mfupi kabla ya mapinduzi, siku nne za mapinduzi na maisha baada ya mapinduzi. wakti wa utawala wa muingereza, zanzibar lilikuwa ni koloni la uingereza chini ya mamlaka ya sultani wa OMAN huku makao makuu ya sultanate hiyo yakiwa zanzibar.

Na kwa kipindi hicho kulikuwa na vyama vya kupigania uhuru ambavyo vilitofautiana sana mitazamo kiasi cha waoigania uhuru wengine wakiamini sultani na vibaraka wake ni wakazi halali na watawala halali wa zanzibar kutokana na historia ya urithi.

Na hivyo uhuru waliokuwa wanadai ni kutoka mikononi mwa waingereza huku wakiungwa mkono na sultani na waarabu.Moja kati ya vyama hivyo ni ZANZIBAR NATIONALIST PARTY(ZNP) ambacho kilikuwa kinajulikana kama HIZB na kiongozi wake alikuwa ni MOHAMMED SHAMTE.

Kwa ujumla hawa walikuwa ni waarabu na mabinamu zao huku wakimtukuza sultani na kujichukulia wao(waarabu) kama daraja la kwanza, mabinamu zao(machotara/wapemba) kama daraja la pili na waafrika kama daraja la tatu na la mwisho.

Hawa walikuwa radhi waendelee kubaki chini ya milki ya sultani milele na kuendelea kuwakandamiza waafrika weusi.IKUMBUKWE TU KUWA ZNP(HIZB) NDIO CHIMBUKO CUF na hata misimamo na malengo yao ni yaleyale kumuenzi sultani na kuwaangamiza waafrika weusi.

Aidha kulikuwa na chama kinachowasimamia waafrika na washirazi.hiki ni ASP-AFRO SHIRAZ PARTY. Hiki kilikuwa kinasimamia misingi ya usawa wa rangi zote na ukoloni walikuwa wanautafsiri kwa mapana zaidi.

Wao walikuwa wanaona muingereza ni mkoloni na sultani ni mkoloni vilevile na dhamira yao ilikuwa ni kuwaondoa woote tena kwa amani kabisa.Ikumbukwe tu kuwa ASP ndio chimbuko la CCM baada ya kuungana na TANU mwaka 1977.


Dhoruba kuu ilitokea pale palipoitishwa uchaguzi wa zanzibar ikiwa ni maandalizi ya kupewa uhuru toka kwa muingereza ambapo vyama vitatu ASP,ZNP na ZPPP(ZANZIBA AND PEMBA PEOPLE'S PARTY) vilipochuana katika uchaguzi mkuu na ASP kushinda ila ikiwa ni chini ya 50%.

Hapo ndipo ZPPP na ZNP zilipocheza mchezo mchafu kwa kushirikiana na sultani na kuunganisha kura zao kisha kutangazwa kama washindi na kukabidhiwa madaraka ya kuiongoza zanzibar huru chini ya SHAMTE.

Jambo hili liliwakatisha tamaa ASP NA KUPANGA NA KISHA KUAYATEKELEZA MAPINDUZI KWA MAUAJI YA HALAIKI (WATCH THE VIDEO) na hatimaye kumtimua sultani na hatimaye kuungana na tanganyika.

Kwa wale wajinga wasio fahamu visasi vilivyotunzwa tangu zama hizo hadi sasa na jinsi waarabu na wapemba wanavyotamani kupata nafasi ya kulipa kisasi, basi na waangalie hii video niliyoambatanisha muone jinsi ambavyo ilibaki kidogo kwa kizazi kizima cha waarabu na wapemba kifutwe kabisa katika ardhi ya zanzibar.
wanatafuta nafasi japo katu hatutawapa.

Mantiki ya andiko langu hili ni KUWAJIBU wale wanaojidanganya kuwa LINAPOKUJA SWALA LA ZANZIBAR eti WAZANZIBAR WOTE WANAUNGANA.Nasema hapana, nasema katu wazazibar waafrika waliojikomboa chini ya mapinduzi matakatifu hawawezi kuwa upande mmoja na wale walioapa kuyapinga mapinduzi hayo.

Nasema mapinduzi ya zanzibar yako mioyoni mwa wazanzibar waafrika na angamizo la mapinduzi hayo ni kiapo kilicho mioyoni mwa waarabu na binamu zao (wapemba.

Mapinduzi yale yaliratibiwa toka tanganyika na wapiganaji wengi walitoka tanganyika.

Vingozi wa mapinduzi(abdul rahman babu na abeid karume) waliyaratibu mapinduzi yale toka tanganyika na walikuwa na mawasiliano ya karibu sana na nyerere. hivyo basi kwa namna yoyote huwezi kuzitenganisha siasa za waafrika wa zanzibar na siasa za tanganyika(tanzania bara).

RAISI KIKWETE anaenda kukabidhiwa rasimu pendekezwa na baada ya hapo tuaingia kwenye referandum, wale wanaodhani huenda zanzibar katiba itakataliwa, basi nawapa pole.

Na walewazalendo wenye hofu labda safari hii waarabu na binamu zao watashinda dhidi ya wanamapinduzi, napenda niwahakikishie kuwa KAMWE HILO HALITATOKEA.

Kwenye kura ya maoni katiba itapita na hicho kikwazo kitasambaratishwa kama vilivyosambaratishwa vikwazo vingine vilivyokuwa vinaiandama mchakato mzima wa katiban na hii sio kwa ajili ya chama fulani au watu fulani bali ni kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu.

Kamwe hatutawapa WAARABU NA BINAMU ZAO kuja kufanya mauaji ya halaiki kama vile walivyojiapiza.Jeshi la wananchi wa tanzania litakuwepo zanzibar kama lilivyo hivi sasa na hii haina tofauti na jinsi wamakonde,wazaramu, wasegeju,wanyamwezi na watanganyika wengine walivyojitolea kuiokomboa zanzibara toka mikononi mwa sultani.

Linapokuja suala la mustakabali wa taifa letu HUWA HATUCHEKI NA NYANI, TUSIJE KULA MABUA.

Wewe unafiti wapi katika hiyo historia?
 
unatumia vigezo gani kuwa walitumiwa?

Kamahuru ilikuwa Zanzibar hasa Pemba. Huku kulikuwa na Chama cha Wananchi chini ya Mzee James Mapalala. Maalim akamrubuni wakaungana na kuwa na CUF ili kutimiza matakwa ya Kikatiba. Baada ya kuungana na kusajili chama, Mzee Mapalala akatoswa!
 
Wacha uwongo ww! 1. Aliye ratibu mapinduzi ya Zanzibar ni John Okello a ugandan. 2. Linapozungumzwa la Wazanzibar kuwa wamoja ni pale wanapokuwa wanadai nchi yao, hamna mzanzibar safi au mzanzibar koko. Ukitaka kuliona hilo zungumzi serikali moja kwa Tanzania. 3. Ni dhahili kuna wanaofaidi ktk mfumo huu huko Zanzibar na hasa viongozi na ufaidi wao ni ubebwa wao na Tanganyika. Kwa hili Tanganyika tutajitegemea. Awali baada ya uchaguzi kila kitu kitakuwa kipya yaani rais mpya,bunge jipya and of course sheria mpya ya mchakato wa katiba.
kuna tofauti kati ya kuratibu na kutekeleza. huenda una akili ndogo sana ya kushindwa kutofautisha hayo mabo mawili..
na kwa taarifa yako tu, OKELLO aliongoza utekelezaji wa mapinduzi na katu hakuwa mratibu. na ndio maana ilikuwa rahisi sana kumuondoa pale walipotaka. mratibu siku zote anafahamu njia ya kuingilia na kutokea lakini mtekelezaji(kama OKELLO) huwa hajui pa kuingilia wala pa kutokea
 
Mwandishi unajua unachokiandika au unacopy na kupaste ,kwanza kwa taarifa yako mambo ya kasumba za kurudisha waarabu hizo zishapitwa na wakati ,maana inaonyesha hata hujui kama hapa Tanganyika wenyeji wengi ni kutoka Congo ,Tanganyika ilikuwa pori la wanyama tu hadi baharini ni wanyama watupu ,hio ndio historia na itabakia kuwa hivyo.

Juma Duni Haji unamjua ni muarabu ? Marehemu Shabaani Mloo ni mwarabu ,na wapo wengi tu ,ila Kwa Zanzibar kama huelewi ni kisiwa na kawaida ya visiwa ni mchanganyiko ,halafu naona umechelewa kuleta hiki kirago chako ,Zanzibar ya leo haidanganyiki tena na siasa za kurudisha waarabu ,pole sana.
kudanganyika!!!!
ni heri kudanganyika kuliko kujidanganya. hebu leo hii tuambie, fedha za kuwafadhili UAMSHO zinatoka wapi???
NINI HASA DHAMIRA NA MALENGO YA UAMSHO???
DINI NA SIASA ZINATOFAUTI GANI MBELE YA MACHO NA FIKRA ZA UAMSHO???
katu na haitakuwa zanzibar iwe kama HONGKONG(mwiba katika koo la china).tutawadhibiti kwa siku zote na miaka yote. nawashauri mkajiunge islamic state,alshabaab au alqaeda ili mfundishwe jinsi ya kujilipua.
uzuri ni kwamba mtalipuka na kufa wenyewe
 
ewe punguwani unawajua waasisi wa CUF? Hivi akina Jemus Mapalala wanatoka upande upi wa Pemba? ama kweli wewe ni taahira tena sio kidogo.
UNAJUA NINACHOKIONGELEA ILA UNAJILAZIMISHIA UJINGA.. na sisi wenye akili zetu mwishowe tunakuona mjinga kwelikweli.
UNAMUONGELEA JAMES MAPALALA WAKATI UNAJUA ALIFANYIWA FITNA NA SEIF MPAKA AKAONDOLEWA??? hivi tunaposema muasisi wa TAA(TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION ) alikuwa ni nyerere wewe unadhani nyerere ndio alikuwa wa kwanza kutoa hilo wazo?????!!! yeye nyerere ndiye aliyekifanya TAA kuwa na mtazamo wa kitaasisi na kuweka malengo yanayowasilishika mbele ya watu.. tutaendelea kuwapa darasa kupitia humuhumu
 
asante kwa ufafanuzi lakini hata hivyo natafuta source ya kujiridhisha na haya uliyoyasema.

Kamahuru ilikuwa Zanzibar hasa Pemba. Huku kulikuwa na Chama cha Wananchi chini ya Mzee James Mapalala. Maalim akamrubuni wakaungana na kuwa na CUF ili kutimiza matakwa ya Kikatiba. Baada ya kuungana na kusajili chama, Mzee Mapalala akatoswa!
 
UNAJUA NINACHOKIONGELEA ILA UNAJILAZIMISHIA UJINGA.. na sisi wenye akili zetu mwishowe tunakuona mjinga kwelikweli.
UNAMUONGELEA JAMES MAPALALA WAKATI UNAJUA ALIFANYIWA FITNA NA SEIF MPAKA AKAONDOLEWA??? hivi tunaposema muasisi wa TAA(TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION ) alikuwa ni nyerere wewe unadhani nyerere ndio alikuwa wa kwanza kutoa hilo wazo?????!!! yeye nyerere ndiye aliyekifanya TAA kuwa na mtazamo wa kitaasisi na kuweka malengo yanayowasilishika mbele ya watu.. tutaendelea kuwapa darasa kupitia humuhumu
unamaanisha TANU? maana nijuavyo TAA ilianzishwa mwaka 1925 mwaka aliozaliwa Mwinyi wakati huo nyerere akiwa na miaka 3 tu. au nyerere aliweza kuanzisha chama akiwa na miaka 3? haya endelea kutupa darasa humuhumu.
 
Kwaakili na elimu yako,mpaka leo unakaririshwa kuwa ASP ndiyo waliofanya mapinduzi ya 1964?Unaelewa nini kuhusu vijana shupavu wa UMMA party?Kwataarifa tu Karume na chama chake walidandia mapinduzi ya watu wengine!
 
Abdurahaman Babu wa UMMA Party jembe mojawapo lilitumika kuangusha uongozi wa kiisultani wa Mohammed Shamte,na kuleta mapinduzi ya kweli ndani ya Zanzibar."historia ya sasa imechakachuliwa"
 
Source gani zaidi yetu sisi ambao tulishuhudia?

Mkuu Kimbunga zaidi ya kuona comments zako hapa JF sina cha ziada kuvarify chochote ukiandikacho. hata mimi naweza kuandika chochote kwa hiyo usishangae kutilia shaka kila kinachotupiwa kwenye mitandao na unknown person.
 
Acha hiyo historia yako ya kuchachua, Zanzibar ilikua nchi huru ya kidemokrasia wakati ilipopinduliwa kwa msaada wa askari wa kukodiwa kama wakina Okelo. Ingekua leo wote wangeishia ICC kwa mauwaji ya watu wasio na hatia. SWALI KUBWA muhimu ni je wananchi wa Zanzibar na Tanganyika walihusishwa vipi katika maamuzi ya kuunganisha hizi nchi mbili ? au ni watu wawili tu ndio waliamua kuunganisha nchi ? huu muungano bado haujaaka kwenye nguzo za kisheria !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom