UKAWA haikujiandaa kwa mafuriko haya

UKAWA haikujiandaa kwa mafuriko haya

yoyote yule anaeogopa changamoto kamwe hawezi kufanikiwa maishani mwake. katika vitu vinavyo sababisha kudumaa kwa vyama vya upinzani ni pamoja na mawazo kama haya yako.

ukweli ni kwamba hawa wahamiaji wengi ambao ni viongozi wapo kimtego pia. walipaswa kufanya kama Bulaya na Yule mzee lembeli kwa kuhamia mapema hata kabla ya michakato ya kuenguliwa. subiri utasikia dr titus kamani naye kajiunga na ukawa. hofu hapa tusije kuzalisha kina Arfi na Shibuda
 
Mkuu hata Mwenyezi Mungu huwa anawaumba wengine kuandaa mapito tuu kisha wajibu wao ukitimia anawaweka pembeni. Musa alipewa jukumu la kuwaondoa utumwani wana wa Israel lakini hakuingia nchi ya ahadi na hakulalamika.
Mzee wetu atulie tuu maana mbona tunaiheshimu kazi aliyoifanya na tutamuenzi tuu.

ni hulka ya kibinadamu kuumia pale mambo yanapokwenda ndivyo sivyo. hata yohane hakuamini kuona anaozea jela wakati yule aliyemsafishia njia akiwa hana habari naye
 
SIo kwamba haikujiandaa kwa kimakosa bali pengine haikutarajia haya yanayoendelea. Pamoja na Mbowe kusema wengi watahamia Ukawa na chadema, alisema kimhemko na kihisia kulingana na wakati ule. Lowasa aliwahi kuema wakati bado yuko CCM akiwa Dodoma kuwa mtu hawezi kuzuai mafuriko kwa mikono. Kauli hiyo nayo ilijibiwa kishabiki na Nape ambapo sas anaona wazi jinsi mafuriko hayo yalivyo na madhara. Wako viongozi wengi pamoja na wanachama wengi wa ccm watafurikia Ukawa na hasa chadema. Mbowe aliwahi kusema kuwa mwanachama wa siku moja na wa miaka 20 wote wana haki sawa. Kiuhalisia hii si kweli.

Juzi Arusha tumeshuhudia aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani akihamia chadema mbele ya mkutano wa kumtambulisha Lowassa. Masha si mtu mdogo tu. ana ushawishi kwa vijana hasa wa kanda ya ziwa. Ushawiwi wake utakua baada ya wananchi kuona kahamia ukawa. Hili la Masha kuhamia ukawa nililiona kwa sura mbili; kwanza yeye ni kundi la Friends of Lowassa. Pili hakuwania ubunge jimbo la Nyamagana (jimbo la chadema chini ya Wenje) na badala yake kawania Sengerema kwa aliyekuwa mwanaccm mwenzake, Ngeleja. Hiki ni kizazi cha uongozi na kuja kwao ukawa ina maana kuna utafutaji wa madaraka na si uanachama wa kawaida tu.

Bado tutawaona wanaccm wengi tu ambao ni kizazi cha viongozi wakihamia ukawa na chadema. Hawa watu ukawa wanawapokeaje? Watakuwa wanachama tu au watapewa uongozi kama ukawa wakishika Dola? Kama Prof Kitila alivyomnukuu Nkrumah kwamba 'utafuteni kwanza ufalme wa kisiasa na mengine yatafuata'. Baada ya Oktoba ukawa watajipangaje?

Maono yangu ni kuwa miaka mitano ya ukawa madarakani itakuwa ya mkanganyiko sana maana serikali itakuwa na mseto wa hali ya juu ambao haujawahi kutokea katika Taifa hili. Vipaumbele vitawekwa upande gani?

Kwa upande wa ccm wanaweza kukubali kushindwa na wakakaza moyo na kujikunyata pamoja wakijiuliza ni nini kimetokea. Kisha wakaanza kujianga tena taratibu na baada ya miaka mitano wakawa tishio tena kwa ukawa. Kitakachotokea sasa ni kizazi cha viongozi wa ccm 'wanaokatwa' huko kuhamia ukawa kwa shinikizo na upepo wa mabadiliko. Bado tunawasubiri kina Nchimbi, Kingunge, na tetesi kuwa kuna kina Sumaye na wengine.

Napenda tujadili hili. UKAWA imejiandaaje kwa mabadiliko na mapokezi haya?

Mkuu samahani sana kwa kuku Quote, Niko mbali sana alafu nilikuwa busy sana sikuwa na nafasi ya kuingia jf, ni Laurance Masha yule wa Mwanza ndo amehama?
 
Mkuu samahani sana kwa kuku Quote, Niko mbali sana alafu nilikuwa busy sana sikuwa na nafasi ya kuingia jf, ni Laurance Masha yule wa Mwanza ndo amehama?

yap. ni yule aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani
 
umepotea sweety!! si jui ni nini kimekukuta pande za huko!!! au Tsunamni ya Lowasa nini????

Hata tsunami hutulia yenyewe haihitaji mtu kuizuwia.

Binadam anaefata mafuriko huyo hajielewi, anakwenda na maji.
 
Kkwamba UKAWA wakishindwa watakwenda wapi ...hii ni akili finyu isyokuwa ya kijemedari...tunataka watu daring...eti ukawa wakishindwa...na so what...yaani opportuinstic minds huwa ni malsahi zaidi...mis powers umekosea...ukitaka mafanikio usilenge kupata tu!

Wengi wanaoshindwa kwenye kura za maoni majimbon mwao, ndio wanaohamia Ukawa.. Wakijua kbsa Ukawa inaweza ikashinda na wenyew hawataachwa.. Hasara watapata pale Ukawa itaposhindwa, cjui wataelekea wap tn! maana wanahama kwa mbwembwe hao, kurud kwao itakuwa aibu kubwa..
 
katika hali halisi hivi kuna anayeweza kuchagua pakuelekea akizolewa na mafuriko?

Katibu Mkuu wa chadomo babu daktari wa kanoni padri Dr.W.Slaa yuko wapi? Au na yeye kakumbwa na mafuriko?
 
Back
Top Bottom