Ni jambo jema chadema kupata wageni wengi kiasi hicho, ila pia na wao wajitafakari sana ujio wa wageni hao, na wengi wao ni wale wanaoshindwa kwenye kura za maoni. na hao wageni wengi wanaingia chadema si NCCR wala CUF au NLD, hao wageni wengi wao wanataka nafasi za uongozi kwenye hicho chama, hasa ubunge na hatimaye waweze pata uwaziri wenye uzoefu wa kazi, kwani UKAWA ndo kuna nafasi nyingi za kugombea, Mbowe alisema kwamba kutatokea mabadiliko kwenye nafasi za ubunge, maana yake kuna nafasi walizochaguliwa za ubunge kubadilishwa kwa kiasi kikubwa, wataanza kuchomoa wa zamani na kuweka wapya wa mzee Lowasa,
Lakini nimeona baadhi ya vijana leo wanasema Dr. Slaa ana uroho wa madaraka, wamekwishasahau mroo wa madaraka, je ni sahihi kusema maneno hayo? vijana wanatumika vibaya sana, haya mageuzi yote yameletwa na akina Dr, na pia inatakiwa wafurahie matunda yao, ss kama ndo tunafanya hivo si jambo jema sana.
Angalizo langu, kama UKAWA wakishindwa uchaguzi huu, basi ni wazi kwamba upinzani utashuka sana sana, na itawachukua tena muda mrefu kuaminiwa na wanachi, je ni nani atayekubali kuimalisha chama alafu kikipendeza watu wanazamia? siku zote unapotafuta faida ujue pia na hasara ipo. Hao wazee kukaa pembeni iko siku watajua nn kiliwafanya wakae pembeni.