MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wakuu ninaandika haya nikiwa nimepata kusikia wanaCCM wakijitapa mahali kua UKAWA kwa sasa bungeni hakutakua na wa kumnyooshea mtu kidole kwa sababu wao wenyewe wamekaribisha mafisadi ndani ya vyama vyao hakua ajenda tena! Niliposikia hili nikahusianisha na yale maneno ya juzi ya vijembe vya waziri wa habari,vijana,sanaa na michezo ndg Nape Nnauye kua eti "UKAWA wakitaka kuwa safi tena wamfukuze Mh Lowassa"
Kama kweli haya ndio maneno ya wanaCCM basi 2020 lolote laweza kutokea katika uchaguzi mkuu, uhakika wa ushindi bado ni mkubwa. WanaCCM wamebweteka na kuridhishwa na utendaji wa miezi michache iliyopita chini Rais Magufuli wakatia mikono mifukoni, hili halitawapeleka Salama 2020 nawaambia.
Hivi ccm hizi changamoto kwa Magufuli wameziona na watie mikono mifukoni?
1. Mgogoro wa kisiasa huko Zanzibar,
2.Upatikanaji wa katiba mpya,
3.ESCROW bado haina majibu na wahusika bado wanazawadiwa vyeo,
4.Elimu bure utekelezaji wake unahitaji kujipanga,
5.Ujenzi wa Zahanati kila kijiji,
6.Kudhibiti Rushwa
7.Utozaji mkubwa wa kodi kwa wafanyakazi,
8.Utitiri wa kodi serikali za mitaa.
Kwa ufupi hizi zote bado ni ajenda kubwa sana upande wa upinzani CCM wasiweke mikono mifukoni.