Ukatili wa Polisi Arusha:Mbunge Joyce Mukya anyimwa kumnyonyesha mtoto mchanga mwenye miezi Miwili

Polisi kwa nini mnanilazimisha kuwachukia hata ndugu zangu ambao ni askari?!!!!! I hate polisi'

Mkuu tuko pamoja kwa hilo!
Nina mtoto wa mdogo wangu kijana amemaliza shule akaniambia anataka kwenda Chuo cha Polisi kusomea uaskari polisi nikamwambia ukitaka udugu ufe kasomee upolisi...
Inatisha sana, kwa kuwa nina hakika wengi wetu tunao ndugu zetu askari polisi, tunaishi nao majumbani mwetu, lakini tulipofika sasa watu tunakosa hata imani nao. Ninaamini kabisa kuna baadhi yao wakipewa amri kuumiza ama hata kuua raia wasio na hatia akili zao za kuzaliwa zinaenda likizo ndefu...
 
Hii sasa ni kufuru katika ukiukaji wa haki za binadamu. Ni vema sasa viongozi wa nchi wakatathmini namna vyombo vya dola vinavyoendehwa na watu waliowapa dhamana na kujirekebisha. Hii itaichafua sana serikali, wakati labda ni mtu mmoja tu aliyetoa amri hiyo ya kipuuzi.
ndio akina nani hao!?
 
Unamnyima mtoto maziwa ya Mama??? Kweli??? Wazee hii mbaya acheni bwana.
 
Tangia lini Polisi wamekuwa na Utu, hii thread haina mashiko kwasababu Polisi wetu siyo wageni kwa ukatili, hivi Polisi wangekuwa na Utu unadhani mauaji yanayoendelea nchini kama ya akina Mwangosi yangekuwepo? na kama siyo maagizo ya Rais wahusika wangepandishwa vyeo na kuongezwa mikataba kwa kufuata vizuri maagizo?
 
Huu ni ukatili na unyanyasi dhidi ya watoto, tena kitoto kichanga cha miezi miwili!

Wana Jf kama mnavyokumbuka jana Mbunge Joyce Mukya alikamatwa na polisi katika vurugu zilizotokea jana, akiwa pamoja na wabunge wengine watatu Tundu Lissu, Said Arfi na Mustapha Akonaay.
Joyce Mukya aliletewa mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili ili akamnyonyeshe, Polisi wakakataa wakasema hatamnyonyesha, na kweli mtoto hakunyonyeshwa mpaka hivi tunavyoongea, tokea Mh. Joyce akamtwe jana na polisi!

Inasikitisha, inasononesha kwa kila binadamu mwenye moyo wa utu kuona haya yanatokea. Sijui kwanini jeshi letu linatumika kunyanyasa raia hasa watoto.

Polisi wanamnyima mtoto mdogo asinyonye maziwa ya mama, kana kwamba wao hawakuzaliwa na mama na hawajawahi kunyonya.

Mambo mengine ndugu zangu tuweke siasa pembeni, polisi wetu watangulize utu mbele.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Hoja ya CCM hapo ni kwamba mtoto huyo wa Mukya amezaa na Mbowe hivyo wanalipa visasi!!
 
Ngoja nirudi ofisini faster, maana nahisi kuchemka kiasi kwamba nikikutana na polisi naweza kumchanachana kama simba.
 
kuwa na mtoto mchanga wa miezi miwili na kumuacha mtoto nyumbani na kuenda kwenye maandamano,huo ni uzembe wa huyo mama,na anastahili kuwa mahabusu,hana tofauti na wale wanaotupa watoto,au wale wanaowaacha watoto na kwenda disco.
 
Polisi wengi wa Tanzania ni zao la wananchi waliokata tamaa ya maisha baada ya anguko la kielimu, hivyo kimbilio pekee kwao ni jeshi hilo.
Usitegemee hata siku moja mtu wa namna hii kuwa na roho ya kibinadamu au hata kuipenda na kuthamini kazi yake...
 
  • Thanks
Reactions: mob
Unamnyima mtoto maziwa ya Mama??? Kweli??? Wazee hii mbaya acheni bwana.

Hivi mkuu mfano wewe, kama mkeo kakamatwa kwenye maandamano halafu nyumbani kaacha mtoto wa miezi miwili utamfanyaje?? tuache siasa ongea kama a reasonable man...
 
ee Mungu wangu hawa si ndo wasimamizi wa haki za binadamu kumnyima malaika wa bwana kunyonya ni sawa na kumnyima chakula malaika.Naamini iko cku tutajaulizwa ulitenda mema sana ila nilikuja kwako kama mtoto mdogo unipe maziwa ya mama ukashindwa kunipa..................................................................
 
swali la kujiuliza, hivi kweli mama mwenye mtoto, unatoka wapi kwenye maandamano??
pum***vu sana alikua anaandamana au alikuwa anaaga marehemu kama nyinyi ambavyo huwa mnaaga wakwenu?mijitu mingine bwana shkuru jf hai2oneshi mnapopatikana watu kama wewe maana tukianza kuwaondoa nninyi mafanikio yataonekana tumalizie na wakubwa wenu
 
Huu ni ukatili na unyanyasi dhidi ya watoto, tena kitoto kichanga cha miezi miwili!

Wana Jf kama mnavyokumbuka jana Mbunge Joyce Mukya alikamatwa na polisi katika vurugu zilizotokea jana, akiwa pamoja na wabunge wengine watatu Tundu Lissu, Said Arfi na Mustapha Akonaay.
Joyce Mukya aliletewa mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili ili akamnyonyeshe, Polisi wakakataa wakasema hatamnyonyesha, na kweli mtoto hakunyonyeshwa mpaka hivi tunavyoongea, tokea Mh. Joyce akamtwe jana na polisi!

Inasikitisha, inasononesha kwa kila binadamu mwenye moyo wa utu kuona haya yanatokea. Sijui kwanini jeshi letu linatumika kunyanyasa raia hasa watoto.

Polisi wanamnyima mtoto mdogo asinyonye maziwa ya mama, kana kwamba wao hawakuzaliwa na mama na hawajawahi kunyonya.

Mambo mengine ndugu zangu tuweke siasa pembeni, polisi wetu watangulize utu mbele.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Hatuna polisi wenye weledi.....most of them ni losers...mwingine aliwahi kuwa RPC Arusha... alitokea u-house boy mpaka RPC...imagine utayakuta yanazunguka na mibunduki kama mazuzu vile. Jana Arusha wako happy kufyatua mabomu ya machozi mpaka yanaingia katika ofisi na na nyumba binafsi. Mijitu mizima inafanya kazi kama robbot haya-reason .. wasted my time kuzungumzia hopeless people....Poleni kwa ukali wa maneno limeniuma sana swala la kukataliwa kunyonyesha mtoto.
 
Back
Top Bottom