Ukatili wa Polisi Arusha:Mbunge Joyce Mukya anyimwa kumnyonyesha mtoto mchanga mwenye miezi Miwili

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Huu ni ukatili na unyanyasi dhidi ya watoto, tena kitoto kichanga cha miezi miwili!

Wana Jf kama mnavyokumbuka jana Mbunge Joyce Mukya alikamatwa na polisi katika vurugu zilizotokea jana, akiwa pamoja na wabunge wengine watatu Tundu Lissu, Said Arfi na Mustapha Akonaay.
Joyce Mukya aliletewa mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili ili akamnyonyeshe, Polisi wakakataa wakasema hatamnyonyesha, na kweli mtoto hakunyonyeshwa mpaka hivi tunavyoongea, tokea Mh. Joyce akamtwe jana na polisi!

Inasikitisha, inasononesha kwa kila binadamu mwenye moyo wa utu kuona haya yanatokea. Sijui kwanini jeshi letu linatumika kunyanyasa raia hasa watoto.

Polisi wanamnyima mtoto mdogo asinyonye maziwa ya mama, kana kwamba wao hawakuzaliwa na mama na hawajawahi kunyonya.

Mambo mengine ndugu zangu tuweke siasa pembeni, polisi wetu watangulize utu mbele.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Wakulaumiwa ni sisi wananchi tunaokubali kuendelea na jeshi la polisi wauaji ,kama wanapiga risasi na kufumua ubonggo motto wa miaka saba unadhani wa miezi miwili wa tamjari na akisogezwa karibu Chagonja atamnyonga kabisa ndio squad imara inayoaminiwa na Mwema baada ya kupewa nishani ya kutukuka
 
chago.jpg Majitu kama chagonja wana roho kama masokwe
 
Wakulaumiwa ni sisi wananchi tunaokubali kuendelea na jeshi la polisi wauaji ,kama wanapiga risasi na kufumua ubonggo motto wa miaka saba unadhani wa miezi miwili wa tamjari na akisogezwa karibu Chagonja atamnyonga kabisa ndio squad imara inayoaminiwa na Mwema baada ya kupewa nishani ya kutukuka

Mkuu jeshi la polisi wameamua kwa makusudi kutumia silaha kuwapiga raia. Polisi ni adui namba moja wa raia
 
Hii sasa ni kufuru katika ukiukaji wa haki za binadamu. Ni vema sasa viongozi wa nchi wakatathmini namna vyombo vya dola vinavyoendehwa na watu waliowapa dhamana na kujirekebisha. Hii itaichafua sana serikali, wakati labda ni mtu mmoja tu aliyetoa amri hiyo ya kipuuzi.
 
Angalia hao policcm wasije wakasema hatujamruhusu kwa sababu labda maziwa ya mama yatakuwa yameathiriwa na moshi wa mabomu....:disapointed:
 
Polisi kwa nini mnanilazimisha kuwachukia hata ndugu zangu ambao ni askari?!!!!! I hate polisi'
 
Mkuu jeshi la polisi wameamua kwa makusudi kutumia silaha kuwapiga raia. Polisi ni adui namba moja wa raia
Mungi na kubali kabisa Polisi ni adui namba moja wa raia lakini tujiulize je tunahitaji kuwa na jeshi la polisi kama hili kila siku nikuuwa,kwa mwezi wana wastani wwakuwaondolea uhai wananchi 150 na sisi tumenyamaza si tutaisha kweli na kuwa na sampuli za askari kama akina chagonja wanaofikiri kwa masaburi
 
Kwa nini kujitafutia chuki na wananchi kiasi hiki? Sasa nimejua kwa nini kule Iraq kila siku utasikia vituo vya polisi vinalipuliwa, kumbe yaweza kuwa chuki zidi yao kwa matumizi mabaya ya nafasi zao kama polisi.
 
Ile kauli iliyowahi kutolewa na mkuu wa nchi kwamba CCM wasitegemee kusaidiwa na polisi, je ilikuwa ni changa la macho?
 
aiseeeee babayangu hi serekali muda si mrefu itaanguka kwanini chadema isitupe mabomu na a k 47 tuingie kazini mimi nitakula saani moja na kova
 
Akimaliza tatizo hili afungue mashtaka mahakamani kwa kitendo alichofanyiwa cha kunyimwa haki ya msingi ya kumnyonyesha mtoto wake.
 
Inasikitisha tanzania ya sasa si ile ya miaka ya 1980, chonde selikali muwaelimishe polisi wajue selikali ilikubali yenyewe mfumo wa vyama vingi ili kuleta demokrasia, sasa kuvibana vyama vingine inakuaje? Polisi wanafanya kazi kama wao ni ccm wanapendelea upande mmoja, wanasiasa wa ccm wanatumia jeshi la polisi ni hatari sana hata sisi ambao ni ccm tunachukia tupambane kwa hoja na sera tuwajubike tusitumie nguvu lugha kama za kina nape na mwigulu zinatupoza chama hakina washauri? Kikwete una busara nyingi ebu weka mambo sawa haya ya arusha bomu hadi kuvuruga watu wasiage yanaonyesha selikali inanyanyasa chadema mbona bomu la kanisani marehem waliagwa tena kwa maandamano?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom