Uganda: Mwanamke amzika mtoto wake wa miezi miwili akiwa hai

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Polisi katika Wilaya ya Apac nchini Uganda wameanza uchunguzi dhidi ya mwanamama anayedaiwa kumzika akiwa hai mwanaye wa kiume mwenye umri wa miezi miwili.

Imeelezwa kuwa Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kijiji cha Awiri katika Parishi ya Kidilani katika mji wa Chegere alichimba kaburi na kumzika mwanaye siku ya jana (Jumatatu)

Imesemekana kuwa mwanamke huyo alifikia hatua hiyo baada ya wazazi wake kumnyima chakula wakidai kuwa amezaa mtoto haramu.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alitoweka na mtoto wake nyumbani kwao kwa muda wa siku tatu na aliporudi siku ya Jumatatu hakuwa amerudi naye.

Vyombo vya usalama wilayani humo vimethibitisha kujiri kwa tukio hilo na kusema kuwa vinaendelea na uchunguzi.

Imearifiwa kuwa baada ya kuulizwa kueleza alipo mtoto wake, mwanamke huyo alikiri kuwa amemzika akiwa hai, na kudai kuwa ni baada ya yeye na mwanaye kutengwa na familia yake.

Mtuhumiwa huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Apac

*******

Police in Apac District are investigating the circumstances under which a teenage mother allegedly buried her two-month-old son alive.

The 19-year-old resident of Awiri Village, Kidilani Parish in Chegere Sub-county allegedly dug the grave and buried her son on Monday.

Sources say that the incident happened after the suspect’s parents denied her food on grounds that she had given birth to a bastard.

Catherine Eunice Agwang, Officer in Charge of Criminal investigations in Apac, confirmed the incident, and noted that they were investigating the matter.

“We are going to seek a court order to allow us exhume the body and examine it to find the exact cause of the child’s death,” she said.

The suspect is detained at Apac Central Police Station.

He says that when the suspect was pressured to disclose the whereabouts of her child, she confessed that she had buried the baby alive.

“She told us that she buried the child over frustration that her family has neglected her and the baby,” Mr Okello says.

Source: Daily Monitor
 
Mi ndiyo maana siyo hakimu. Kesi ngumu ngumu kama hizi hata siziwezi.
 
Dah kumnyima mtoto chakula kisa ni haramu kweli,hao wazazi wake nao wanamkosa pia maana mtoto hana hatia yoyote.
 
Hata dunia nzima imkatae mtoto wangu, bado nitasimama mpaka mwisho, she has no motherhood in her, mtoto niliyembeba tumboni miezi tisa hakuna wa kunifanya niutoe uhae wake labda Mungu aamur kukatisha maidga yake,huyo mama ni katili anatakiwa kunyongwa hadi kufaaa
Dah kumnyima mtoto chakula kisa ni haramu kweli,hao wazazi wake nao wanamkosa pia maana mtoto hana hatia yoyote.
 
She is just19.. Kuna watu huo umri ni bado watoto sana kifikra na kufanya maamuzi sahihi
Hata dunia nzima imkatae mtoto wangu, bado nitasimama mpaka mwisho, she has no motherhood in her, mtoto niliyembeba tumboni miezi tisa hakuna wa kunifanya niutoe uhae wake labda Mungu aamur kukatisha maidga yake,huyo mama ni katili anatakiwa kunyongwa hadi kufaaa
 
Been just 19 is ot a point ya kuua mtoto, wanawake ni walezi, mimi tangu nipo darasa la nne mama anenda shamba ananiachia mfogo wangu wa miaka mieili na nimemlea, sasa at the age of 19 manake meanamke wa kiafrika ana uweza wa kuachiwa hata mtoto wa mwezi mmoja na akalea mpaka akakua
She is just19.. Kuna watu huo umri ni bado watoto sana kifikra na kufanya maamuzi sahihi
 
Hata dunia nzima imkatae mtoto wangu, bado nitasimama mpaka mwisho, she has no motherhood in her, mtoto niliyembeba tumboni miezi tisa hakuna wa kunifanya niutoe uhae wake labda Mungu aamur kukatisha maidga yake,huyo mama ni katili anatakiwa kunyongwa hadi kufaaa
Nakupendaga wewe daaah... aliyekuoa amebahatika sana kuishi nawe Mama.
 
Back
Top Bottom