Ukatili wa Kijinsia katika zama za sasa nini kifanyike ?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
Katika Kipindi cha miaka iliyopita, utamaduni ulikuwa ni moja ya sababu kubwa zilizopelekea Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia kuwa sababu kubwa ya mateso Katika Jamii,wengi waliathirika kisaikolojia, kimwili na wengine kiroho kwa kupoteza Maisha yao na wengine kupata matatizo ya kiafya ya kudumu ambayo waliishi nayo na wataishi nayo Katika Maisha yao yote.

Baada ya Elimu kutolewa na sheria kali kutumika, Unyanyasaji na Ukatili dhidi ya Wanawake ulipungua kwa asilimia kubwa japo hatuwezi kusema kwamba ulipotea moja kwa moja.

Vitendo kama Ukeketaji vilikuwa vimeshamiri Katika Jamii nyingi na hata baadhi ya Jamii kuchukulia kuwa bila ya Ukeketaji ,Mwanamke hawezi kuwa salama Katika ndoa yake, na anaweza kuwa sehemu ya laana kwa sababu tu ya kuolewa bia ya kukeketwa.

Ukeketaji ulisababisha vifo kwa watu wengi na wengine kubaki na matatizo Katika mifumo yao ya kiafya.

Leo hatuna budi kutazama matatizo ya Ukatili wa Kijinsia na unyanysaji ambao bado upo sana Katika Jamii zetu ingawa baadhi yao hayaonekani wazi kwa watu wengi kwa sababu ni sehemu ya Ukatili unaofanyika ndani ya majumba yetu na kubaki kuwa siri.

Wanawake wengi kwa sasa wamekuwa ni wahanga wakubwa wa vipigo Kutoka kwa waume zao au wapenzi wao, wengi wamekuwa wakiishia kupata maumivu Katika miili yao na wengi wamekuwa wakibaki kuwa wasiri kutokana na vitendo wanavyofanyiwa.

Wanawake wengi wanaokumbana na vitendo vya kupigwa, wanakuwa hawafahamu ni taratibu gani wachukue ili kuondokana na madhila hayo, wengine huishia kukalishwa chini na kufanyika vikao vya upatanishi ambavyo bado kwa upande mwingine havimalizi matatizo ya Wanawake kupigwa na waume zao, na Wanawake wengine huchukulia hali hiyo kuwa ya uvumilivu na kuona kuwa hawana namna zaidi ya kukubali kuishi Katika Maisha ya aina hiyo ili kuendelea kuhudumia Watoto na familia zao.

Kutokana na Dunia kuwa Katika zama za teknolojia na Mawasiliano ambayo inakuwa kila siku, huku aina mbalimbali za mitandao ya kijamii na watumiaji wa internet wakiongezeka.

Hali ya utumiaji wa mitandao imekuwa ikihusisha pia baadhi ya watu waovu na wasio na maadili kutumia kama mwanya wa kuwanyanyasa Wanawake kwa kuweka maudhui ama kusambaza picha zisizofaa kwa malengo ya kuwadhalilisha Wanawake huku wakisahau kuwa kitendo hicho kinawatesa Wanawake kisaikolojia Pamoja na kuwatesa watu wanaofahamiana na Mwanamke huyo ama ndugu zake na jamaa zake wa karibu Pamoja na kudhalilisha utamaduni wa mtanzania.

Mbali na kuwa usambazaji wa maudhui yasiyofaa dhidi ya Wanawake ni mateso ya kisaikolojia lakini pia ni sababu ya kumfanya Mwanamke huyo kuingia Katika mgogoro wa kiajira kwa sababu waajiri wengi hawakubali kirahisi kumuajiri mtu ambae wanahisi hana maadili mema Katika Jamii.

Wanawake na wasichana wengine wamekuwa ni sababu ya picha na video zao kusambazwa Katika mitandao ya kijamii hasa kwa wao kukubali kupigwa picha ama kujipiga picha kwa hiyari yao na kutuma kwa wapenzi wao ambao baadae kwa nia mbaya kabisa ama kama njia ya kupiza kisasi hutumia picha na video hizo kwa kuziweka mtandaoni.

Siyo tu kwamba sheria kali zinahitajika kuwekwa ili Kupambana na Ukatili wa Kijinsia, bali Jamii inapaswa kuelimishwa zaidi kuhusiana na vitendo hivi vya kikatili na Unyanyasaji dhidi ya binadamu, watu wengi wanapaswa kuelimishwa juu ya kuepuka kufanya vitendo vya Ukatili.

Wanaume kama sehemu ya Jamii wanapaswa Kushirikishwa na kuelewa ni namna gani wanashiriki kufanya ama kufanyiwa Ukatili wa Kijinsia, tatizo kubwa lilipo sasa ni Elimu hii kuwafikia baadhi ya watu wachache huku wengi wakiwa hawana uelewa.

Vyomba vya habari vinaweza kutumika na kuwa na vipindi vingi vya kuelimisha kuhusu Ukatili, wasanii wa sanaa mbalimbali ni wakati wao sasa kutumia sanaa zao kuelimisha kuhusu Ukatili kwa Kijinsia.

Ukatili wa Kijinsia ni tatizo letu sote, tusimame Pamoja, mambo yatakaa sawa,

Idd Ninga
Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom