Ukatili ni tokeo la udhaifu fulani ndani ya mtu

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,054
Hello bosses and roses....

Hivi umeshagundua kuwa watu wakatili ni watu ambao wana udhaifu (weaknesses) fulani ambazo hawataki kuzikubali na hivyo kutaka kutumia ukatili kujidanganya (kutengeneza illusion) kwamba wana nguvu au wana control na hali yao kumbe sio.

Wengi utakuta aidha ni mtu mfupi ila hajikubali kwa ufupi wake, au ana maumbile madogo au hata hana nguvu za kiume (kwa wanaume), au ni homosexual asietaka kujulikana (in closet), etc........

Madhaifu hayo hufanya hawa watu kutokujikubali na hivyo kutumia ukatili kujipa moyo (kujidanganya) kwamba wana-control situation na kulazimisha waogopeke au waheshimiwe.

Utakuta mtu anapenda kupigana tu hovyo, tumewaona baadhi hata kwenye vyombo vya media wao wanawapiga hadi watu wanaohojiwa huko. Mtu analazimisha kuheshimiwa, mtu analazimisha kutambulika kwamba ana mamlaka fulani. Hayo yote ni viashirio kwamba huyo mtu nyuma ya pazia ana udhaifu mmoja hatari ambao aidha hataki watu waujue au kama wanaujua basi hajajikubali.

Hili ni gonjwa la kiakili(kisaikolojia), na magonjwa kama haya ni hatari zaidi kuliko hata BP, HIV na Covid kwa sababu kwanza wagonjwa wengi huwa hawajui kama wanaumwa na pili wagonjwa kama hawa ukiwapa madaraka hata 'ukiranja' tu basi yatakayotokea nadhan mtaelewa.

Kama Seneca alivyowahi kusema "All cruelity springs from weakness" basi kama ukikutana na mtu katili basi jua kabisa hio ni escape route yake anayotumia kujidanganya kwamba yupo 'in-control'.

Na kuna watu wanaweza kuchanganya haya maneno 'UKATILI' na 'MSIMAMO MKALI'. Mtu kuwa na msimamo mkali haimaanishi ni katili, kwa hio hapa siongelea wenye misimamo mikali.

Happy fridaying.....
~Kali Linux
 
Huwa wanakuwa narcissist.
Jitoe muhanga kukaa nao karibu sasa watakubebesha kila mzigo wa lawama.

Kama ni wapenzi utateswa kimwili (vipigo)na kihisia ( kashfa na matusi) mpaka unajiuliza nimekosea wapi kuonyesha upendo kwa huyu mtu.
Point.
 
Bandiko bora kabisa....

Bandiko muruwa haswa

Kongole kamarada

Kinyume na hayo mazuri uliyotudadavulia kamwe mwanadamu hathubutu kuwa katili...

Na pia CHILD ABUSE inachangia sana POST-TRAUMATIC STRESS DISORDER (PTSD).....

Watu hao wakiwa "maboss" wako...kazi utakuwa nayo huko kazini

Ukiwaangalia kwa nje wanajiamini sana...wanapendeza sana.... ndani ni "empty" na ILLUSION kwa kwenda mbele....

#Siempre JMT
 
Back
Top Bottom