Ukatili katika malezi

Ukatili katika malezi

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
UKATILI KATIKA MALEZI

Katika sayansi ya saikolojia ya ukuaji wa mtoto, kuna ukweli mmoja usiopingika: mtoto huchukua sauti ya mzazi wake kama sauti ya dunia.
Anaposikia matusi badala ya busara, anapopigwa kupita kiasi badala ya kuelekezwa, anapolaaniwa badala ya kufundishwa,mtazamo wake wa kidunia huvurugika, na msingi wa kujithamini huanza kuporomoka.

Mzazi anayepayuka kila kosa, anayetoa laana kana kwamba ni maelekezo ya kawaida, huacha makovu yasiyoonekana kwa macho lakini yanayoathiri ubongo wa mtoto moja kwa moja.

Tafiti zinaonyesha kuwa watoto wanaolelewa katika mazingira ya ukali usio na kiasi huathirika kisaikolojia, hujenga hofu ya kudumu, hukosa uwezo wa kujiamini, na mara nyingine huishia kuwa na matatizo ya mahusiano ukubwani.

Lakini haimaanishi kuwa watoto hawapaswi kuadhibiwa. La hasha. Nidhamu ni nguzo ya malezi bora. Lakini nidhamu ya kweli huambatana na maadili, kiasi na busara. Mtoto hapaswi kuadhibiwa kwa hasira ya mzazi bali kwa lengo la kumrekebisha, kwa njia anayoelewa, na kwa lugha inayojenga. Adhabu yoyote inayodhalilisha hailekezi, bali huharibu.

Maneno laini hayamaanishi udhaifu, huonyesha ustaarabu wa akili na ukubwa wa moyo.
Kumpa mtoto nafasi ya kuelewa kosa lake, kumuonyesha njia sahihi, na kumkumbatia baada ya makosa, humjenga na kuwa mtu kamili. Kumpiga bila kiasi, kumtukana kila siku, au kumlaani, ni sawa na kumfundisha kuwa hapendeki. Na mtu anapojifunza kuwa hapendeki, huacha hata kujiokoa.

Mzazi, kabla hujasema neno gumu au kunyanyua mkono, jiulize: "Je, nafundisha au ninalipiza hasira zangu binafsi?"

Maana hakuna adhabu mbaya kama mzazi aliyechoka kihisia, anayetumia mtoto wake kama sanduku la maumivu yake mwenyewe.

Abuuabdillah ✍️

#MaleziYenyeMaarifa
#SayansiYaMalezi
#TujengeTusiadhibu
#MzaziMwalimuWaMwisho
#Mahusianoseason
 
Well said, nafanya meditation sana kuondoa hizi hasira zangu za karibu, nimegundua ni makaripio niliyokua nayapata kila siku kutoka kwa mzazi
 
pole sana utakaaa sawa sababu umejua tatizo
Nimekua nashindwa kuzuia hasira kisha najutia maamuzi baadae, hii pia imenifanya hata nikiwa na furaha sana najiachia na kufanya vitu ambavyo sometimes sio vya kawaida, sio kumlaumu mzazi ila hata sasa nimekua nikirudi nyumbani nikiona madogo wanavyokaripiwa kila wakifanya kosa hata dogo sana naona wanavyokosa kujiamini na kufanya vilevile wakikosana na watoto wenzao,
Sababu wanaona ndio njia waliyofundishwa ya kukabiliana na mtu aliyekukasirisha,
Ni ngumu kutoka huku ila najikaza niwe nice person kabla sijawa na familia sababu nitawarithisha watoto tabia ambayo siipendi,
Malezi ya kiafrika yana faida na hasara zake, kulelewa hivyo kumenipa faida ya kuwa na discipline kitu kinachonifanya nikubalike kila ninapoenda sababu ya nidhamu yangu japokua ni ya uoga
 
Back
Top Bottom