Ukatili huu mpaka lini?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Mkono wa mtoto Clement unavyoonekana baada ya kuunguzwa na mama yake mzazi kwa kisa cha kuiba mkate.
Kiukweli mi sina lakusema kuhusiana na hili, kwa maana mpaka sasa najiuliza inakuwaje mzazi unaamua kumfanyia mtoto tena wakumzaa mwenyewe ukatiri wa dizani hii na kumpa mtoto kilema cha makusudi bila hata ya huruma, bila kupata majibu.

20100821092349_1.jpg

20100821092349_2.jpg

20100821092349_3.jpg
 
hivi hizi mimba zao zinakuwagaje jamani mpaka inatokea mtu huna uchungu na mwanao uliembeba miezi 9 na kujikakamua labour mpaka dk ya mwisho, nahic hizi ni tofauti na mimba za wanawake wengine...khaaa hapana jamani....
 
Adhabu yao ni kuchomwa na wao huko huyo mtoto alikotokea....:mad2::mad2::mad2:

Watu wengine wanafanya tunapata dhambi bure....:pray::pray::pray::amen:
 
Watoto wa kupewa na waganga wa kienyeji hawana uchungu hata kidogo
hivi hizi mimba zao zinakuwagaje jamani mpaka inatokea mtu huna uchungu na mwanao uliembeba miezi 9 na kujikakamua labour mpaka dk ya mwisho, nahic hizi ni tofauti na mimba za wanawake wengine...khaaa hapana jamani....
 
Kuzaa mtoto isiwe sababu. Wazazi wengine ni wanyama hata kwa watoto wao na wanadhani wana haki ya kumpa mtoto adhabu wanayoamua wao. Hii ni mentality ya ki-afrika zaidi na imepitwa na wakati. Inabidi tuendane na mabadiliko ya wakati. Sipingi uwepo wa adhabu ila adhabu iwe ya kiasi na iendane na kosa na umri wa mtoto. Mi nakumbuka nilivyokuwa mdogo kuna watoto wenzangu walikuwa wanapigwa na wazazi wao mpaka wanapoteza fahamu. Mnakumbuka ile stori ya mtoto alifanya kosa akaunguzwa sehemu za siri? Just imagine mzazi anachoma sehemu za siri za mwanae! Huyu si mzazi, ni mnyama. Halafu hakuna hatua yeyote inachukuliwa. Ndo maana watoto wengine akili zimevia kwa ajili ya vipigo visivyo na udhibiti toka kwa wazazi wao. Iko haja ya wazazi kudhibitiwa na jamii kuhusu hizi adhabu zisizo na tija!
 
hii tunaiita internecine violence. pale ambapo mtu anafanyiwa maovu na kushindwa kulipiza kwa mhusika ndio anaamua kuzimalizia kwa mwingine. hii huwakumba sana watu kama walimu, manesi, wanawake walioolewa n.k. cha msingi ni kujidhibiti tu
 
unajua bwana ukatili huu hakika Mungu msamehe mama huyo kiukweli wanawake akili zao hazifanyi kazi vizuri na wao ndo chanzo cha maovu na kumuasi Mungu wanawake hawahawa walisababisha si unaona ongezeko la ngono zembe now days wanawake kuacha manyonyo yao nje,makalio nje,nguo za ndani nje yaani kwanini Mola alimpa Adam janga hili wanawake nyie vipi mmeshatukosanisha na Mungu basi inatosha badilikeni tuungane pamoja kufanya toba jamani aaaaaaah
 
Tamko la kijumla na la kmfumo dume kama hilo (bold hapo juu) sio sahihi na linawachokoza wanawake.
 
Back
Top Bottom