Ukarimu wangu umeniponza

Ukarimu wangu umeniponza

Wewe acronomy ni mtu wa ajabu sana jamaa kachukua maamuzi kuhusu familia yake wewe unakuja kulialia hapa.

Nakuunga mkono pia,kwani kafanya kosa kuamua kuwa responsible na familia yake au mdau ulitaka wew ndo uwe unawapeleka.
 
ha ha haa Preta acha basi lile subaru lako kesho nyumbani sema limeharibika nikupitie nikupe lifti aki vile.

He he he.........kesho napumzika.......leo nilichoka sana nilikuwa namdhamini rais.......halafu Subaru zaidi naitumia summer........
 
Ningekutatiria mbali shit unambeba mke wangu ww km nani... tena uache kimbelembele hicho tulia na familia yako.. ole wako urudie nitakuua
 
Wana MMU,

Nimekuwa nikichangia mada za wengine ila leo yamenikuta. Mahali ninapoishi kuna nyumba tano ambazo ni za mtu mmoja, zimezungushiwa ukuta na wote kwa pamoja. Tupo familia tano kama idadi ya nyumba zilizopo. Binafsi mi ni wa mwisho kuhamia hapa, hizi familia nyingine zipo kwa muda sasa.

Moja kati ya familia hizi nilibahatika kujenga nao urafiki kwa kuwa baba wa familia tunatoka mkoa mmoja, yeye ni mtu mzima kiasi ana mke na pia anaishi na mdogo wake, yeye pamoja na mkewe ni wafanyakazi katika ofisi tofauti, mdogo wake yeye ni mwanachuo. Jamaa ana gari ambalo hulitumia kumpeleka mkewe kazini na kumpitisha mdogo wake chuoni asubuhi.

Baada ya mimi kuhamia hapa nikawa nawapa lift mke na mdogo wake na huyu jamaa kwa kuwa kibaruani kwangu ni uelekeo mmoja na anapofanya kazi mke wa jamaa na anaposoma mdogo wake. Hili halikuwa tatizo kwangu kwa kuwa ni kawaida yangu kuishi vizuri na jirani zangu.

Hali imeendelea hivi kwa miezi mitatu sasa lakini jana jamaa akaja kunisalimu usiku wa saa mbili na kuniambia kuwa kuanzia kesho (leo) atakuwa anawapeleka mke na mdogo wake mwenyewe ofisini na chuoni japo kwa kufanya hivi atakuwa anazunguka maana ofisini kwake ni uelekeo mwingine.

Ilinishtua lakini nikaona nisiulize chochote nikamwambia sawa,jamaa akaaga.Nilitafakari na nikataka kujua kwanini jamaa amebadili maamuzi, nikahisi labda jamaa anahisi namtaka mdogo wake?! Sikupata jibu, leo mchana mdogo wake akanitumiasms " mambo, bro amemind wifi kukuzungumzia kila mara.."Nikachoka kabisa, ila nimejifunza kitu unaweza kuhisiwa vibaya bila kufanya ubaya. Tuwe makini na wake za watu.

Note: Sikuwahi kumtamani mke wa jamaa wala mdogo wake.

Jamaa mwenye mke yupo sahihi kabisa hata kama ni mimi ningefanya hivyo.
 
He he he.........kesho napumzika.......leo nilichoka sana nilikuwa namdhamini rais.......halafu Subaru zaidi naitumia summer........

haya bwana si inaandaa system ya kuwa karibu na mjengoni??? Basi ukiwa sawa nistue nama jana nlikuona na subaru yako impreza unasumbua kweli duuh wewe ni noumar zaid ya euro mamy
 
Back
Top Bottom