"ukarimu sifa muhimu sana ndani ya nyumba"

"ukarimu sifa muhimu sana ndani ya nyumba"

Hilo nalo ni tatizo jingine ila mi nafikiri kulisolve angalau mtu unakuwa na juisi ndani ya nyumba au hata chai isikosekane,mgeni akifika angalau mpe chai au juisi ya kupotezea muda huku unapika chakula fasta fasta au kama ndo zenu kununua chipsi mpe juisi au chai ya kianzio afu hao mbebane wote baani kula hivyo vyepe vyenu ila angalau awe amejisikia kapokelewa vizuri na kujaliwa kama mgeni.
sasa kizazi kipya wao ni materialistic life!! Nyumbani hawapiki chakula, zaidi ya kuagiza chips/kuku pale kona....
Na mgeni wa karibu yupo mda mrefu kwenye sofa...!! Sijui vipi wenye nyumba wanatizamanajee?
 
Lakini hapa tena mwanmke kwa nini uone uvivu kupika ulipoolewa ulidhani utakaa wewe na mumeo peke yenu?huyo mumeo ulipanga atakuwa anakula baani tu wakati we upo unafanya nini?nadhani wanawake wanapaswa kuwa makini katika hili,mwanamke ni kupika jamani,hata kama ulikuwa mvivu kwenu jitahidi ukiolewa na kuwa na nyumba yako uvivu huo uweke pembeni kwani utaonekana si mkarimu hata kama ni mkarim,kwani kweli wapo ambao ni wakarimu ila wavivu wa kupika,asante kwa kunikumbushia hili Afro-Arabica
Sasa kizazi kipya wao ni materialistic life!! Nyumbani hawapiki chakula, zaidi ya kuagiza chips/kuku pale kona....
Na mgeni wa karibu yupo mda mrefu kwenye sofa...!! Sijui vipi Wenye nyumba wanatizamanajee?
 
Last edited by a moderator:
mkuu Jerrymsigwa ukarimu niliouongelea hapa ni ule wa ukaribishaji wageni,yaani wageni wafikapo kwako je wako huru au ndo wanajuta kufika kwako wakiwaza sijui tutakuwa tunashiba au ndo kulala na njaa?unawathamini?unawafanya wajisikie vizuri au wawe wa kujishukushuku?hii hasa ni kwa nchi zetu za kiafrika ambako tumezoea sana ukarimu hata kwa mgeni wa ghafla,tofauti na wenzetu ambao wao wanaishi kulingana na taarifa ya ujio wa mgeni,lakini hata kama tukija kufikia huko je bado utamfanya mgeni awe huru au bado utakuwa unamchunguza ulaji wake na mengineyo mengi yasiyoonesha uakrimu?nadhani hapo umeelewa au siyo mkuu?
Ukarimu ni tabia ama ni kitu gani? Sio mtu ukijuskia tuu kwa mda fulani kwani lazima kila siku kuwa hivyo?

Dah mi naona sielewi kbs, nawaza tu kuwa ukarimu ni kuwaje? Hivi hata nje ya Tanzania hiyo kitu ipo? Au kila mtu anaishi kwa apatacho? Pls anaeweza nielekeza
 
Last edited by a moderator:
nayo haipendezi..kwanza ni aibu sana ati alafu kwenye jamii yetu hii hata mwanaume akiwa mchoyo lawama mara nyingi zinaelekezwa mke,mwanamke ndo atabeba lawama za dhambi ya uchoyo wa mumewe bana...
ni nadra kusikia 'Baba Juma mchoyo' ila 'mama Juma' mchoyo utasikia sana
kwenye suala la ukarimu ni rahisi kwa mke kuziba mapungufu ya mume kuliko mume kuziba mapungufu ya mke asee
kweli mwallu ila inahitaji mwanamke jasiri sio kidogo kupambana na hiyo tabia chafu ya mumewe kwani kumbuka kuwa mwanaume ni kichwa cha familia kwa hiyo wengi huweza kutumia mamlaka yao isivyo,so mwanmke asipokuwa imara ni kazi ngumu kweli.
 
Last edited by a moderator:
Hakika ndugu umegusa palepale kunako...nimeishi katika familia zenye watu wa tabia hizi ( mume mkarimu, mke balaaa). Chakula na makazi Kwa wanandugu na hasa upande wa ndugu wa mume Ni chukizo kwa wanawake wengi hasa wa mjini hapa DSM. Kitu cha kuzingatia tu Ni kuwa wengi wa wadada tunaowaoa hapa mjini wameishi maisha ya kibepari zaidi, wengi wao Hata hawawatambui ndugu zao na Hata hawaishi ama hawakuwahi kuishi na ndugu, jamaa Hata marafiki toka wakue. Hivyo, anapoolewa na sie wa kutoka SIKIMBI ambao katika familia kuishi na ndugu, jamaa na marafiki Ni jambo la kawaida, inakua mtihani mkubwa sana sana kwa wake zetu hawa.

Mbali na Hilo Ni kuwa kuna wadada (wake zetu) wanahulka za uchoyo na ubinafsi. Kwao ndugu na mtu anayestahili kula vizuri na kupewa mahitaji yote kama mwanafamilia Ni Yule wa upande wa MKE (huyu atakula, kunywa, kupewa fedha na Hata kusomeshwa Kwa gharama yoyote na kuthaminiwa sana tofauti na ndugu wa MUME ambaye kwake kupewa Hata 5000 na kaka yake, ama baba mdogo/mkubwa, mjomba Ni kero Kwa mke).

Hili linatokea na limejichimbia mizizi sana Kwa jamii nyingi za mjini na HASA hapa DSM Kwa wala NUSU na ROBO. Kuna baadhi ya makabila pia yanahusishwa sana na hizi tabia hasa WACHAGA, WAHAYA ambao inasemekana (na baadhi tumeshuhudia Kwa kuwa tumeishi katika sakata hili) binti akishaolewa basi kama ana mdogo wake ama Hata dada/kaka yake mkubwa au ndugu yeyote ambaye yupo nyumbani na anahitaji kusaidiwa basi anapoolewa tu Yule ndugu yake atakabidhiwa ahakikishe shemeji mtu anasaidia kufikia malengo fulani (hasa kama ndo una mihela yako). Huyu mdogo mtu akishafika basi atataka ndiye awe na usemi na kauli juu ya mambo ya familia hasa inapohusisha ndugu wa pande mbili (ndugu wa mume na ndugu wa mke) Kwa kigezo tu dada Yao ndiye ana mamlaka juu ya Mali.

Hii Ni tabia chafu sana maana imekuwa Ni chanzo cha kuharibika Kwa mahusiano mazuri baina ya ndugu wa pande mbili. Na mbaya zaidi Ni pale ambapo mume unakuwa na mahusiano mazuri tu na ndugu zako (ambao Hata unapokuwa katika uchumba na mchumba wako atakuwa anawafahamu na tena akiwa Ni rafiki Yao mkubwa na wakati fulani akikushauri juu ya nini uwafanyie ndugu zako kimaisha na ki elimu pia) lakini baada tu ya kufunga pingu za maisha (ambazo Kwa karne na kizazi hiki naamini Ni za makubaliano ya kuishi kadri mtakavyoweza na Kwa muda mtakaoweza) mahusiano yanaingia nyongo, masimango, masengenyo, matusi, uchoyo na Hata kusingiziwa mambo (e.g. Wadogo zako hawaniheshimu, mara wananitongoza Mimi, Mara wameiba, etc) vinaibuliwa na kupelekea kuharibika Kwa mahusiano ya wanandugu.

Kwa hakika, Ni tabia zisizopendeza na ikumbukwe kwamba mnapokubali kuoana basi manunganisha familia mbili katika uhusiano wa kindugu na kidamu. Hima wanawake tunaowaoa muone umuhimu wa kuthamini ndugu zetu maana pasi wao msingetuona hivi mnavyotuona sasa. Kama unamnyima chakula hadi BABA/MAMA yangu mzazi na wadogo/wakubwa zangu, je, Mimi Ni nani pasi wao? Hao watoto tutakaowazaa ndugu zao Ni kina nani? Nikisema twende nyumbani likizo, tutafikia Kwa akina nani na kutembelea akina nani? Mbona mwatufanya tuwe na wakati mgumu turudipo nyumbani/vijijini kwetu? Tuziweke wapi sura zetu mbele ya ndugu, jamaa na marafiki zetu Kwa matendo yenu maovu juu Yao?

Ni mengi sana ya kuandika, lakini Kwa THREAD hii Ni dhahiri kuwa tatizo hili Ni kubwa sana na kama lisipoangaliwa na HASA kina dada, basi TALAKA hazitaacha kuwaandama hapa mjini. Kama mume nahitaji kuwa na mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki. Ninachokitafuta natafuta Kwa ajili ya familia yangu (ambayo ndiyo ya kwanza), ndugu zangu (wazazi, wadogo/wakubwa zangu, ndugu wa karibu), jamaa na marafiki. Siwezi kuishi Mimi kama Mimi na mke na watoto wangu. Siku hazilingani, Leo na kesho nikitoweka duniani, watoto wangu wataishi katika Hali gani (japo si guarantee kwamba ukisaidia basi utegemee nao wakusaidie)?

Hima hima kina dada muache tabia hizi na mjapo katika familia ya watu fulani, jaribuni kuziimarisha zaidi ya kuzisambaratisha. Tunaishi Africa, Tanzania kwenye ujamaa na si ULAYA kwenye ubepari na UBINAFSI (umimi).

KUDOS Kwa muanzisha mada.
 
mkuu Jerrymsigwa ukarimu niliouongelea hapa ni ule wa ukaribishaji wageni,yaani wageni wafikapo kwako je wako huru au ndo wanajuta kufika kwako wakiwaza sijui tutakuwa tunashiba au ndo kulala na njaa?unawathamini?unawafanya wajisikie vizuri au wawe wa kujishukushuku?hii hasa ni kwa nchi zetu za kiafrika ambako tumezoea sana ukarimu hata kwa mgeni wa ghafla,tofauti na wenzetu ambao wao wanaishi kulingana na taarifa ya ujio wa mgeni,lakini hata kama tukija kufikia huko je bado utamfanya mgeni awe huru au bado utakuwa unamchunguza ulaji wake na mengineyo mengi yasiyoonesha uakrimu?nadhani hapo umeelewa au siyo mkuu?

Ok asante, kumbe ni specific kwa kitanzania!! Ukarimu mwingine ni kwa sababu mtu masikini, akiwaza kutoa kesho aishi vip! Kwa hilo nawakubali wazungu, hata mtoto ukishafika umri wa kujitegemea u must pay back hela walizokutunzia...kuna mmoja kamaliza deni hadi akaweka sherehe.

Sisi umasikini na unafiki ndio unatusumbua, hatuko straight mpk mtu aweza ona ni mchoyo. Sema bwana karibu ila mm nina hali mbaya so leo no food...kueleweka hapo sasa oooh ngumu sana
 
Last edited by a moderator:
Lakini hapa tena mwanmke kwa nini uone uvivu kupika ulipoolewa ulidhani utakaa wewe na mumeo peke yenu?huyo mumeo ulipanga atakuwa anakula baani tu wakati we upo unafanya nini?nadhani wanawake wanapaswa kuwa makini katika hili,mwanamke ni kupika jamani,hata kama ulikuwa mvivu kwenu jitahidi ukiolewa na kuwa na nyumba yako uvivu huo uweke pembeni kwani utaonekana si mkarimu hata kama ni mkarim,kwani kweli wapo ambao ni wakarimu ila wavivu wa kupika,asante kwa kunikumbushia hili Afro-Arabica
The Man (Mbaba) ni watu waajabu ukishampikia na kumhangaikia the whole day... eti anakuja Mama fulaniee umepika nini leo? halafu anasema Khaa.. kila siku walimchuzi tuu!! au kila siku matokemuhogo au kila siku sangara!! hujifanya kakinai au kujiondokea Uongo mtupu huenda zake nyamachoma baa au mama ntilie!!hizo zao Lakini waMama wapo na ukarimuwa mapishi lukuki.. ila wanataka maneno mazuri na kushajiishwa na appreciations!!
 
ni kweli uyasemayo ila si unajua tena jamani nyuso zetu zimeumbwa na haya afu ukichanganaya na utamaduni wa toka enzi zile za mababu,afu kumwambia mtu uso kwa uso sio rahisi ndg yangu ndo maana mwingine anaweza hata kwenda kukopa tu kwa ajili ya mgeni wakati mwingineutaratibu huo wa ktoa taarifa mapema ni mzuri ila ndo hivyo tena hatujazoea hivyo.
Ok asante, kumbe ni specific kwa kitanzania!! Ukarimu mwingine ni kwa sababu mtu masikini, akiwaza kutoa kesho aishi vip! Kwa hilo nawakubali wazungu, hata mtoto ukishafika umri wa kujitegemea u must pay back hela walizokutunzia...kuna mmoja kamaliza deni hadi akaweka sherehe.

Sisi umasikini na unafiki ndio unatusumbua, hatuko straight mpk mtu aweza ona ni mchoyo. Sema bwana karibu ila mm nina hali mbaya so leo no food...kueleweka hapo sasa oooh ngumu sana
 
The Man (Mbaba) ni watu waajabu ukishampikia na kumhangaikia the whole day... eti anakuja Mama fulaniee umepika nini leo? halafu anasema Khaa.. kila siku walimchuzi tuu!! au kila siku matokemuhogo au kila siku sangara!! hujifanya kakinai au kujiondokea Uongo mtupu huenda zake nyamachoma baa au mama ntilie!!hizo zao Lakini waMama wapo na ukarimuwa mapishi lukuki.. ila wanataka maneno mazuri na kushajiishwa na appreciations!!
neno hilo nalo ndg yangu eti itabidi siku moja hilo nalo tulianzishie thresd wanaume kuwathamini wake zao.
 
ni kweli uyasemayo ila si unajua tena jamani nyuso zetu zimeumbwa na haya afu ukichanganaya na utamaduni wa toka enzi zile za mababu,afu kumwambia mtu uso kwa uso sio rahisi ndg yangu ndo maana mwingine anaweza hata kwenda kukopa tu kwa ajili ya mgeni wakati mwingineutaratibu huo wa ktoa taarifa mapema ni mzuri ila ndo hivyo tena hatujazoea hivyo.
Jerrymsigwa

Ndugu Blue G.. kweli nahakikisha wewe ni Karimu na umetoka kwenye ukoo wenye Ukarimu mkubwa sana.....
Nakupongeza kwa ukarimu kwani bado unaamini ukarimu upo miongoni mwetu.
Mungu akuzidishie ukarimu kwakuwa Mungu ni mwingi wa karam !!
God bless you.
 
mmh! kusema kweli katika hali ya kawaida, imezoeleka mwanamke kuwa mchoyo/ ana roho mbaya... kwahiyo hali ya mwanamke kukosa ukarimu haishtui sana ingawa ni aibu kweli, yaani inatia aibu saaana! na kwa upande wa wanaume, inakuwa mbaya zaidi maana si hali tuliyozoea kuiona katika jamii zetu kwahiyo hilo la mwamume kukosa ukarimu/kuwa mchoyo linashangaza zaidi na huleta hata fedheha kwa mke wake ktk familia hata asipoambiwa........
 
Mwanamke kutokua mkarimu ni aibu la mume duuuuh hatari.
 
Hili lilinikuta nilifika katika familia moja(mjomba) kwa kuwa nilikua na shughuli maeneo hayo akashaur nifikie kwake...nilipofika mjomba akaomba nipelekwe chumba cha wagen...mkewe akatoka uko alikotoka..ufunguo hauonekan akalale tu kwa hausgel..halikua tatizo
mjomba akajaribu kufunika tabia ya mkewe akamwambia anipe soda..mkewe..soda imebak kidogo nlikuwekea wew mgen atakunywa kesho.....,na mengine meng..yule mwanamke alikosa sana ukarim katika nyumba japo mumewe anamsaidia lakin mpaka leo ndugu wa mjomba hawapend kufika pale...
Kukosa ukarimu katika nyumba pia kunaweza kuchangia kuharibu mahusiano mazur na ndug wa karibu....
 
hahahaha umeniacha hoi hapo namba mbili dume linavyopiga misele mpaka jikoni na kusema angalia huu ndio mchele wa mwisho,aisee Duniani kuna vimeo ile mbaya mtu anamaindi hata msosi hii ni hatari kwei kwei.
Ila na sisi tusiende kuwatembelea watu kwa mahesabu kwamba tutamanga sana kwenye hiyo nyumba.
Nalog off
 
au mpo mezani mnakula....kila tonge analitolea maneno.......lakini baba huyu ukimkuta bar anavyotoa ofa za nyama.....mwe...

Niliwahi kupewa lifti ya kama km 15, bibi ndo aliniomba niwajoin. kumbe bwana hakutaka nipande ili wapite njia ya shortcut. bibi akatoa amri lazima wanichukue wapite njia ndefu. njiani tulikutana na bonge la foleni basi bwana alilalamika njia nzima mpaka nikataman kushuka ila nikamuonea aibu bibie
 
Back
Top Bottom