"ukarimu sifa muhimu sana ndani ya nyumba"

Blue G

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Posts
5,339
Reaction score
3,674
Wakubwa zangu shikamooni wadogo zangu marahabani na wa rika langu habari zenu,

Jamani kuna hili swala nimeliona kutoka pande mbili na familia mbili tofauti,nalo limenifanya nifikirie mengi nakujiuliza mengi nami nikaona si vibaya ikiwa nitaliwasilisha hapa jukwaani tulidadavue sote kwa pamoja.

Jamani "UKARIMU" ndani ya nyumba yeyote ile ni muhimu sana kuwepo lakini kuna nyutu mbalimbali ndani ya nyumba yaani utu wa mume na utu wa mke.kuna baadhi ya nyumba mke ni mkarimu sana,nyingine mume ni mkarimu sana na nyingine wote ni wakarimu sana na nyinigne wote hawana ukarimu au wote wana ukarimu wa kiasi.

Concern yangu inkuja hapa kutoka kwenye hizi scene mbili:

1.Baba ni mkarimu sana ndani ya nyuma lakini mama ni kimeo na majanga yaani kama ni chakula au kuwapa watu vitu roho inamtoka anaumia hapendi anatamani kila kitu kibakie kwao,mume asipokuwepo ni majanga matupu wageni wafikapo,kwani kula na kupewa huduma nyingine kama mgeni ni kitu haba lakini baba akiwepo hali inakuwa shwari kwani baba anamjua mkewe vilivyo kwa hiyo anatumia mamlaka yake kusema hii imezidi pika chakula cha kutosha wageni wale wasaze,lakini mwanamke mkosa ukarimu atawaangalia wageni mezani anavyokula mpaka,kiasi cha chakula anachochukua kiasi kwamba kama mgeni ni mjali mabo madogo madogo anaweza ale asishibe.Kwenye nyumba hiyo watu wataondoka hapo wakisema jamani mume wa ile nyumba mkarimu kweli ila mke sasa ni kichomi omba ukitoka safari umkute mwanaume na sio mwanamke utajuta.

2.Mama ni mkarimu sana kiasi kwamba wageni wakifika wanajiona wamefika nyumbani kwani watapa ta huduma zote kama wageni,watakula maji ya kuoga watapewa na watapumzika kwa amani ila kimbambe kinakuja pale ambapo mume ataingia baada ya kutoka kazini hapo mambo yote yanaharibika kwani wageni wataanza kuangaliwa kwa jicho la umakini wa hali ya juu kujua anakulaje,anakula sana au kidogo,kama mama yuko jikon anapika basi mzee wa nyumba ruti hazikatiki,kwenda kuangalia mama anapika kiasi gani,utakuta anaenda jikoni mama nanilihiii angalia nyama hizo unajua kwenye friji zimesiha usiwe unaangalia leo tu.........au mama fulani unajua huo ndo mchele wa mwisho angalia kipimo chako.......yaaani mbaba mzima full majanga yaani kufuatilia fuatila mambo ya misosi ptuuuuuuuu aibu hadi wageni wanshtukia ruti zisizoisha za kwenda jikoni mwanaume mzima unatafuta nini huko badala ukae na wageni mbadilishane mawili matatu,kwa wasoma nyakati watajua tu nini kinaendelea,watajua mume vitu vinamuuma kwa hiyo anenda kucheki,ila kwa wasiojua watadhani labda ni maepenzi mume anenda kumsaidia mamsapu na cooking.

Mimi kwa hapa na hili suala la ukarimu maoni yangu ni haya kwako mwanamke ni aibu sana kukosa ukarimu ndani ya nyumba kwani nyumba ni mwanamke,nawe mwanamke ukiwa makarimu na una hekima hata ikiwa mume si mkarimu waweza okoa janga kwa kuziba uchoyo wa mumeo kwa hiyo wanwake mjitahidi kwa hili.

Kwa wanaume ,wewe mwanaume narudia tena wewe mwanaume ni aibu sana tena sana kuwa mchoyo vitu vinakuuma kama vile utazikwa navyo,aibu kubwa mno sikuzote mwanaume anapaswa kuwa dismainder anayejali mambo ya maana na sio chakula kinakutoa roho ptuuuuuu ni kinyaa kwa mwanaume jamani,mwanume fuatilia mambo ya maana na mazito sio chakula kinataka kukutoa roho,mwachie mama apange mambo ya jikoni wewe kaa pembeni labda kama wampenda sana na wataka kumsaidia na sio kwenda kumpimia michele unga na kumhesabia nyama.

Hayo ni maoni yangu wana MMU karibuni na nyie pia mtoe maoni yenu na hapa pia ningependa kujua ni upande upi unaotia aibu zaidi kwa kukosa ukarimu?upande wa mume au mke ndani ya nyumba?

KARIBUNI.
 
ni kweli Lizzy inatia aibu kwa pande zote ila em tua kidogo na ufikirie kwa upande wa mwanaume,unajua imezoeleka wanaume ni watu wasiojali mambo madogo madogo kama hayo lakini unakuta ye ndo kwenye chakula roho inamhama hatuliiiii????????em piga picha yuko anahaha kila dk mbili jikoni kisa chakula how do you see it????????
Hahahahaha. . .Kaaazi kweli kweli.
Hamna unafuu kwa mwanamke/mwanaume kuwa mchoyo au mroho kwenye maswala ya chakula ila huyo mbaba ni kiboko.
 
Last edited by a moderator:
yaani nimeguswa na hapa bestito nicopy na kupaste:

2.Mama ni mkarimu sana kiasi kwamba wageni wakifika wanajiona wamefika nyumbani kwani watapa ta huduma zote kama wageni,watakula maji ya kuoga watapewa na watapumzika kwa amani ila kimbambe kinakuja pale ambapo mume ataingia baada ya kutoka kazini hapo mambo yote yanaharibika kwani wageni wataanza kuangaliwa kwa jicho la umakini wa hali ya juu kujua anakulaje,anakula sana au kidogo,kama mama yuko jikon anapika basi mzee wa nyumba ruti hazikatiki,kwenda kuangalia mama anapika kiasi gani,utakuta anaenda jikoni mama nanilihiii angalia nyama hizo unajua kwenye friji zimesiha usiwe unaangalia leo tu.........au mama fulani unajua huo ndo mchele wa mwisho angalia kipimo chako.......yaaani mbaba mzima full majanga yaani kufuatilia fuatila mambo ya misosi ptuuuuuuuu aibu hadi wageni wanshtukia ruti zisizoisha za kwenda jikoni mwanaume mzima unatafuta nini huko badala ukae na wageni mbadilishane mawili matatu,kwa wasoma nyakati watajua tu nini kinaendelea,watajua mume vitu vinamuuma kwa hiyo anenda kucheki,ila kwa wasiojua watadhani labda ni maepenzi mume anenda kumsaidia mamsapu na cooking.
 
ni kweli Lizzy inatia aibu kwa pande zote ila em tua kidogo na ufikirie kwa upande wa mwanaume,unajua imezoeleka wanaume ni watu wasiojali mambo madogo madogo kama hayo lakini unakuta ye ndo kwenye chakula roho inamhama hatuliiiii????????em piga picha yuko anahaha kila dk mbili jikoni kisa chakula how do you see it????????
au mpo mezani mnakula....kila tonge analitolea maneno.......lakini baba huyu ukimkuta bar anavyotoa ofa za nyama.....mwe...
 
Last edited by a moderator:
haaaaaaaaaaahaaaaaaaaahaaaaaaaaa em niambie ndugu yangu si aibu hiyo!!!!!!!!!!mwanaume mzima badala ufikirie labda wageni hawa watahitaji nauli ya kurudia nianze kuwaweka kwenye mahesabu,we mgeni akichukua kijiko jicho lina yeye akikipandisha lina yeye akiweka kijiko mdomoni unaye,,,,ptuuuu si ainu hii jamani!!!!!!kwa wote haipendezi ila nahisi kama kwa wababa inachefua zaidi,kwani a man was created to despise small samll things like food.
yaani nimeguswa na hapa bestito nicopy na kupaste:

2.Mama ni mkarimu sana kiasi kwamba wageni wakifika wanajiona wamefika nyumbani kwani watapa ta huduma zote kama wageni,watakula maji ya kuoga watapewa na watapumzika kwa amani ila kimbambe kinakuja pale ambapo mume ataingia baada ya kutoka kazini hapo mambo yote yanaharibika kwani wageni wataanza kuangaliwa kwa jicho la umakini wa hali ya juu kujua anakulaje,anakula sana au kidogo,kama mama yuko jikon anapika basi mzee wa nyumba ruti hazikatiki,kwenda kuangalia mama anapika kiasi gani,utakuta anaenda jikoni mama nanilihiii angalia nyama hizo unajua kwenye friji zimesiha usiwe unaangalia leo tu.........au mama fulani unajua huo ndo mchele wa mwisho angalia kipimo chako.......yaaani mbaba mzima full majanga yaani kufuatilia fuatila mambo ya misosi ptuuuuuuuu aibu hadi wageni wanshtukia ruti zisizoisha za kwenda jikoni mwanaume mzima unatafuta nini huko badala ukae na wageni mbadilishane mawili matatu,kwa wasoma nyakati watajua tu nini kinaendelea,watajua mume vitu vinamuuma kwa hiyo anenda kucheki,ila kwa wasiojua watadhani labda ni maepenzi mume anenda kumsaidia mamsapu na cooking.
 
majanga tena sio kidogo,ni makubwa familia za hivivwanawake huwa wanajitahidi sana kufunika mapungufu ya waume zao kwa wao kujitahidi sana kuwa wakarimu hasa wasipokuwepo,ila wakiwepo tu huwa hawawezi kujizuia na hapo ndipo anapoharibu mpaka wageni kumjua.
kuna wanaume wanatia aibu.....ukiwa na mme wa aina hiyo ni majanga.....
 
majanga tena sio kidogo,ni makubwa familia za hivivwanawake huwa wanajitahidi sana kufunika mapungufu ya waume zao kwa wao kujitahidi sana kuwa wakarimu hasa wasipokuwepo,ila wakiwepo tu huwa hawawezi kujizuia na hapo ndipo anapoharibu mpaka wageni kumjua.

mpaka inafikia hatua ndugu wakitaka kuja kukutembelea ....wanauliza kwanza kama mmeo yupo...
 
hebu fikiria mdogo wangu si aibu hiyo jamani mwanaume??????hapana kwa wote ni tabia mbaya ila kwa mwanaume inatia aibu zaidi.
mpaka inafikia hatua ndugu wakitaka kuja kukutembelea ....wanauliza kwanza kama mmeo yupo...
 
Siku zote nyumba ni mwanamke mwanamke akiwa na roho mbaya ndg, pamoja nawageni au majirani mtajuta kumfahamu au kuifahamu hiyo familia, inakuwa maradufu kuliko baba kuwa na roho mbaya.

Baba muda mwingi hayupo nyumbani hata akiwa na roho mbaya c tatizo sana ila mwanamkeee!!
 
ni kweli habari ya hapa ila aibu zaidi ni kwa mwanaume kwani anatakiwa awe anajali mambo ya maana na si mambo madogo madogo kama hayo.
Siku zote nyumba ni mwanamke mwanamke akiwa na roho mbaya ndg, pamoja nawageni au majirani mtajuta kumfahamu au kuifahamu hiyo familia, inakuwa maradufu kuliko baba kuwa na roho mbaya.

Baba muda mwingi hayupo nyumbani hata akiwa na roho mbaya c tatizo sana ila mwanamkeee!!
 
Last edited by a moderator:
ni kweli uyasemayo mwallu ni afadahli mke awe mkarimu zaidi kwani,yeye ndio nyumba lakini em niambie hata kwa upande wako unamuonaje mume mchoyo hapendi ukarimu chakula kinamuuma weeee mpaka basi?
wakati mwingine huwa naona bora mume mwenye roho mbaya kuliko mke awe na roho mbaya
ni balaaa,wageni mtawasikia tu kufika kwenu nehi
 
Last edited by a moderator:
nayo haipendezi..kwanza ni aibu sana ati alafu kwenye jamii yetu hii hata mwanaume akiwa mchoyo lawama mara nyingi zinaelekezwa mke,mwanamke ndo atabeba lawama za dhambi ya uchoyo wa mumewe bana...
ni nadra kusikia 'Baba Juma mchoyo' ila 'mama Juma' mchoyo utasikia sana
kwenye suala la ukarimu ni rahisi kwa mke kuziba mapungufu ya mume kuliko mume kuziba mapungufu ya mke asee
ni kweli uyasemayo mwallu ni afadahli mke awe mkarimu zaidi kwani,yeye ndio nyumba lakini em niambie hata kwa upande wako unamuonaje mume mchoyo hapendi ukarimu chakula kinamuuma weeee mpaka basi?
 
Sasa kizazi kipya wao ni materialistic life!! Nyumbani hawapiki chakula, zaidi ya kuagiza chips/kuku pale kona....
Na mgeni wa karibu yupo mda mrefu kwenye sofa...!! Sijui vipi Wenye nyumba wanatizamanajee?
 
Ukarimu ni tabia ama ni kitu gani? Sio mtu ukijuskia tuu kwa mda fulani kwani lazima kila siku kuwa hivyo?

Dah mi naona sielewi kbs, nawaza tu kuwa ukarimu ni kuwaje? Hivi hata nje ya Tanzania hiyo kitu ipo? Au kila mtu anaishi kwa apatacho? Pls anaeweza nielekeza
 
Back
Top Bottom