Ukarabati miundo mbinu, kiini macho cha Uchaguzi mkuu?

Shishye

JF-Expert Member
Feb 26, 2009
269
1
Mabarabara mengi ya jijini yako kwenye matengenezo yasiyo ya lazima wala plani ya kueleweka. Barabara ya Old Bagamoyo inatolewa lami na kukarabatiwa. Barabara hii kero yake kubwa huwa ni ufinyu zaidi kuliko ubora wa lami. Anyway, inapigwa greda kufurahisha watumiaji, je ni mkakati wa dhati au ndio yale 'mambo yetu' yamekaribia?
 
Hata sielewi...hii barabara ilitakiwa upanuzi kuwa njia nne toka pale Morroco mpaka Lugalo Junction na New Bagamoyo road...just under 5kms....siku hizi jioni ni balaa....sasa kama inatiwa lami mpya kwa single lane then upanuzi ni mpaka lami hiyo ichakae...15 years!
 
Mimi nilisikia hiyo barabara itaanza kutengezwa ili iwe njia nne mwezi nov.na hizo njia nne zitaanzia moroko mpaka njia panda wazo.mmh sasa sijui ndio ujenzi umeanza au?
 
Mtukwao,
Hiyo ni New Bagamoyo inayopitia mwenge,lugalo mbezi beach...old Bagamoyo inapita kule kwa mwalimu,mwinyi,kawe etc...ndio inakwanguliwa....new bagamoyo ina hadithi nyingi sana...
 
Mabarabara mengi ya jijini yako kwenye matengenezo yasiyo ya lazima wala plani ya kueleweka. Barabara ya Old Bagamoyo inatolewa lami na kukarabatiwa. Barabara hii kero yake kubwa huwa ni ufinyu zaidi kuliko ubora wa lami. Anyway, inapigwa greda kufurahisha watumiaji, je ni mkakati wa dhati au ndio yale 'mambo yetu' yamekaribia?

Wizi mtupu! Na bado watu watawachagua wale wale! Walichosema Msekwa na Malecela kwamba wabunge wengi wa CCM wataanguka majimboni mwao SI KWELI! CCM itaendela kutawala, kwani Wadanganyika wenyewe wameamua KUDANGANYI-KA!

./Mwana wa Haki
 
Back
Top Bottom