Ukanda wa pwani na radi

WILSON MWIJAGE

JF-Expert Member
May 30, 2011
276
76
Ndugu zangu,

Mimi nimezaliwa na kukulia kanda ya ziwa (Bukoba) ambapo RADI wakati wa mvua hata kama ni mvua wenyewe ni kidogo radi ni lazima. Nilipokuja Dar es salaam mwaka 1996 sikuwahi kusikia wala kuona radi wakati au kabla ya mvua kunyesha. Pamoja na kuuliza kwa watu wengi, hakuna mwenye jibu la uhakika au linalojitoshereza la kwanini Dar es salaam hapakuwepo na radi kupindi cha nyuma.

Baada ya mvua ya juzi iliyoambatana na radi nilistahajabu na kumuliza mama mmoja ambaye alinipa majibu haya;

Mwanangu ..... "Ukanda huu wa pwani ikiwa ni pamoja na Dar es salaam hauna miinuko, mawe na miamba mingi ndiyo maana hakuna radi" Angalia mikoa yenye miinuko na mawe kwa wingi (Mwanza, Msoma, Kagera, Morogoro, Songea, Mbeya, Iringa n.k) huko ndiko radi zinatokea kwa wingi.

Je mama huyu alikuwa sahihi? au ni sababu zipi za kisayansi zinazosababisha radi itokee sehemu furani na sehemu nyingine isitokee?

Nawakilisha

 
Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba, chaji za umeme tuli (electrostatic charges) huwa zinajikusanya zaidi kwenye miinuko na milima. Umeme tuli ndio unaohusika na mchakato mzima wa radi. Zinapokuwa kwenye miinuko zinakuwa jirani zaidi na chaji za kwenye mawingu tayari kwa ajili ya kupiga shoti, ndipo hutokea mwanga(radi). Linganisha na umeme unapogusisha nyaya mbili hasi na chanya. Muungurumo unatokana na spidi kubwa ya kutanuka na kusinyaa kwa chembe ndogondogo kwenye eneo la shoti. Hii ni kwa mujibu wa Fizikia yangu ya sekondari. Karibuni kwa marekebisho.
 
nilipokuwa mdogo radi za vuli nilikuwa nakimbilia uvunguni, siku hizi zimeisha?
 
mara nyingi radi hutyoka katika wingi lijulikanalo kama cumulonimbus type 3. katika classification ya mawingu, haya ndiyo mawingi 'makubwa' kuliko yote na ni mazito sana. Ndioy ambayo husababisha mbua kubwa za ghafla ambazo hunyesha kwa muda mfupi. Mawingi haya hujitengeneza katika hali ya hewa maalum na kwa kuwa sehemu za milima zina athiri kwa namna fulani mfumo wa hewa angani, hivyo ndio mana mara nyingi utayaona mawingu haya yakiwa kwenye sehemu za miinuko na ndio maana radi zinakuwa nyingi sehemu hizo.
 
Back
Top Bottom