Ukakasi wa Uendeshaji Kesi. Mzungu Rogers/Dr Mvungi/Mawazo/Mbwambo

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,333
72,791
Yapo mambo yanaleta ukakasi na kujiuliza kuhusu dhamira yetu ya kuendesha kesi zinazohusiana na mauaji.

Imekuwaje kesi ya rubani mzungu Rogers ndani ya wiki moja imepelelezwa na kuhukumiwa tena kwa tukio lililotokea porini na zipo kesi zingine za mauaji kama ya hao wallotajwa hapo juu na kuna watu waliowaona wauaji bado zinapigwa danadana mpaka kusahaulika.

Jee hiyo ya mzungu yaweza kuwa kumekuwa na shinikizo toka kwa nchi wahisani? Au hizo zingine hazishughulikiwi kwa kasi kwa vile hao hawakuwa "rafiki" na utawala?

Ikoje hii?
 
Hizi ni zama za Hapa Kazi Tu. wakati akiongea na Majaji kwenye Siku ya Mahakama, Rais alishangazwa na kuchelewa kwa kesi ambazo ushahidi upo wazi. Aliagiza kuwa ikiwa ushahidi upo wazi, kesi hizo ziamuliwe haraka.

Kwenye hili tukio la kuuawa kwa huyo Rubani, watuhumiwa wamekamatwa, wamekutwa na silaha na wamekiri kuhusika na mauaji hayo. Hivyo nawapongeza Mahakama kwa kwenda na kasi ya Magufuli
 
Ni mbinu tu mafisiem kutaka kuwaonesha hizo nchi..""marafiki"", kuwa serikali hii inafuata sheria na inatenda Haki kwa waliodhulumiwa(wafiwa)...

Hiyo ni danganya toto tu...

kama kweli wana dhamira ya kuharakisha kesi za mauaji...mbona wapo mahabusu kibao tu wanasota jela na kesi zao znapigwa kalenda ...wala hakuna ushahidi unaoendelea.

Waambie waache double standard.
 
Hizi ni zama za Hapa Kazi Tu. wakati akiongea na Majaji kwenye Siku ya Mahakama, Rais alishangazwa na kuchelewa kwa kesi ambazo ushahidi upo wazi. Aliagiza kuwa ikiwa ushahidi upo wazi, kesi hizo ziamuliwe haraka.

Kwenye hili tukio la kuuawa kwa huyo Rubani, watuhumiwa wamekamatwa, wamekutwa na silaha na wamekiri kuhusika na mauaji hayo. Hivyo nawapongeza Mahakama kwa kwenda na kasi ya Magufuli
Kwani matukio aliyoyabainisha mleta mada hao watuhumiwa hawajakamatwa? Watuhumiwa wamekamatwa lakini hakuna kinachoendelea ukweli unabaki wazi kuwa wanapouawa wapinzani wa CCM hakuna hatia.
 
Yapo mambo yanaleta ukakasi na kujiuliza kuhusu dhamira yetu ya kuendesha kesi zinazohusiana na mauaji.
Imekuwaje kesi ya rubani mzungu Rogers ndani ya wiki moja imepelelezwa na kuhukumiwa tena kwa tukio lililotokea porini na zipo kesi zingine za mauaji kama ya hao wallotajwa hapo juu na kuna watu waliowaona wauaji bado zinapigwa danadana mpaka kusahaulika.
Jee hiyo ya mzungu yaweza kuwa kumekuwa na shinikizo toka kwa nchi wahisani? Au hizo zingine hazishughulikiwi kwa kasi kwa vile hao hawakuwa "rafiki" na utawala?
Ikoje hii?

Na Filikunjombe, It is Possible Ndege yake Ilitunguliwa au Kutegewa, Mnakumbuka Ilifanana sana na Kifo cha George Saitoti, Lakini Tanzania watu wanachukulia vitu kiwepesi, hakuna uchunguzi. Nchi zingine hata Kama Kila wazo linaashiria ilikuwa ni ajali ya kawaida, watachunguza. Kenya Iligunduliwa Saitoti Aliuawa kwa Hujuma za Kisiasa na Ndugu Ojore na Marubani walikuwa ni Colateral Damage. Je Inawezekana Filikunjombe alicheza too close akacross mamistari za joka la makengeza au wengine? Tungejuaje hatuchunguzi anything! Ajali, ajali Zikeni, Bwana ametoa, Bwana ametwaa! Inasikitishaaaaaa!

Deat of Saitoti

Only in Africa, Nakumbuka Miaka ya Tisini, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Nd. Robert Ouko, Aliuawa kwa risasi na Kutupwa Kwenye Msitu wa NgongKisha mwili wake Kuchomwa moto., Ukatolewa Utetezi kuwa Alijua kwa Risasi, Lakini Ilipoonekana Mtu hawezi Kujiua kwa Risasi Kisha Ajiteketeze kwa Moto, au Ajiteketeze kwa Moto ndipo ajipige risasi, Stori ya wauaji Ikaingia Dosari.

Samahani mtoa mada.
Kama watuhumiwa wamekiri kama walihusika,ulitaka hakimu afanyeje??
 
Hizi ni zama za Hapa Kazi Tu. wakati akiongea na Majaji kwenye Siku ya Mahakama, Rais alishangazwa na kuchelewa kwa kesi ambazo ushahidi upo wazi. Aliagiza kuwa ikiwa ushahidi upo wazi, kesi hizo ziamuliwe haraka.

Kwenye hili tukio la kuuawa kwa huyo Rubani, watuhumiwa wamekamatwa, wamekutwa na silaha na wamekiri kuhusika na mauaji hayo. Hivyo nawapongeza Mahakama kwa kwenda na kasi ya Magufuli
Kesi ya mauaji haijatolewa maamuzi yale makandokando ndo yametolewa maamuzi usitafute kiki.
 
Bila kusahau matukio haya
1. Waliolipua mabomu kule Arusha KANISANI Olasity na Mkutano wa CDM Soweto
2. Waliomuua kwa kumchinja mwenyekiti wa CDM Usariver
Waambie Mbowe na Lema wawasilishe mapema ile video inayoonesha walipuaji ili mahakama ihukumu fasta
 
Kwa kweli hukumu ya kesi hii imewahi sana
Hatukatai kuwahi ila tunauliza kwa nini zingine haziwahi ila ya huyu mzungu tuu? Tena iliyotokea porini? Wauaji wa Mawazo walitambuliwa kabisa na wenyeji,vitu vya Dr Mvungi walikamatwa navyo walioshukiwa kunuua na Wauaji wa Mbwambo kule Arumeru walikamatwa lakini eti wakatoroka mikononi mwa polisi mahakamani na askari wahusika wapo tuu na sio ajabu wametunukiwa vyeo.
Haya ndio maajabu kama ya wauaji wa Gen Kombe, kutoka adhabu ya kifo hadi kifungo cha maisha hadi kuwa uraiani.
 
Ni mbinu tu mafisiem kutaka kuwaonesha hizo nchi..""marafiki"", kuwa serikali hii inafuata sheria na inatenda Haki kwa waliodhulumiwa(wafiwa)...

Hiyo ni danganya toto tu...

kama kweli wana dhamira ya kuharakisha kesi za mauaji...mbona wapo mahabusu kibao tu wanasota jela na kesi zao znapigwa kalenda ...wala hakuna ushahidi unaoendelea...

Wambie MAFISI waache double standard....

pumbavu zao
Pole sana ndugu. Wapinzani mtaugua vidonda vya tumbo bure. CCM inadizi kupaa
 
Hatukatai kuwahi ila tunauliza kwa nini zingine haziwahi ila ya huyu mzungu tuu? Tena iliyotokea porini? Wauaji wa Mawazo walitambuliwa kabisa na wenyeji,vitu vya Dr Mvungi walikamatwa navyo walioshukiwa kunuua na Wauaji wa Mbwambo kule Arumeru walikamatwa lakini eti wakatoroka mikononi mwa polisi mahakamani na askari wahusika wapo tuu na sio ajabu wametunukiwa vyeo.
Haya ndio maajabu kama ya wauaji wa Gen Kombe, kutoka adhabu ya kifo hadi kifungo cha maisha hadi kuwa uraiani.
Nimewaambia muwaombe akina Lema na Mbowe wawasilishe zile video za waliolipua Olasit ili wahukumiwe fasta. Mbona mna kigugumizi? Au na nyie mlikuwa mnatafuta kick tu?
 
Yapo mambo yanaleta ukakasi na kujiuliza kuhusu dhamira yetu ya kuendesha kesi zinazohusiana na mauaji.

Imekuwaje kesi ya rubani mzungu Rogers ndani ya wiki moja imepelelezwa na kuhukumiwa tena kwa tukio lililotokea porini na zipo kesi zingine za mauaji kama ya hao wallotajwa hapo juu na kuna watu waliowaona wauaji bado zinapigwa danadana mpaka kusahaulika.

Jee hiyo ya mzungu yaweza kuwa kumekuwa na shinikizo toka kwa nchi wahisani? Au hizo zingine hazishughulikiwi kwa kasi kwa vile hao hawakuwa "rafiki" na utawala?

Ikoje hii?

Chakaza kwani Dr.Mvungi,Mwangosi,Mawazo na wengineo kwani wao ni binadamu???Huyu Mzungu ni Binadamu wa ngazi ya kwanza, pili yake ni Mfadhili wa Tembo na hao wengine kama unadhani ni binadamu wako ngazi ipi???

Waliowaua hao siyo kwamba hawajulikani wanajulikana na wengine waliotoa order ya kuua wamepandishwa vyeo.Jiulize hao ni binadamu na kama ni binadamu yupo grade ya ngapi???

Wale Mazombi huko Zanzibar yanapiga,kuchoma maeneo ya biashara za wengine ilipounguzwa ofisi ya Mazombi serikali yote ilitega sikio ikapiga kelele wahusika watafutwe haraka,je hao wanaobomolewa maeneo yao Serikali haioni au ni binadamu wa grade ipi???

Siku serikali itakapoacha kuturank kwa grade ndipo hapo HAKI itakapokuwa inatendeka.Kwa sasa ni Maruweruwe tu hakuna haki hapo.

Hata hao waliokamatwa sioni sura ya mtungua ndege.Aliyetungua ndege yuko wapi???
 
Hawajui kuwa hizi ni zama za Hapa Kazi Tu
Pamoja na zama lakini serikali no ileile, in mabadiliko kama ya timu ya Moira tuu. Namba 7 akacheze 9,huyo 9 arudi beki 2 Nk Nk. Hivyo kujisafisha ilikuwa muhimu
 
Back
Top Bottom