Washitakiwa wanne mauaji wa Dr. Mvungi waachiwa huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
SERIKALI imewaachilia huru watuhumiwa wanne kati ya saba wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kukusudia ya Dk Sengondo Mvungi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Watuhumiwa walioachiwa huru ni Ahmad Kitabu (30), Zacharia Msese (33), Masunga Makenza (40) na John Mayunga (56).

Pamera Shinyambala, wakili wa serikali amesema kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), hana nia ya kuendelea kuwashtaki watu hao na kwamba amewaondoa katika mashitaka hayo kwa muhibu kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Baada ya taarifa hiyo, Hakimu Thomas Simba ameutaka upande huo kupeleka cheti cha kifo cha mtuhumiwa namba moja ambaye aliripotiwa mahakamani hapo kuwa amefariki. Amesema kuwa kabla ya kufika Mahakama kuu upande huo unatakiwa ufike na cheti hicho ili kuepuka vikwazo.

Watuhumiwa waliobaki katika kesi hiyo ni Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Msungwa Matonya (30) na Longishu Losingo aliyekuwa mlinzi wa Dk Mvungi.

Inadaiwa kuwa, kwa pamoja watu hao walimshambulia kwa mapanga na hatimaye kumsababishia kifo Dk. Mvungi mnamo tarehe 3 Novemba, 2013. Wanadaiwa kufanya kosa hilo la mauaji kinyume cha kifungu cha 196 cha Sheria na Kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
 
Hesabu ni janga la kitaifa, wameachiawa 4 kati 7 lakini ukihesabu wamebaki watano(Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Msungwa Matonya (30) na Longishu Losingo aliyekuwa mlinzi wa Dk Mvungi.)
 
Magazeti ya leo
20161230_044437.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya 10 waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya bila kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi.

Washitakiwa walioachiwa ni Masunga Makenza (40), mkazi wa Tabata Darajani, Zacharia Msese (33), Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala na John Mayunga (56).

Waliachiwa kwa mujibu wa Kifungu Namba 91 Kifungu kidogo cha kwanza cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). Wakili wa Serikali, Pamela Shinyambala alidai mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba kuwa upande wa mashitaka umeshasajili jalada hilo Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mshitaka Nchini (DPP), hakuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao kwa mujibu wa kifungu hicho. Awali, Shinyambala alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa maelezo ya mashahidi baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Hakimu Simba alisema anawaachia washitakiwa hao, kama walivyoomba upande wa mashitaka. Alisema kwamba washitakiwa sita, ndio watakaosomewa maelezo hayo ya mashahidi.

Washitakiwa hao ni Longishu Losingo (29), Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa Vingunguti, Juma Kangungu (29) mkazi wa Vingunguti, Msungwa Matonya (30), mkazi wa Vingunguti na Masenga Mateu.
 
Taifa lilipoteza mtanzania mpenda Nchi
 
Back
Top Bottom