Ukaguzi wa vyeti kwa watumishi wa umma ilikuwa ni danganya toto

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
IDARA YA UTUMISHI UKAGUZI WA VYETI ULIKUWA NI WA MAZINGAOMBWE.

Mimi ni Mtanzania ninayekanyagwa kanyagwa bila sababu yoyote kisa tu Ukweli una uma.

Tulikuwa na ukaguzi wa Vyeti kwa Watumishi wa umma nchi nzima, lengo kuwabaini wanaotumia vyeti vya watu na wenye vyeti vya kufoji na wasio na vyeti kabisa ila wamepata ajira.

Ukaguzi huu ni kama ilikuwa blablaa tu kwani kuna maeneo Rushwa ya Ngono imefanyika na wahusika wameachwa na hawakuwa na vyeti.

Idara hii, pia wale ambao hawakuwa na vyeti wengine waliwahonga Maafisa Utumishi na hivyo majina yao yalipita blablaa na kurejeshwa kazini nyuma ya pazia. Kwa kifupi hakuna waliotolewa.

Mchezo huu wa propaganda ni kuidharirisha nchi kwa kufanya maigizo kwenye mambo ya msingi. Maswala nyeti kama haya halafu mnatufanyia maigizo yaani bora msingekagua kabisa.

Watu makini wanashangaa, mbona watu Fulani hawana vyeti na hata kwenye ukaguzi walikimbia, mbona wamerejea tena. Je wameprintiwa vyeti vipya kama ilivyo ada.

Nawasilisha:

Deogratius Nalimi Kisandu
16 Jan 2017
 
Hebu Taja Baadhi Yao Unaowafahamu Na Taasisi/sehemu Wanazofanya Kazi! Vinginevyo Wewe Ndo Unaleta Blablaa
 
IMG_20161212_142200.jpg

Nami nikiwa huko Ngorongoro crater kuangalia maeneo alipokuwa akiishi Faru John, ofisini kwa watumishi nikakutana na Tangazo hilo....nikajiuliza sana ila sikupata majibu nikaishia kuangalia ofisi zao jinsi nao wanavyowajibika mle ndani.....kuna watu vyeti vyao tangu waanze kazi haviko kwenye mafaili na sijui waliwatambuaje kama wanasifa kupitia vyeti?
 
Kama umekua muwazi mpaka kuandika jina lako,basi kua muwazi kutaja eneo husika na watu husika wanaoendelea na kazi kinyume na taratibu za nchi.wahusika wanapita humu na watalifanyia kazi
 
Tanzania kila kitu kinawezekana..........

Kama watu waliomba rushwa ya ngono kuwapandisha haraka madaraja baadhi ya watumishi Wa umma uko kwenye halimashauri.........

Ije ishindikane hii inawezekana kabisa .........
 
KISANDU, wanasheria wrote wa chama wanaenda kwenye kesi ya Lema nawe unajiweka kati, hakuna wa kukutetea tusilaumiane!
 
Wapi huko mkuu? Nawafahamu walimu wawili na mpaka sasa wanatarajiwa kusomewa mashtaka mahakamani
 
Kisandu umeamua kuwa muwazi,weka ushahidi usio na shaka kuhusiana na haya maneno hapa



"Ukaguzi huu ni kama ilikuwa blablaa tu kwani kuna maeneo Rushwa ya Ngono imefanyika na wahusika wameachwa na hawakuwa na vyeti.

Idara hii, pia wale ambao hawakuwa na vyeti wengine waliwahonga Maafisa Utumishi na hivyo majina yao yalipita blablaa na kurejeshwa kazini nyuma ya pazia. Kwa kifupi hakuna waliotolewa"
 
Kumbe rushwa ya ngono, kutoa uchi ilitembea na watu wasio na sifa walirudishwa makazini, na walikimbia kuhakikiwa vyeti vyao? Utaisadia serikali ni taasisi, wakala, mamlaka au wizara ipi watu wamefanya hivyo, sbb ni kosa kubwa sana kisheria..

Deo, wasaidie UTUMISHI, na utakuwa umetoa mchango mkubwa sana kwa serikali, plse
 
kuna wakati kichaa husema neno lenye ukweli
Iliwahi kutokea tupo msibani, jamaa mmoja akasimama mchafu mchafu hivi na wengi walisema akili zake hazipo sawa alipo pewa nafasi Aliongea point ya msingi alisisitiza watu wapime afya zao mara kwa mara, kila mtu aliyekuwepo pale alibaki akicheka kwa jinsi tulivyokuwa tunamchukulia yule jamaa na maneno aliyoyaongea. Alichokisema Kisandu ni kweli kabisa hakuna mtu aliyefukuzwa kazi kwa kutumia vyeti bandia.
 
Kumbe rushwa ya ngono, kutoa uchi ilitembea na watu wasio na sifa walirudishwa makazini, na walikimbia kuhakikiwa vyeti vyao? Utaisadia serikali ni taasisi, wakala, mamlaka au wizara ipi watu wamefanya hivyo, sbb ni kosa kubwa sana kisheria..

Deo, wasaidie UTUMISHI, na utakuwa umetoa mchango mkubwa sana kwa serikali, plse
Hao utumishi ndio waliendesha zoezi hilo, halafu unataka Kisandu awasaidie nini sasa.
 
Back
Top Bottom