Kwa taarifa yako kwenye sekta binafsi watu hawajali vyeti wanajali uwajibikaji. Nadhani unaona tija katika taasisi binafsi kulinganisha na serekali. Huko kwenye sekta binafsi uwe na cheti usiwe na chetim, kinacholinda ajira yako ni kufikia lengo la muajiri basi.
Waanze na wanaotakiwa kukagua, yaani wakaguaji na mabosi wao kwanza ndo wakaguliwe baada ya hapo ndo wakakague sasa.
Hili ni jambo jema maana tumechoka kuwa na Vihiyo wengi maeneo ya kazi.Hata hivyo nashauri waanze na wakubwa kwanza halafu ndiyo wateremke hadi kwa wadogo.Nashauri hivi kwa sababu kuna jamaa mmoja nadhani anaitwa Kainerugaba Msemakweli ambaye aliwahi kuandika kitabu kilichoelezea Mafisadi wa Elimu Tanzania lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kuthibitisha kama kilichoandikwa ni kweli au uongo.Kwa nyongeza ni kuwa Kihiyo mkubwa ana madhara makubwa zaidi kwa jamii ukilinganisha na Kihiyo mdogo.
Jamani mie cha kwangu cha fm 4 kilipotea katika mazingira ya utata sana na sijui itakuwaje siku nikamkamata anayekitumia kwasababu naamini yupo tu.
upo sahihi wasije tumbua majipu ya wenzao wakat na wenyewe watumbuajia wanayo
Kwenye vyeti tupo mtaani tu hatuna kazi..wangeanza na polisi..
JK alijaribu na alianzia polisi na jeshi nadhani, alichokiona huko nadhani ndio maana lilisitishwa ghafla. Kama kweli ni serious basi masharti ya vibali vya kazikwa wageni inabidi yalegezwe!
Lukuvi hachomoki ....
Mkuu vipi mbona unamkomalia sana huyu Jamaa labda nini kipo nyuma ya pazia?
Tegemeeni watu wengi kupoteza uhai kwa kiharusi. Tena nawashauri wahakiki vyeti vyote kuanzia sekondari yaani form four hadi vyuo. Tunaweza kushangaa asilimia 75 wana vya magumashi.Katika kuhakikisha wafanyakazi wa Serikali ni wale wenye sifa stahiki, Serikali imeanza ukaguzi wa vyeti ili kuhakiki kama ni vyeti ambavyo sio feki.
Baadhi ya mikoa walimu wametakiwa kuwasilisha vyeti vyao kwa uhakiki.
Baada ya walimu wataofuata ni Halmashauri zote nchini kwa kuwa fedha nyingi za maendeleo hupelekwa huko.
Connect Dots fedha za Elimu kupelekwa moja kwa moja kwa wakuu wa shule.
Taasisi binafsi kabala ya cheti unatakiwa upige kaz waione. Unaweza ukawa na chet kaz hujui.
bahati mbaya vyuo vyetu huwa havitunzi kumbukumbu za wahitimu wao,nina ushahidi wa hilo,jaribu kwenda hapo udsm uombe rekodi za mwanafunzi aliemaliza chuo 2005 uone kama watakupa.me binafsi nilimaliza pale 2013,bahati mbaya transcript yangu ililowana na mvua ikaharibka,mwaka huu nimeenda kuomba nyingne,cha ajabu wanasema nlishafutwa kwenye database ya chuo hvyo record zangu hazipo tena,sasa hyo ni udsm tu,bado sijajua hvi vyuo vidogo vinavyochipukia vyenyewe viko vipi.ndo maana nakuambia kwa necta watawakamata ila kwa vyuo vikuu sidhani.