Jana Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kiliketi ambapo pamoja na mambo mengine yote kiliwapokea Wanachama wapya waliojiunga na CCM wakitokea upinzani. Mmoja wao aliyepokelewa alikuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi aliyeamua kuacha vyeo vyote vizito alivyokuwa navyo Chadema na kuamua kujiunga na CCM.
Mara baada ya kujiunga, akaibuka Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi, Edward Lowassa aliyeibuka na mtazamo wa ukabila juu ya Patrobas kujiunga na CCM. Lowassa alisema; “Nikajiuliza hata Patrobas Katambi? Nikagundua ooohh kumbe ni Msukuma … Ndio maana” Mwisho wa kunukuu.
Lowassa aliyasema maneno hayo Jana Jumanne Novemba 21, 2017 akiwa kwenye kampeni Makiba, Meru. Hii haikuwa kauli sahihi kwa Lowassa kuisema mbele ya hadhara tena jukwaani akiwahutubia watu. Huu ni ukabila mkubwa, kwani Wasukuma sio watu? Lowassa anataka kutuambia wanaohamia CCM wote ni Wasukuma? Ina maana Prof. Kitila Mkumbo ni Msukuma? Samson Mwigamba ni Msukuma? Edna Sunga ni Msukuma? Alberto Msando ni Msukuma? Ama wale Madiwani wanaojiuzulu kila siku huko Arusha na sehemu nyinginezo kujiunga na CCM nao pia ni Wasukuma?
Hizi ni dharau na ubaguzi wa hali ya juu ambao Lowassa ameonyesha kwa Wasukuma. Na hii ni tabia yake endelevu ya kupenda kuendekeza ubaguzi. Utakumbuka mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu Lowassa alihutubia akiwa Kanisani na kuwaambia Waumini sasa ni zamu ya Warutheli kuongoza nchi. Hapa Lowassa alikuwa anaomba kura kwa kutumia ushawishi wa ubaguzi wa mwamvuli wa udini, ni kama ambavyo alivyokuja hivi sasa na ubaguzi wa ukabila.
Taratibu naanza kuona misukosuko ambayo atapitia Katibu Mkuu wao Dk. Mashinji ambaye nae ni Msukuma kwa kabila ikiwemo ya kutengwa na kuhisiwa wakati wowote anaweza kujiunga CCM. Hakika, dhambi hii ya ubaguzi haitawaacha salama.
Lowassa huyu huyu alienda kumpigia debe Uhuru Kenyatta kwenye kinyang’anyiro cha Urais nchini Kenya sera zake kubwa zilikuwa ni ukabila na udini kwa Wakikuyu wa Kenya. Lowassa huyu anautaka urais kwa kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ubaguzi wa udini na ukabila ambavyo vimemtawala sana akilini na midomoni mwake jambo ambalo halivumiliki hata kidogo.
Kauli hii ya Lowassa ni hatari inayopaswa kukemewa vikali kwani masuala ya uchochezi wa ubaguzi wa ukabila unaweza kuleta maafa makubwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mathalani, mwaka 1994 kuliibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda kati ya makabila ya Wahutu na Watutsi yaliyosababisha na ubaguzi wa kikabila baina yao kama ambavyo Lowassa anavyoenenda.
Ndugu zangu, amani kuivunja ni kazi rahisi sana kuliko kuijenga tena kwani ni sawa na kuichezea shilingi katikati ya bahari yenye kina kirefu. Wapo wanaosema kuwa amani ni sawa na yai mkononi, ukilivunja hautaweza kuliunganisha kamwe; wengine wanasema kuwa amani haina bei na ikipotea haina soko la kununua. Tuitunze amani yetu kwa kukemea vikali kauli za kibaguzi za kikabila kama hizi zinazotolewa na Lowassa.
Shilatu E. J