Ukabila wa Lowassa hauvumiliki kabisa

Ukabila wa Lowassa hauvumiliki kabisa

Jaji mkuu kanda ya ziwa
Mwanasheria mkuu kanda ya ziwa
Mkuu wa majeshi kanda ya ziwa
Katibu mkuu wizara ya fedha mtoto wa dada
Igp siro msukuma
Mkuu wa majeshi msukuma
Waziri wa nishati mtoto wa mjomba
Wenye hatia wameshika mpini
Wenye haki wameshikishwa makali
Tundu lissu
 
Na utafukiwa au kuliwa na wadudu bila kuzikwa umuache mzee wa watu anadunda hayawani mkubwa! kuna marehemu wenzako walitamka ujinga kama wako waliishasahaulika tayari. Siasa uchwara zisiwaondolee akili kichwani. Kipi kibaya kilichotamkwa na Lowasa kama mlishangilia zuio la kubomoa nyumba Mwanza kwa kigezo cha kura, baada ya kuvunjia wa Kimara pamoja na zuio la mahakama? Acha ujinga!
kwani uongo? Hayo maneno si sawa na marehemu tu?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] nawaza tu hivi tukianza kuendekeza ukanda na ukabila..

naona kuna chama kitaambulia patupu kila uchaguzi.
 
Lowasa na Chadema wasahau kura za kanda ya ziwa .Wasahau kabisa .

Mkuu cdm wataomba kura kwa sera zao nchi nzima, ila kama kanda ya ziwa hawajali sera wanatoa kwa kuangalia kabila hata cdm sidhani kama wanazitaka. Hiyo tabia ya ukabila ni ya ccm na hilo liko wazi. Nyie jizungusheni anzisheni post za kudhani mnawachafua cdm lakini ndio mjue mnaweka uwanja wa kujadili na kuona tatizo la ukabila limeletwa na nani nchi hii. Kumbuka huku kwenye mitandao watu wanafunguka bila hofu wala kuremba. Hiyo kete ya ukabila ccm wameitumia sana nchi hii bila kujali madhara yake, wanachokifanya cdm kwa sasa ni kuweka mambo hadharani.
 
Sijawahi mkubali Lowassa tangu nilipojua anatumia hela kuingia ikulu. Hili ndo linamtafuna zaidi ya yote.
 
Ni nani fukara wa akili anayeamini, kwa mfumo wetu wa maisha ya Kitanzania, nyumba zote za Mwanza zitakazonusurika ni za Wasukuma? Yaani nyumba zote zilizovunjwa Dar ni za Wazaramo?
Na ni nani fukara wa akili anayeamini kwa mfumo wetu wa maisha ya Kitanzania, watu wote walioko Kilimanjaro na Arusha, ni wachaga tu? Wakati mwingine muwe mnajadili hoja kwa kuangalia context nzima, siyo unachota kaneno kamoja unakimbia nacho!
 
Na ni nani fukara wa akili anayeamini kwa mfumo wetu wa maisha ya Kitanzania, watu wote walioko Kilimanjaro na Arusha, ni wachaga tu? Wakati mwingine muwe mnajadili hoja kwa kuangalia context nzima, siyo unachota kaneno kamoja unakimbia nacho!
Context nzima ya kuvunjwa nyumba na maendeleo kwa misingi ya ukabila? au Context ya Vyama kujengwa kwa misingi ya ukabila na udini?
 
Context nzima ya kuvunjwa nyumba na maendeleo kwa misingi ya ukabila? au Context ya Vyama kujengwa kwa misingi ya ukabila na udini?
Context ya wanasiasa wanapozungumzia ukabila. Wewe unafahamu miaka mingi tu CCM waliasisi propaganda kwamba Chadema ni ya Kilimanjaro- ya wachaga, na hawakujali kwamba Kilimanjaro kuna wanyakyusa na wasukuma pia. Kumbe wewe hupaswi pia kushangaa leo inapokuja hoja ya usukuma wa Mwanza, hata kama kuna akina Ambonile huko! it is simple like that!
 
Ukabila Wa magufuli lieteua nusu ya mawaziri wasukuma unavumilika??
Mkuu kabla ya kusema unachosema ungefanya utafiti,ndipo ujenge hoja yako.Nimesoma hoja zako nami nakaamua kujiridhisha na ulichosema nilichogunduwa ni hiki:-
JINA LA WAZIRI MKOA ANAOTOKA
1-Mh Kariuki Kagera
2- MhMakamba Tanga
3-Mh Mwakyembe Mbeya
4-Mh Mwinyi Zanzibar
5-Mh Ndalichako Kigoma
6-Mh Mpango Kigoma
7-Mh Mkuchika Mtwara
8-Mh Mahiga Iringa
9-Mh Lukuvi Iringa
10-Mh Ummy Mwalimu Tanga
11-Mh Mchemba Singida
12-Mh Jafo Pwani
13-Mh Mwijage Kagera
14-Mh Mbawara Zanzibar
15-Mh Dr Kigangwala Tabora
16-Mh Mhagama Ruvuma
17-Mh Mpina Songwe
18-Mh Kabudi Dodoma
19-Mh kalemani Geita
20- Mh Tizeba Shinyanga
21-Mh Kamwelwe Katavi

Hao ndiyo mawaziri wa sasa.Fanya hesabu kwa namna yote unayoona inafaa,kama nusu ya mawaziri wanatoka sehemu moja

Kitu cha kujifunza ni kwamba,chadema wameamua kwa makusudi kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali

ya Rais Magufuliikiwa ni pamoja na propoganda za kuwa mawaziri wengi wanatoka kwake,lakini ukweli ndio huo.

Katika kitu kizuri alichotuachia Rais mstaafu Kikwete,ni Kwamba akili za kuambiwa changanya na........................
 
Sioni ukabila kwa hapo,baraza hili limegusa kila kona ya nchi,naamini mawaziri wote wanawatumikia Watanzania bila kujali maeneo wanayotoka.
 
Kama kweli kauli hii imetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama hiki huko Meru, basi ni wazi kuna hitaji la wakuu hawa kuueleza umma na hasa wanachama wao usahihi wa hii kauli.

Patrobas alikuwa kiongizi Mkuu wa BAVICHA na alikuwa ni moja ya viongozi waandamizi wa chama hicho. Si kwa ajili ya usukuma wake ndio aliingia Chadema, bali ni kijana Msomi wa Tanzania aliyeamini Chama hicho ni chama cha Watanzania wote bila kujali dini,rangi au Kabila.

Leo hii anapotumia haki yake kikatiba na kuamua kuhamia Chama kingine, halafu ghafla anaibuka kiongozi mwandamizi wa Chama alichoondoka na kutoa kauli kama hii ya kibaguzi dhidi ya jamii ingine inatia hofu na shaka juu ya agenda za chama hiki.

Je, Chama hiki hakina wanachama wa kabila hili la Wasukuma? Je, wao watajisikiaje kwa kauli hizi?

Ni vyema tukalaani kwa nguvu zote kauli hizi za kibaguzi. Na kama kuna maelezo yoyote juu ya kuwa ni upotoshaji tupewe maelezo tujue ni uongo.
 
Jana Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kiliketi ambapo pamoja na mambo mengine yote kiliwapokea Wanachama wapya waliojiunga na CCM wakitokea upinzani. Mmoja wao aliyepokelewa alikuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi aliyeamua kuacha vyeo vyote vizito alivyokuwa navyo Chadema na kuamua kujiunga na CCM.

Mara baada ya kujiunga, akaibuka Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi, Edward Lowassa aliyeibuka na mtazamo wa ukabila juu ya Patrobas kujiunga na CCM. Lowassa alisema; “Nikajiuliza hata Patrobas Katambi? Nikagundua ooohh kumbe ni Msukuma … Ndio maana” Mwisho wa kunukuu.

Lowassa aliyasema maneno hayo Jana Jumanne Novemba 21, 2017 akiwa kwenye kampeni Makiba, Meru. Hii haikuwa kauli sahihi kwa Lowassa kuisema mbele ya hadhara tena jukwaani akiwahutubia watu. Huu ni ukabila mkubwa, kwani Wasukuma sio watu? Lowassa anataka kutuambia wanaohamia CCM wote ni Wasukuma? Ina maana Prof. Kitila Mkumbo ni Msukuma? Samson Mwigamba ni Msukuma? Edna Sunga ni Msukuma? Alberto Msando ni Msukuma? Ama wale Madiwani wanaojiuzulu kila siku huko Arusha na sehemu nyinginezo kujiunga na CCM nao pia ni Wasukuma?

Hizi ni dharau na ubaguzi wa hali ya juu ambao Lowassa ameonyesha kwa Wasukuma. Na hii ni tabia yake endelevu ya kupenda kuendekeza ubaguzi. Utakumbuka mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu Lowassa alihutubia akiwa Kanisani na kuwaambia Waumini sasa ni zamu ya Warutheli kuongoza nchi. Hapa Lowassa alikuwa anaomba kura kwa kutumia ushawishi wa ubaguzi wa mwamvuli wa udini, ni kama ambavyo alivyokuja hivi sasa na ubaguzi wa ukabila.

Taratibu naanza kuona misukosuko ambayo atapitia Katibu Mkuu wao Dk. Mashinji ambaye nae ni Msukuma kwa kabila ikiwemo ya kutengwa na kuhisiwa wakati wowote anaweza kujiunga CCM. Hakika, dhambi hii ya ubaguzi haitawaacha salama.

Lowassa huyu huyu alienda kumpigia debe Uhuru Kenyatta kwenye kinyang’anyiro cha Urais nchini Kenya sera zake kubwa zilikuwa ni ukabila na udini kwa Wakikuyu wa Kenya. Lowassa huyu anautaka urais kwa kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ubaguzi wa udini na ukabila ambavyo vimemtawala sana akilini na midomoni mwake jambo ambalo halivumiliki hata kidogo.

Kauli hii ya Lowassa ni hatari inayopaswa kukemewa vikali kwani masuala ya uchochezi wa ubaguzi wa ukabila unaweza kuleta maafa makubwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mathalani, mwaka 1994 kuliibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda kati ya makabila ya Wahutu na Watutsi yaliyosababisha na ubaguzi wa kikabila baina yao kama ambavyo Lowassa anavyoenenda.

Ndugu zangu, amani kuivunja ni kazi rahisi sana kuliko kuijenga tena kwani ni sawa na kuichezea shilingi katikati ya bahari yenye kina kirefu. Wapo wanaosema kuwa amani ni sawa na yai mkononi, ukilivunja hautaweza kuliunganisha kamwe; wengine wanasema kuwa amani haina bei na ikipotea haina soko la kununua. Tuitunze amani yetu kwa kukemea vikali kauli za kibaguzi za kikabila kama hizi zinazotolewa na Lowassa.

Shilatu E. J
Acha aendelee hajui ndio inayo ubomoa chadema watu wameshituka chama cha kasikazini kadri anavyo lopoka ndio jahazi linazidi kuzama kasahau katibu mkuu wake ni msukuma
 
Mkuu kabla ya kusema unachosema ungefanya utafiti,ndipo ujenge hoja yako.Nimesoma hoja zako nami nakaamua kujiridhisha na ulichosema nilichogunduwa ni hiki:-
JINA LA WAZIRI MKOA ANAOTOKA
1-Mh Kariuki Kagera
2- MhMakamba Tanga
3-Mh Mwakyembe Mbeya
4-Mh Mwinyi Zanzibar
5-Mh Ndalichako Kigoma
6-Mh Mpango Kigoma
7-Mh Mkuchika Mtwara
8-Mh Mahiga Iringa
9-Mh Lukuvi Iringa
10-Mh Ummy Mwalimu Tanga
11-Mh Mchemba Singida
12-Mh Jafo Pwani
13-Mh Mwijage Kagera
14-Mh Mbawara Zanzibar
15-Mh Dr Kigangwala Tabora
16-Mh Mhagama Ruvuma
17-Mh Mpina Songwe
18-Mh Kabudi Dodoma
19-Mh kalemani Geita
20- Mh Tizeba Shinyanga
21-Mh Kamwelwe Katavi

Hao ndiyo mawaziri wa sasa.Fanya hesabu kwa namna yote unayoona inafaa,kama nusu ya mawaziri wanatoka sehemu moja

Kitu cha kujifunza ni kwamba,chadema wameamua kwa makusudi kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali

ya Rais Magufuliikiwa ni pamoja na propoganda za kuwa mawaziri wengi wanatoka kwake,lakini ukweli ndio huo.

Katika kitu kizuri alichotuachia Rais mstaafu Kikwete,ni Kwamba akili za kuambiwa changanya na........................
Hhahahhaha
Unataka kudanganya uma?
Karriuki ni mp are hatoki kagera
Philip mpango mgogo hatoki Dodoma
Luhaga mpina msukuma hatoki singer
Sitaki kuendelea kukurekebisha nataka utaje mawazir wasukuma wangapi na wanaotokabkanda ya ziwa wangapi
 
Sioni ukabila kwa hapo,baraza hili limegusa kila kona ya nchi,naamini mawaziri wote wanawatumikia Watanzania bila kujali maeneo wanayotoka.
Lowassa ana ukabila na udini siyo bure
 
Acha aendelee hajui ndio inayo ubomoa chadema watu wameshituka chama cha kasikazini kadri anavyo lopoka ndio jahazi linazidi kuzama kasahau katibu mkuu wake ni msukuma
Watajikuta wanabaki wa kaskazini, mara wa Kilimanjaro, mara wa Hai, na mwisho wa siku watabaki wa Wamachame peke yao yaani Mbowe na Lema
 
Kuna makabila huwa hawana misimamo. Na mara nyingi huwa hawatembelei wanachokiamini
 
Wakiambiwa huyu mzee mgonjwa watu wanabisha eti mgonjwa mpka alazwe muhimbil hawajui kunaugonjwa wake wa kupungukiwa ufahamu
Ufaham wake hauko sawa kwa sasa

Vipi kwani si musukuma???
 
Back
Top Bottom