UK - Ushoga si hoja - ubakaji demokrasi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Yanayojilia hoja za UK kupunguza mkopo tuliozoeshwa kuita msaada wa bajeti kwa Tanzania si ushoga, bali ni ubakaji wa demokrasia nchini. Viongozi waandamizi wa serikali wamekomalia kuongelea ushoga ili kutuyumbisha ukweli wenyewe. Na hata Cameroon ametumia neno la jumla zaidi katika haki za binadamu, na haki za binadamu ni mambo mengi ingawa ushoga laweza kuwa mojawapo. Ukweli kama alivyosema balozi wa UK ukweli wa jambo lenyewe limepotoshwa na wanasiasa kupata mahali pa kusimamia utetezi wa maovu wayafanyayo.
 
Kaka uwezi kutetea chochote kwenye hili ata uje na thread ya maneno matamu kiasi gani, ushoga upo pale pale kaka
 
Kaka uwezi kutetea chochote kwenye hili ata uje na thread ya maneno matamu kiasi gani, ushoga upo pale pale kaka

Hakuna anayetetea ushoga, na mimi nikiwa mmoja wapo ambaye kwa 100% sikubaliani na ushoga.

Cha msingi hawa kuna mambo mengi wanayopima katika haki za binadamu. Na serikali inatumia mbinu kujenga hoja ya utetezi kwa jambo mojawapo ili kutuzipa mwono mpana wananchi. Tusikubali, hakuna wa kutulazimisha ushoga.
Lakini Uingereza isitetereke haki kieleweka kutokana na serikali hii kudidimiza demokrasi na kuvunja miiko ya haki za binadamu kwa kuua watu ovyo na kusuia hazi wa watu kuandamani kwa wanasiasa fulani na wengi kuwa huru kufanya watakavyo na hawakamatwi au kufunguliwa mashtaka.
 
Tumezoea kukurupuka ndio sababu tunapinga pasipo kujua tunapinga nini Ushoga upo na hakuna anaeupinga hapa nchini kilichopo nikutambua uwepo wake hiyo ndio hoja hoja sio kupinga au kukubali mfano uchawi upo lakini serikali haitambui uwepo wa uchawi hiyo haiondoi ukweri tuwape haki zao tutambue uwepo wao ilikama wakibakwa waweze kushitaki kilichopo tunajidai hawapo wakati tunawaona kilasiku na wengine wanachangia kiasi kikubwa sana kutoa huduma kwa jamii na kuchangia pato la taifa niwatanzania wenzetu tuwape haki zao watambulike na kuheshimiwa tuache ushabiki serikali haina dini na maadiri nihiari ya mtu kufuata au kuacha huwezi kushitakiwa kisa hujampisha mkubwa kiti nihiari yako kufuata maadiri au kukiuka wapeni haki zao
 
usilete porojo mkuu cameron kachemka !!!

Wengi hawajapata hapa hoja yangu ni nini. Uingereza inafanya majumuisho ya mambo mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Na katika mengi hayo waandamizi serikalini wamajitahidi sana kuchuja na kuchukua point moja tu ili kutetea na kulinda maslahi yao. Mbona yalipolalamikiwa ya utupaji maiti barabara hawakuja na nguvu kama ya leo? Ushoga na uuaji kipi kibaya zaidi?
 
Tumezoea kukurupuka ndio sababu tunapinga pasipo kujua tunapinga nini Ushoga upo na hakuna anaeupinga hapa nchini kilichopo nikutambua uwepo wake hiyo ndio hoja hoja sio kupinga au kukubali mfano uchawi upo lakini serikali haitambui uwepo wa uchawi hiyo haiondoi ukweri tuwape haki zao tutambue uwepo wao ilikama wakibakwa waweze kushitaki kilichopo tunajidai hawapo wakati tunawaona kilasiku na wengine wanachangia kiasi kikubwa sana kutoa huduma kwa jamii na kuchangia pato la taifa niwatanzania wenzetu tuwape haki zao watambulike na kuheshimiwa tuache ushabiki serikali haina dini na maadiri nihiari ya mtu kufuata au kuacha huwezi kushitakiwa kisa hujampisha mkubwa kiti nihiari yako kufuata maadiri au kukiuka wapeni haki zao

wapewe haki zao au mmepewe haki zenu ? (WEWE NI FULL BROWN SHOGA) USHOGA NI UHALIFU DHIDI YA UBINADAMU...
 
Back
Top Bottom