UJUZI: Nahitaji kufahamu zaidi kuhusu PayPal...

UJUZI: Nahitaji kufahamu zaidi kuhusu PayPal...

Mkuu Mzee wa Rula umesema ABc ukisha nunua master/visa card 20$ haukatwi hela zaidi
Confirm plz maana mm CRDB
Wananikata 23,000/- za online transaction
20,000/- for Mpesa reversal maana huwa na fund kwa Mpesa
500/- ya ATM Na 500/- ya kuuliza salio Kwa Sim BANKING

Duh
Kumbe CRDB wana makato mabaya namna hii?
NBC nao wakoje makato yao?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mi pia ni mtumiaji wa paypal nilijiunga miaka kadhaa iliyopita a/c yangu ni ya kawaida sio ya mwanafunzi lakini sijaona makato km hayo kwa crdb for sure unaweza tembelea web ya crdb angalia tarrifs charges zote zinaonyeshwa humo,kuhusu mtuma thread kwa maelezo zaidi jinsi ya kujiunga km yuko crdb kwa visa/mastercard anachotakiwa kufanya aende tawi lolote aombe form ya Online Purchase Enabling Request au adownload hiyo form ktk web ya crdb then akaijaze na kuipeleka tawi lolote la crdb ili itumwe makao makuu ili wakaactivate kadi yake,ikishakuwa activated sasa anaweza kuisajili ktk paypal baada ya kujaza details zake ktk paypal ataombwa na paypal kuverify kadi yake km ndo yeye mwenye nayo kwa kujaza verification code,kimsingi hiyo verification code ni transanction Id kwani paypal huwa wanafanya sample ya transanction ya Debit kwenye a/c yako ya kiasi kidogo cha pesa lakini baadae huwa wanakirefund.Sasa hii code paypap wakisha kunotify cose kwa email inabidi upige makao makuu ili waweze kukusomea hiyo code kwani inakuwa kwenye statement yako makao makuu na huwa inatumwa kwenye tawi lako monthly hivo tawini kwako hawawezi kuiona at the time makao makuu unaweza kuwasiliana nao kwa no.s 0714-
0789- }197700 na +255222197700
0755-
Kama ukipata ugumu popote usisite kuwasiliana na mimi kwa msaada no zangu 0767992250 ,0784992250 na 0658092250 emai:dkashombo@gmail.com,skype,Tango,Wahatsapp,facebook,Twitter; Kashombo Donasian .heri mkuu

Maelezo makini.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mbona mi sikatwi? crdb hata sh 10 hawakati crdb natumia acount ya mwanafunz

Yaani mm mwezi huu ndo wamenichinja statement ina makato ya 90,000/= for online transaction
Ngoja niwawekee screenshots

Makato.PNG

Maneno matupu hayavunji mfupa

Hii BANK naiama mwezi ujao bra niamie TPB kabisa na hii ni acc ya mwanafunzi eti

attachment.php

c.c chief-mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Yaani mm mwezi huu ndo wamenichinja statement ina makato ya 90,000/= for online transaction
Ngoja niwawekee screenshots

View attachment 107264

Maneno matupu hayavunji mfupa

Hii BANK naiama mwezi ujao bra niamie TPB kabisa na hii ni acc ya mwanafunzi eti

attachment.php

c.c chief-mkwawa
lakni mkuu hayo makato ni malipo ya manunuzi uluyofanya online na sio bank charges kwa ajiri ya online services
 
Ok mkuu paypal kwa uelewa wangu ni mfumo wa malipo ambao inabidi ujisajili baada ya kuwa na kadi yako ya aidha VISA, Mastercard n.k

Mfano ni mimi nilinunua kadi kupitia BankABC kwa $20 ambayo baada ya kununua unaachana na makato mengine yote hadi inapo expire.

Labda kama utakwenda kutoa fedha kwenye ATM utachajiwa Tshs 500.00 kama transcation charge.

Baada ya hapo nikaisajili paypal.

Kwa hiyo paypal ni nini sasa?

Paypal ni kama nikivyosema ni mfumo ambao mtumiaji anabidi ajisali ili aweze kulipia vitu online. Na siyo kulipia tu hata kupokea.

Mfumo huo unamuhakikishia mlaji usalama wa matapeli au hackers. Mfumo huo hautoi details za akaunti yako kwa mnunuaji na hivyo kuepuka madhara yasiyo ya msingi.

Pia mtandao huu kama una compromise na mnunuaji wanaweza kukurudishia hela kama hutapata bidhaa yako.

Lakini ili uweze kuisajili kadi yako inabidi uende kwenye mtandao wao ambao ni www.paypal.com na kujaza details za kadi yako kisha utakuwa unverified member.

Itabidi ulink card yako kwa kui conferm. Hapo ukifanya hivyo watapeleka namba kwenye bank yako na itakubidi urudi kwenye tawi ulilofungulia ili upate namba hiyo na kuja kuijaza na kuwa verified.

Wanafanya hivyo siyo kwa usumbufu bali makusudi maana mtu anaweza akaiba au akaiokota na kuisajili kisha akafanya malipo online kaka kadi ina credit balance. Kwa hiyo namba inapelekwa kwenye tawi ili kama siyo yako watakutambua kuwa siyo yako na hutapewa namba hizo.

Mara ukiwa verified unaweza kununua vitu online kwa salama na haraka.

Mfano umeona kitu mtandao wa ebay ambao mimi ndiyo nilinunua basi unaenda buy now na kisha utatakiwa kulipa kama muuzaji ana support paypal.

Once ukiconferm ni hapo hapo hela yako inakatwa kwenda kwa muuzaji na kisha wanakujulisha kuwa umekatwa kiasi fulani kwa ajili ya kitu ulichokinunua. Charges anakatwa muuzaji wa bidhaa na siyo wewe. Hapo unaepuka mlolongo wa kwenda mabank kama NBC, CRDB n.k kisha kuwa charged hela nyingi kwa ajili ya kutuma fedha hiyo.
Ni nzuri na salama kaka.
Nimevutiwa xana na maelezo yako naomba kujua utaratibu wa upokeaji wa mzigo kwa ujumla kuanzia ukiwa nje na mpaka unakufikia
 
lakni mkuu hayo makato ni malipo ya manunuzi uluyofanya online na sio bank charges kwa ajiri ya online services

Ni kweli ulivyosema hizo transaction sio bank charges bali ni transactions alizofanya online. Haiwezekani hizo charges ziwe kwa akaunti yake tu na wengine tusizione while ni akaunti za bank moja.
 
lakni mkuu hayo makato ni malipo ya manunuzi uluyofanya online na sio bank charges kwa ajiri ya online services

Hizo ni BANK CHARGES zile ambazo nimefanya Online zina neno PAYPAL Angalia hiyo ya chini yake ya 75k
Kwamba mm ni chizi sijui Online Charges zinakuwa Vp na nilizifanya lini?
c.c BobKinguti
 
Last edited by a moderator:
Hizo ni BANK CHARGES zile ambazo nimefanya Online zina neno PAYPAL Angalia hiyo ya chini yake ya 75k
Kwamba mm ni chizi sijui Online Charges zinakuwa Vp na nilizifanya lini?
c.c BobKinguti
Mkuu amini ninachokuambia, hizo transactions ni zile ambazo ulinunua kitu online lakini at that moment akaunti yako haikukatwa na bank system as it supposed to be. So baadae wanapokuja kufanya reconciliation wanakata manually na hapo ndipo utaona narrations zake zipo tofauti na zile zinazopita automatically. Ufafanuzi huu niliupata baada ya akaunti yangu kukatwa helaambazo nilikua sikumbuki ni kitu gani. Uzuri wanakua na details za kila transaction lini ulifanya na iliku ni amount gani! Ni vizuri ukafuatilia kwakua hizi za manual sometimes wanakosea!
 
Hizo ni BANK CHARGES zile ambazo nimefanya Online zina neno PAYPAL Angalia hiyo ya chini yake ya 75k
Kwamba mm ni chizi sijui Online Charges zinakuwa Vp na nilizifanya lini?
c.c BobKinguti
2i21qpt.jpg

​
​Hayo ni maelezo ya CRDB sasa sijui wamenidanganya, naambatanisha na PDF ya tariffs za 2013
cc: chief-mkwawa
 

Attachments

Last edited by a moderator:
mkuu ningar nafkiri we umefunga kazi, sasa bwana njunwa we unaibiwa inabidi uende bank wakurudishie hela zako au wakupe maelezo ni makato ya nini
 
Back
Top Bottom