Fahamu Kuhusu B2B Model katika biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,506
Habari za wakati huu;
Ni matumaini yangu kwamba unaposoma andiko hili na mengine ninayoandika utapata hamasa ya kuingia katika biashara na uwekezaji wa aina tofauti.

Leo nimeleta mjadala mdogo tu unaohusu Modeli ya biashara.Kuna miundo ya B2B na B2C ambapo B2B ni Business to Business na B2C ni Business to Consumer na kuna B2B2C na miundo mingine kama hiyo.Kimsingi unapofanya au kuanzisha biashara yako ni muhimu utambue kwa uhakika iwapo unafanya biashra ya B2B au unafanya Biashara ya B2C hii itakusaidia kutambua wateja wako na kuelewa soko lako na changamoto zilizopo.

Mara nyingi soko la B2C ni soko ambalo linaweza kuwa na ushindani mkubwa na ambalo linaweza kuwa na changamoto katika usimamizi kuliko soko la B2B.Hata hivyo soko la B2C ni kubwa na mtu yeyote anaweza kuwa mteja katika mfumo wa B2C.Mara nyingi mtu anayefanya biashara za B2C huwa anamlenga mlaji wa mwisho ambaye kimsingi huwa anaenda kutumia na sio kuuza wala kuongeza thamani kwa ajili ya kuuza. Mfano mwenye BAR,Mgahawa,Restaurant,Duka la Takataka etc hawa huwa wanamlenga zaidi mlaji wa mwisho na mara nyingi wanaweka bidhaa zao karibu na mlaji wa mwisho.

Mfumo wa B2B ni tofauti na B2C kwa namna ambayo inalenga Mfanyabiashara mwenzako ambaye naye ama huuza kwa mlaji wa mwisho au huongeza thamni kwa kuzalisha bidhaa ya ziada.

Kwa kawaida B2B business ni biashara ambayo ukiweza kuisimamia vizuri inakuwa ni baisahra ya uhakika,yenye faida nzuri na soko la uhakika.

Baada ya utangulizi huu naomba sasa nikupe mbinu na mikakati ambayo inafaa katika usimamizi ha unapotaka kufanya Biashara na Biashara ya mtu mwingine Hizi na hatua za kufuata ili kuweza kufanya biashara na biashara nyingine:

  1. Hatua ya kwanza na ya muhimu ni Kutambua na kujitambulisha: Katika hatua hii unapaswa kufahamu na kuwa na vitu vifuatavyo.
    1. Nyaraka na vibali mbalimbali vya usajili kama Usajili wa kampuni,Kodi,leseni na Vibali vinginevyo
    2. Pili uwe na taarifa ya wasifu wa viongozi muhimu katika kampuni yako
    3. Uwe maelezo ya shughuli za kampuni(Company Profile ambayo itaambatanishwa pamoja na hivyo hapo juu.
    4. Uwe na taarifa za wateja unaotaka kufanya biashara nao kama vile,Aina ya biashara/shughuli zao,Wasimamizi na wamiliki,Mawasiliano ya watu muhimu katika kampuni.
  2. Hatua ya Pili ni kufanya Mawasiliano ya mwanzo na wateja unaotaka kufanya nao:Hapa unaweza kuwatembelea kama mteja kwanza ili ufanye uthibitisho wa bidhaa na huduma zao na pia kuwa na mawasiliano nao na kufahamu zaidi kuhusu huduma au bidhaa zao na mahitaji yao.Hii hatua ni muhimu sana ni zingatia sana uweze kuonana na watu wa muhimu kwa kuwa na mkakati sahihi kabisa wa kukutana nao.
  3. Hatua ya tatu ni kuandaa Proposal:Unapoandaa Proposal ni muhimu kuhakikisha kwamba unazingatia mahitaji ya mteja husika.Hakikisha unaeleza zaidi kuhusu ile bidhaa anayohitaji,hakikisha unaeleza iwapo unatoa credit na ya siku ngapi na kwa masharti gani,eleza pia iwapo una warant zozote,bima au faida za ziada ambazo mteja anaweza kupata kwa kufanya biashara na wewe.
  4. Hatua ya nne ni kuwa na tovuti:Watu wengi huchukulia swala la kuwa na website kwa wepesi kwa sababu ya kutokuwa na mkakati.Ni lazima uwe na mkakati wa website jinsi ya kuitumia kuuza na kuhakikisha kwamba unaweka mawasiliano ya mara kwa mara na taarifa za muhimu kuhusu bidhaa na huduma zako
  5. Hatua ya tano ni kuwa na updates/mawasiliano ya mara kwa mara:Hapa unaweza kuwa unafanya mawasiliano ya mara kwa mara na wateja wako kwa njia ya email,simu na kuwajulisha kuhusu mabadiliko na taarifa muhimu za biashara yako.Unaweza pia kutumia tovuti na mitandao ya kijamii katika kusimamia mwonekano wa bidhaa na huduma hizi.
Haya ni baadhi tu ya maelezo na mikakati ambayo inaweza kutumika kwa ajili ya kusimamia Biashara ya B2B.

Karibu tujadili na kushirikishana mbinu nyingine ambazo unaweza kuzitumia kwa ajili ya kuuza huduma zako.
 
Back
Top Bottom