Ujumbe wanaume walio na ndoa: Wanawake wanavyopambana kujikwamua kiuchumi ndoa nyingi zinazidi kuingia matatizo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,899
155,954
NAOMBA NIONGEE KIDOGO NA WANAUME MLIOOA

(Kopi kwa wanawake wote mlioolewa)

Kadiri wanawake wanavyopambana kujikwamua kiuchumi ndivyo ndoa nyingi zinazidi kuingia matatizoni. Tatizo sio wao kupambana bali tatizo liko hapa:

Wanapambana kwa madhumuni gani? Wanawake wengi hawapambani kwa maana ya kuwasaidia waume zao [kama Mungu anavyotaka] bali kwa maana ya kutoka kivyao; ndio maana utawasikia wanaongea kauli zao za kiuanaharakati, "Usimtegemee mume", "wanaume hawaaminiki", "bora mwanamke niwe na uchumi wangu n.k".

Hivi mnajua kuwa...
Kama mume ni kichwa maana yake mke ni kiwiliwili; bahati mbaya ni kwamba macho na ubongo viko kwenye kichwa na sio kiwiliwili. Kiwiliwili kisipokiamini kichwa "automatic" kitaielekeza miguu kokote na kwa kuwa hakuna macho kuna mawili; mwili(ndoa) kuumia kutokana na kujikwaa ama kufa kabisa kwa kutumbukia shimoni.

Ngoja niwambie; ndoa yeyote ambayo mwanamke amekaa kiuanaharakati uwe na uhakika ilishajifia siku nyingi ama iko njiani kufa na ukiona wanandoa wanaendelea kuishi pamoja basi ujue ni kwa "kujilazimisha". Sijakutana na mwanamume yeyote duniani ambae anaweza kuishi kwa furaha nyumba moja na mwanamke anaeleta tabia za uanaharakati ndani ya ndoa.

Nataka ufahamu...
Ukiruhusu mwanamke ndani ya ndoa ajione anaweza kusimama bila wewe (mumewe) basi, ujue unacheka na nyani na muda wowote tutakuja tukusanye mabua tukalishie ng'ombe wetu. Kuishi na mke hakuhitaji DEMOKRASIA, kunahitaji AKILI, ujinga unaofanywa na wanaume wengi siku hizi ni kuruhusu DEMOKRASIA kutawala ndoa badala ya AKILI. Wewe kama unadhani demokrasia ndio uzungu na mapenzi kwa mkeo, shauri yako; hao wazungu unaowaigilizia ndoa zishawakimbiza siku nyingi.

Msifanye mchezo wandugu...
Ninawaonya mapema ili nisije kusikia eti mtu ananiambia mke aliemtafuta na kumuoa mwenyewe, amemshinda! Khaa! Yaani hapo itabidi utandikwe viboko vya mgongo; maana unakuwa umemdhalisha Mungu na umeudhalilisha uanaume pia. Uanaume tafsiri yake ni "Kuishi na mwanamke kwa akili kiasi kwamba abaki akikuheshimu na kukunyenyekea kwa furaha". Ukiona mwanamke anakudharau na hakusikilizi basi ujue umeshapoteza uanaume wako.

Andika hii pointi mahali...
Elewa kwamba uanaume haukai kwenye suruali bali uanaume unakaa kwenye akili.
 
Umenena vyema,ndo maana babu yuko pale kijijini ana wanawake 8 lakini wanamtii na kuheshimu kumbuka babu hajawahi kuhudhuria hata chekechea lakn kuna mwanaume kasoma vizuri lakn kaweka democrasia katika ndoa inamshinda.Ndo yale umeoa mke amekuta umejenga siku mnaacha mnauza Nyumba mgawane hii ni baada ya kugundua wewe ni mpenda democrasia lakini kama anajua wewe unatumia akili na democrasia katu huu upuuze hata ujadili,Maana anakujua fika wewe ni nani.
 
Shida ni moja tu.wanawake wengi wakiweza kujitegemea kwa maana ya kujilisha,kujivisha na hata mahala pa kulala hua hawana moyo kama wa kwetu wa uvumilivu na kujitoa.wanavaa dharau,kujisifu,kashifa na kuzua uhuni wa kingono nje na mumewe.wanajua sana kubeba ujuaji pindi wanapofanikiwa.mwanamke anaekaa nyumbani hata akiwa muhuni hutajua lakini mala nyingi utamkuta ni mwenye nidhamu sana na hofu ya MUNGU pia.hawakuumbwa na uwezo wa kuhimili kumtunza mwanaume maisha yake yote iwapo mwanaume hana kipato,watazua kila aina ya kero ndani ya nyumba.kwangu mimi mwanamke wa nyumbani cha kwanza ni mwenye kuelimika lakini aweze kuheshimu ndoa na mume kwa kiwango kikubwa.atakaa nyumbani kuangalia watoto na yale yote ya kuifanya nyumba ionekane ina watu then mimi kama mimi mwanaume ndo ntaingia mtaa kwa mtaa na kuhakiki familia inakwenda vyema kimaisha.sema tu nitahakiki mwanamke anjua ninafanya nini na nitaweka mazingira hata ya kibiashara ambayo si atashughulika nayo ila atayajua kwa dharula ya kesho na kesho kutwa kama sipo aweze kunyanyuka ili watoto waishi.lakini kama bado nipo na nina nguvu basi mwanamke ni ndani ya geti.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Wanaume tumekuwa wastaarabu kupindukia kwa wake zetu kiasi kwamba wanawake wanatudharau sana.
Demokrasia ya ndoa tuliyoletewa na wazungu haitajiki kabisa kwa wanawake wa kitanzania.
Ndoa zetu bila udikteta hazifiki popote. Ila uwe udikteta wa akili na sio manyanyaso na vipigo kwa wanawake.
umeongea point sana.. mkuu
 
NAOMBA NIONGEE KIDOGO NA WANAUME MLIOOA
(Kopi kwa wanawake wote mlioolewa)
Kadiri wanawake wanavyopambana kujikwamua kiuchumi ndivyo ndoa nyingi zinazidi kuingia matatizoni. Tatizo sio wao kupambana bali tatizo liko hapa: wanapambana kwa madhumuni gani? Wanawake wengi hawapambani kwa maana ya kuwasaidia waume zao [kama Mungu anavyotaka] bali kwa maana ya kutoka kivyao; ndio maana utawasikia wanaongea kauli zao za kiuanaharakati, "Usimtegemee mume", "wanaume hawaaminiki", "bora mwanamke niwe na uchumi wangu n.k".
Hivi mnajua kuwa...
Kama mume ni kichwa maana yake mke ni kiwiliwili; bahati mbaya ni kwamba macho na ubongo viko kwenye kichwa na sio kiwiliwili. Kiwiliwili kisipokiamini kichwa "automatic" kitaielekeza miguu kokote na kwa kuwa hakuna macho kuna mawili; mwili(ndoa) kuumia kutokana na kujikwaa ama kufa kabisa kwa kutumbukia shimoni.
Ngoja niwambie; ndoa yeyote ambayo mwanamke amekaa kiuanaharakati uwe na uhakika ilishajifia siku nyingi ama iko njiani kufa na ukiona wanandoa wanaendelea kuishi pamoja basi ujue ni kwa "kujilazimisha". Sijakutana na mwanamume yeyote duniani ambae anaweza kuishi kwa furaha nyumba moja na mwanamke anaeleta tabia za uanaharakati ndani ya ndoa.
Nataka ufahamu ....
Ukiruhusu mwanamke ndani ya ndoa ajione anaweza kusimama bila wewe (mumewe) basi, ujue unacheka na nyani na muda wowote tutakuja tukusanye mabua tukalishie ng'ombe wetu. Kuishi na mke hakuhitaji DEMOKRASIA, kunahitaji AKILI, ujinga unaofanywa na wanaume wengi siku hizi ni kuruhusu DEMOKRASIA kutawala ndoa badala ya AKILI. Wewe kama unadhani demokrasia ndio uzungu na mapenzi kwa mkeo, shauri yako; hao wazungu unaowaigilizia ndoa zishawakimbiza siku nyingi.
Msifanye mchezo wandugu..
Ninawaonya mapema ili nisije kusikia eti mtu ananiambia mke aliemtafuta na kumuoa mwenyewe, amemshinda! Khaa! Yaani hapo itabidi utandikwe viboko vya mgongo; maana unakuwa umemdhalisha Mungu na umeudhalilisha uanaume pia. Uanaume tafsiri yake ni "Kuishi na mwanamke kwa akili kiasi kwamba abaki akikuheshimu na kukunyenyekea kwa furaha". Ukiona mwanamke anakudharau na hakusikilizi basi ujue umeshapoteza uanaume wako.
Andika hii pointi mahali..
Elewa kwamba uanaume haukai kwenye suruali bali uanaume unakaa kwenye akili.
Aiseee kula like hapa ndio tunapofelii most of me
 
Back
Top Bottom