Ujumbe wa Simu Wasababisha Kifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wa Simu Wasababisha Kifo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Jan 3, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Jan 3, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Joyce Emmanuel [25] mkazi wa Tabata Kimanga amefariki dunia baada ya kunywa sumu ya panya kutokana na ujumbe wa simu aliotumiwa na mumewe.

  Mume wake alitumiwa ujembe huo na mtu asiyemjua na yeye akamtumia mkewe ,Ujumbe huo ulisomeka : " Mwambie mkeo aache kutembea na waume za watu kama wewe humtoshelezi basi mtafutie mwanaume mwingine akusaidie lakini sio mume wangu " ulimalizia ujumbe huo.

  Source: Nifamishe
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duuu??? ndiyo maana tunashauriwa daima tushirikishe watu japo mmoja katika mambo yanayo tutatiza kimaisha. Huyu marehemu dada Joy angepata nafasi ya kumsimulia binadamu mwenzie asingefikia uamuzi huu wa kujichumia dhambi ya kujiondolea uhai!
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Yawezekana Marehemu alikuwa Mzinzi na hiyo sms was "the last nail" kwenye JENEZA. Kama sms pekee inatosha kukatisha uhai wake mostly likely alikuwa akipewa pesa ya matumizi ndogo anaamua ku-supplement na waume za wanawake wenzie huko mitaani...

  KUJIUA NI DHAMBI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inawezekana pia kwamba pesa ya matumizi ilikuwa kubwa kwa hiyo anaamua ku-share na wanaume za wanawake wenzie huko mitaani...
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Inawezekana huyu aliona ameumbuka; kama ungekuwa uzushi, ni dhahiri angeukana.
   
 6. S

  Stone Town Senior Member

  #6
  Jan 5, 2009
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari za wakati huu.

  Sijui marehemu aliharakia nini kujiondosha duniani lakini pengine khofu ya bwana wake ndio umemfanya ajimalize kabla ya kuulizwa maswali lakini kwa kweli amechukua uamuzi wa haraka na ni mbaya wa kujidhulumu roho na nafsi yake bure nafuu angesubiri kitakachomtokea na kuweza kujitetea may be angesalimika kutokana na utetezi wake.

  amechukua maauzi ya haraka ambayo hana tija katika uhai wake wa huko anakokwenda mungu amrehemu na msamehe kutokana na makosa yake
   
 7. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huyu Mwanamke aliishi vizuri sana na mumewe mara nyingi sana amekuwa akimwachia mkewe atumie gari na yeye mume akawa anatumia piki piki. Na bila shaka alikuwa akiwezeshwa sana kifedha. Ilikuwa ni familia iliyotulia na kuwa kama mfano wa kuigwa lakini kumbe mwanya huo mwanamke aliutumia kuvunja agano. Alikuwa mara nyingi kama bibie fulani very serious kumbe nyuma ya pazia hilo akikodolea macho waume za watu. Baada ya kuupata ujumbe toka kwa mke wa mtu akilalamikia tabia ya mkewe kutembea na mumewe, mwanaume aliu-forward kwa mkewe kisha mumewe alirudi nyumbani na kumuuliza kwanini imekuwa hivyo. Baada ya hapo mwanaume aliondoka zake na kuelekea kusikojulikana ndipo huku nyuma mwanamke akaamua kunywa "nauli" ya kwenda mbinguni. Nyumba zetu zina kuta nne na kila nyumba inakelele zake kujulikana hadi yatokee mambo kama hayo kunahitaji kelele za ziada kama siyo kifo.
   
  Last edited: Jan 6, 2009
 8. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyu dada nafikiri sababu siyo SMS ana mambo mengine ya ziada. Hivi kweli katika ulimwengu huu kuna kitu kinachoweza kukusababisha wewe kutoa uhai wako bila sababu?

  Watu tunafiwa na watoto wetu bado tunaomba mungu atupe faraja inazoeleka. Nafsi imekalia vibaya baada ya kuona mumewe kajua.

  Hizi tabia siyo nzuri, we should learn how to communicate, kama unataka kitu fulani toka kwa mumeo/mkeo ambacho hafanyi na unakihitaji kaeni kama kamati kujua mfanyeje, siyo kila kitu tunajua mengine tunajifunza kutokana na matakwa ya familia/au mwandani wako.

  Mawasiliano ndaniya familia ni mazuri sana
   
Loading...