Ujumbe wa leo kwenye katuni

Ujumbe wa leo kwenye katuni

Kipanya ukweli Sana .
Lowassa Hana Mvuto hata chembe, anazidi kunyauka tu UKAWA.
Naamini atafanya maamuzi sahii na kurudi CCM kuwaita mwanachama Safi.
Maana sikuhizi ufisadi hauna nafasi CCM.
 
Kuna hoja ya msingi kwenye hii picha. Kwanza mchoraji kaathiriwa na Propaganda kwamba Lowassa ametumia fedha "nyingi" katika kujijenga kisiasa, na kwa mtazamo wake mvuto wa kisiasa ni kuwa na madaraka. Lakini ajiulize ni kwa nini hao wanaoonekana kwamba wana "mvuto" wanatumia watu wengi tofauti tofauti kupambana na huyo asiye na mvuto?

Kwa mfano ni lini Lowassa ataruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa bila ya kubughudhiwa na Polisi? Mvuto wa Lowassa ni kuandikwa na vyombo vya habari kila siku au kuwa na watu wanaomuunga mkono hata kama haandikwi na vyombo vya habari? Leo hii Lowassa akienda kwa mfano Hospitali ya Muhimbili kutembelea wagonjwa kitatokea nini?

Huyu asiye na mvuto ndiye huyo kuchorwa kwake kumekuwa habari ya kuja kuletwa JF, kwa nini? Kwani kipanya tangu mwezi huu uanze kachora watu wangapi na kwa nini vikaragosi vya watu hao havijaletwa JF?
 
Maana sikuhizi ufisadi hauna nafasi CCM.
Nyie nanyi kwa mbwembwe! CCM gani unayoisema wewe ambayo ufisadi hauna nafasi? Hayo majipu yanayotumbuliwa kila siku yana uhusihano (Connection) na viongozi wa CCM. Kwa taarifa yako kila hayo mnayoyaita majipu yanapotumbuliwa, chanzo chake huwa ni viongozi wa CCM!!
 
Njaa mbaya sana anatafuta ukuu wa wilaya huyu,siku hizi anapigwa fimbo na kina Bonda.
 
Msinichekeshe mimi. Tanzania ina matatizo makubwa ambayo yanahitaji ufumbuzi. Mm nawashangaa Wana ccm. Hivi kwani mliambiwa adui mkuu wa nchi hii ni lowassa. Kwa uelewa wangu mdogo nchi hii ina maadui watatu. Ujinga, maradhi na umasikini. Kwa ushauri wangu mngeanza na maadui hawa watatu ndo muanze kumsakama lowassa wa watu. Nchi imewashinda mnaanza majungu. Mm nilidhani ile slogan yenu ya HAPA KAZI TU mtaitumia kwa vitendo ili watanzania warudishe imani kwenu. Na wa ambiance kitu kimoja. Kama siku mkijiloga mkawapa nchi wapinzani, hamtarudi madarakani maana naamini watafanya maendeleo ambayo nyie yamewashinda



Nchi itushinde, kongoni mtabaki mahala gani sasa
 
WEWEEEE LOWASSA SIO WA HIVYO HATA SIKU 1, ungemjua usingepost umbea umbea wa magazetini.

Ongezeni nguvu za kuiba kura na kuipa ushindi wa goli la mkono CCM kule zanzibar.
Hivi umeelewa hiyo picha au umeitafsiri kama ilivyo?
 
Nyie nanyi kwa mbwembwe! CCM gani unayowe ambayo ufisadi hauna nafasi? Hayo majipu yanayotumbuliwa kila siku yana uhusihano (Connection) na viongozi wa CCM. Kwa taarifa yako kila hayo mnayoyaita majipu yanapotumbuliwa, chanzo chake huwa ni viongozi wa CCM!!

Unaanza kuleta History sasa.
CCM haifugi mafisadi anymore, hiyo tabia tumewaachia CHADEMA na mafisad wote sisi tunawaadhibu.
Ndo maana nimetoa wazo EL akirudi ccm ajue kabisa nafasi ya Ufisadi haipo kabisa huku kwetu.
CCM mpya mbele kwa Mbele
 
Msanii maarufu Masoud kipanya katika ujumbe wake wa katuni amemtaka Lowasa aachane na siasa kwani hana mvuto tena.Ujumbe wake huu hapa

luwasa-jpg.332577
 
Back
Top Bottom