Ujumbe wa kutafakari usiku huu: Fanya hima, tengeneza mahusiano mema na ndugu au wazazi wako ili baraka zako zisizuiliwe

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Habari za wakati huu ndugu zangu!

Nina ujumbe muhimu sana kwetu sote!

“Je, mnaona jinsi tulivyo na UPENDO na Maelewano humu tukiwa tumetawaliwa na Vicheko, heshima pamoja na Furaha?

Vivyo hivyo, tuhakikishe kwa Familia zetu tunakuwa hivi hivi.

Wako watu humu ambao hawana mawasiliano mazuri na wazazi au ndugu. Fanya hima, tengeneza na ndugu au wazazi wako ili baraka zako zisizuiliwe.

Hata kama wao ndio waliokukosea au wasiokuhitaji, jitahidi kutengeneza upande wako na uwatangazie MSAMAHA na kwa hakika mtaona mambo yenu yakiwaendea vizuri.

Chukua hatua, watembelee kama wapo karibu au wapigie simu kama wako mbali.

Nimeguswa tu kuwashirikisha ujumbe huu muhimu kwetu sote.

Nawashukuru ndugu zangu na MUNGU atubariki sote
 
Back
Top Bottom