Ujumbe toka udsm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe toka udsm

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Feb 1, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  TUAMKE JAMANI TUSILALE, MAPAMBANO BADO........
  Napenda kwanza kutoa shukurani zangu za dhati kabisa kwenu ninyi wanachuo wenzangu kwa mshikamano mliouonyesha kipindi chote cha mapambano dhidi ya sera kandamizi na dhalimu ya uchangiaji wa elimu ya juu. Hii inadhihirisha wazi ni jinsi gani tulivyo wazalendo na kuonyesha ukomavu wa kifikra katika kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya Taifa letu. Nawahakikishieni ndugu zangu anayedhania mabadiliko ya kweli yatatokea kwa kuibembeleza serikali ajue anakosea sana. Naimani wengi wetu tumerudi salama chuoni, poleni kwa matatizo yote yaliyotusibu kwa kipindi chote tulichokuwa uraiani naaimani kila mmoja wetu amekuwa barozi mzuri katika kuuelimisha uma wa watanzania kuelewa kiini hasa cha tatizo ni nini. Hatuna sababu yoyote ile ya msingi ya kujilaumu kwa mgomo wetu, kwani tulikuwa tunapigania mustakabari wa maisha ya watanzania masikini na mabadiliko kidogo tumeyaona ingawaje hatujafikia lengo letu. Cha kusikitisha labda ni wenzetu waliopoteza maisha katika ajali ya basi kule singida, ambapo baadhi yetu pia walipata majeraha. Mwenyezi mungu awarehemu na zawadi pekee tuliyonayo kwao ni kufanikisha vita hii tuliyoianza pamoja. Kilicho mbele yetu hivi sasa ni kuendeleza wimbi la mapambano tena safari hii ajenda zetu za msingi ni kuuondoa utawala wa kisiasa chuoni, kurejesha wenzetu chuoni, kupigania muhimiri wetu DARUSO pamoja na kuizika na kuitokomeza kabisa sera ya uchangiaji. Wakati huu ni wa pekee katika historia ya nchi yetu ambapo vijana hasa wasomi ni nguvu ya mabadiliko, tukikaa kimya historia hii ndugu zangu itatuhukumu. Najua wengi wetu sasa hivi tumejawa na roho za uoga wa kinafiki, lakini jua kabisa fika hiyo siyo sirika ya msomi tena wa chuo kikuu mlimani ambayo ni uwezo wa kuhoji yanayokubalika na kukataa vitu vya kishenzi vilivyozoeleka na visivokubalika mbele ya wapigania haki. Kwa sababu tunapokataa tunajenga hoja ya msingi kuonyesha jinsi gani hatukubaliani na maamuzi yanayofanywa kisiasa zaidi na kutukandamiza sie wanafunzi. Wote tunakumbuka fedha ya matibabu iliunganishwa kwenye ada ya mwanafunzi kwa mwaka wa masomo wa jana (2006/07) na tukatangaziwa na huyo Mkaliandara pale Nkrumah, na hata mwaka huu wa masomo kabla ya chuo hakijafungwa ilieleweka hivyo, lakini sasa tumelazimishwa kulipia gharama za ziada shilingi 50,000 eti za matibabu. Jamani hela zetu hizo ndizo zilikuwa zikitumika kujaza mafuta ya AURORA za Mkaliandara, kuwalipa wale washenzi FFU na kulipa allowances za kina BUSH pale getini geti maji. Leo ni wiki ya tatu tangu chuo kifunguliwe mpaka hivi sasa watu hatuna pesa sababu eti bado wanaendelea kuprocess kutokana na batch za malipo, tena wengine wanawekewa laki tatu, wengine laki nne na wengine laki sita au siku hizi kwenye bum kuna grade?. Huo ndiyo wizi tunaoukataa jamani tukigoma wanatuita wahuni, tusipokuwa makini fedha zetu hizi zitakuwa zinafisadiwa, kuna umuhimu wa kuipigania DARUSO yetu. Leo hii tumerudi chuoni mtu ulikuwa na chumba awali na ulikilipia semistor nzima, lakini sasa hivi unanyang’anywa tena bila kulipwa hata fidia anapewa mtu mwingine ambaye alikuwa hana chumba kisa umechelewa kulipa, kweli hiyo ni haki?. Sisemi mliopata mnyang’anywe ila tulipwe tulionyang’anywa. Bei ya vitu zimepanda maradufu si cafteria wala stationary tena hawana huruma kabisa wanadai mambo yamebadilika, je hayo mambo mbona hayakubadilika awali yabadilike leo hii kisa hatuna uongozi wa DARUSO? Tunakatazwa tusibebane tena kwa kukaguliwa kwa usumbufu mkubwa na wafanyakazi wa ofisi ya dean of students usiku wa manane, kweli hiyo ndiyo kazi ya mlezi na bila kubebana tutaweza kuishi ndugu zangu? Tujiulize kwa nini cafteria ya DARUSO imevunjwa? Eti kwa sababu mapato yake yanaingia DARUSO ndiyo yanatupa kiburi sie wanafunzi kugoma tena huyo ni proffesor mzima ndiyo anachangia hoja hiyo kwenye panel badala ya kuainisha kiini cha tatizo. Kweli huku ni kufirisika kimawazo kwa uongozi wetu wa chuo na kuzidi kutawaliwa na fikra za kisiasa. Ndugu zangu kisheria udahili wetu haukufutwa sie bado ni wanafunzi halali wa chuo kiku cha Tanzania, registration number zetu ni zile zile, matokeo yetu ni yaleyale yanaendelea kutumika, iweje leo sasa uniambie eti viongozi wetu wamepoteza sifa za kuwa viongozi kisa tumedahiriwa upya. Huu ni wizi mtupu na propaganda za kisiasa za ndugu yetu Mkaliandara, suala la kutengenezewa vitambulisho vipya lilikuwa ni la lazima ili kurekebisha expiring date na ndiyo maana tarehe ya kuexpire ni sawa kwa wanafunzi wote, na mtakaobakia chuoni mtarudishiwa vitambulisho vyenu vya zamani. Ndugu zangu wasomi haya yote yanafanyika kwa sababu hatuna chombo chetu cha kututetea, huu tena siyo wakati wa kuogopa ni kusimama imara na kupigania kuirudisha madarakani serikali yetu ya DARUSO. Tukulifanikisha hilo wale wenzangu na mimi tuliyonyang’anywa vyumba tutalipwa peza zetu pamoja na fidia juu kwa sababu wametusitishia mkataba ghafla bila kupewa notes, fedha za matibabu zitaeleweka tulizichangia kwa msingi ipi? Na hizo cafteria na stationary ambao wamiliki wake ni wao wenyewe watatueleza ni kwa nini wamepandisha bei ya vitu hovyo? Na itawezesha pia wenzetu walioko nje kwa ajili ya umasikini wetu wanarudi chuoni haraka iwezekanavyo pamoja na mwanaharakati, mpambanaji, ndugu yetu mpendwa na mtetezi wa haki za masikini raia wa Uganda Silas Kefar Odong Odwar ambaye alifutiwa kibali cha kuishi nchini kwa propaganda za kisiasa na kuondolewa nchini mara moja anaungana nasi. Tusipokaa chini na kubadili mwelekeo wa fikra zetu hivi sasa, tutajikuta tumepelekwa tusikotaka kwenda na tusijue tumefikaje huko, kwa pamoja tunaweza “The greatness of our survival here at the hill is not a given we must fight for it and solidarity will be only our truly mace” Aluta continua vita bado inaendelea tusiogope tuimarishe ushirikiano wetu tukutane REVOLUTIONARY SQUARE kwa mikakati zaidi nchi hii ni yetu lazima tuipiganie.Ni mimi mtoto wa masikini tuwasiliane kupitia masikinitz@yahoo.com
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ahh Shy tangu lini wewe ulikuwa mtoto wa maskini?
   
 3. johnj

  johnj Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  nafikiri shy ametumika tu kama daraja !
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  It doesn't matter kama shy ni mtoto wa masikini au laa....cha msingi ni ujumbe aliouweka hapo!

  Hii misukosuko ya Mlimani, binafsi inanikera sana sana tu! Hivi ebu mwenye updates za UDSM, atuambie; walio vijana 2000 mustakabali wao ukoje? je na DARUSO? Wanafunzi waliorudishwa hapo nini kinaendelea? je, UDASA nao madai yao yametekelezwa au longolongo tu?
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbona hamna anayeleta updates on this, mliyoko Dar vipi hapa?
   
 6. M

  Mwanazuoni Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UDSM hali ya chuo ika kama kawaida. wanafunzi wanasoma na hata test wameanza kufanya kwani wamendelea wiki ya saba ya masomo.kama umesoma media, idadi ya wanafunzi wanasemekana kujifukuzisha chuo kwa kutokujaza dorms imekua 143....bado sijui details za wale walioambiwa wamefukuzwa kwa kuwa vinara wa migomo. Udasa siku hizi haina nguvu yoyote. inaongea tu na hakuna anayesikiliza au kuogopa. si ajabu nao vingozi wake ni sehemu ya system iliyotawaliwa na siasa hasa mwenyekiti wao. wao huwa wanajadili vitu baada ya madhara kutokea tena yanapwagusa wao zaidi.
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Thanks for this,

  Mwnyekiti wa UDASA ni nani sasa hivi? Nakumbuka wakati wa uhai wa Prof. Sethi Chachage Sethi ndiye alikuwa mwenyekiti kwa kipindi fulani,na UDASA ilikuwa na msimamo wa hali ya juu sana!
   
 8. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti wa sasa wa UDASA anaitwa Dr. D. L. Nyaoro
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Thanks kijana......!

  Lakini huyu jamaa simfahamu vizuri, anyone with his good CV?
   
 10. M

  Mwanazuoni Member

  #10
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani yuko Civil Engeneering. Nina habari kuwa ana kampuni ya ujenzi ambayo inapata sana tenda za serikali kwa hiyo hawezi kusimama kidete kama mwenyekiti wa UDASA kinyume na serikali
   
 11. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huo ndio uozo wa wanazuoni wetu, UDSM imegeuzwa kwa maksudi na kuendeshwa kisiasa! Ni taifa la watu gani tuliandaa? hata vijana wetu, ambao tunawaandaa kuwa wataalam wabadae tunaendesha mambo yao kisiasa? too tired!
   
Loading...