Ujumbe mzuri

Ujumbe mzuri

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,175
Reaction score
829,138
Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*

*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*

*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.*

```Ujumbe huu mzuri umfikie kila mmoja wetu katika familia yake.

Jr
 
Shukrani sana mshana, ukiacha uchawi una nondo sana zinazogusa.
I am working on this everyday, ila as you said hatujakamilika mara kwa mara tunajikuta tumeteleza. Kuna nguvu kubwa ktk MSAMAHA kiimani na kijamii pia.
 
Ujumbe huu nitaufikisha ndani ya familia yangu ukiwa kwenye hard copy - thank you bro Mshana Jr.
 
Ahsante sana comrade,ujumbe umenifikia na nimeupokea pia nami nitawafikishia na wengine iwe sadaka kwangu na kwako
Mola akujaalie ktk yenye kheri,furaha na mafanikio ktk mwaka huu na mingine iliyobaki ktk uhai wako
Ameen
 
Shukrani sana mshana, ukiacha uchawi una nondo sana zinazogusa.
I am working on this everyday, ila as you said hatujakamilika mara kwa mara tunajikuta tumeteleza. Kuna nguvu kubwa ktk MSAMAHA kiimani na kijamii pia.
Tatizo langu kubwa ni kusahau aisee, yaan mi huwa sisahau baya lolote nalotendewa, hadi leo hii nayakumbuka mabaya yote niliyotendewa na watu mbalimbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom