Ujumbe kwako wewe mwanaume wa leo, mwanaume mramba lipsi, mwanaume mrembuaji, mwanaume unae amini eti mabadiliko ya sayansi na technologia yatakubadilishia maisha yako (sayansi na technologia scam tu kama scam nyingine) 👊
Hebu sikia!!!... Mwanaume wa kweli hapaswi kujilegeza, kuzubaa zubaa tu (hasa wale wanaojitia wasomi, eti wafanya biashara).. Jifunze ujuzi wa mikono — hata kama ni kujenga banda la mifugo, kupiga plasta, kushika nyundo au kurekebisha vitu vidogo nyumbani. Haya mambo ni muhimu sana na ni sehemu ya maisha.
Inasikitisha kuona mwanaume mzima anamwita fundi aje kumfungia pazia. Kila kitu simu kwa fundi (halafu sasa sio fundi ni mtu tu wa mtaani). Mtoto akiharibu kitu kidogo ndani ya nyumba, suluhisho ni simu kwa fundi. Sasa watoto wanajifunza nini kutoka kwa baba wa namna hiyo?
Uanaume sio kuvaa vizuri na kupost picha mtandaoni (tena inasikitisha sikuhizi wanaume mnarembua na kuramba lips) au kujitia unajua kuongea vizuri na kupangilia maneno. Ni uwezo wa kusimama kwenye majukumu, kutatua changamoto na kuwa msaada kwa familia yako.
Wanaume wa zamani walilea familia kwa kutumia akili, nguvu na ujuzi wa mikono. lakini wanaume wa sasa wanakimbia majukumu ya msingi kwa kisingizio cha usomi, utajiri na techologia, hii tabia ikiendelea tutajikuta tunazalisha kizazi tegemezi.
Kushika nyundo sio fedheha wala aibu. Kujifunza kazi ndogo ndogo au kazi za mikono sio kushuka hadhi. Mwanaume anayejitambua anajua kufanya kazi ndogondogo za mikono na anjifunza kila ujuzi mpya.
Tuache uvivu wa kujifunza kazi mikono. Maana hiyo ndiyo asili ya Uanaume sio kuwa na maneno mengi, kufanya ngono hovyo na kushinda tiktok, facebook au instagram kwa kujifanya content creator. AMKA MWANAUME